TAARIFA KAMILI KUHUSU WALIOFUNIKWA NA KIFUSI MKOANI SHINYANGA!
Eneo la
machimbo ya madogo ya dhahabu ya kijiji cha Kalole kata ya Runguya
tarafa ya Msalala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Mpaka
sasa inadaiwa wachimbaji wadogo wadogo 20 wa dhahabu wamefariki dunia
baada ya kufunikwa na kifusi kufuatia wa mvua zinazoendelea kunyesha na
kusababisha kubomoka kwa mashimo hayo katika machimbo madogo ya dhahabu
ya kijiji cha Kalole kata ya Runguya tarafa ya Msalala wilaya ya Kahama
mkoani Shinyanga.
Kwa
mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha amesema
waliofariki dunia ni watu 19 ambapo usiku wa kuamkia leo kuna wachimbaji
ambao walivamia machimbo hayo ambayo yalishaachwa kuchimbwa muda mrefu
na ndipo wakaanza shughuli ya uchimbaji kutokana na machimbo hayo
kuonekana kutokuwa imara na mvua iliyokuwa ikinyesha ndipo mashimo hayo
yakabomoka na kuwafukia na kusababisha vifo vyao.
Baadhi ya duara ya simo la kuchimba dhahabu katika kijiji cha Kalole wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Comments
Post a Comment