MENGI NA MKEWE KYLN WALIVYO FUNGA NDOA YA KIHISTORIA


Mr and Mrs Mengi wakiwa na furaha siku ya Ndoa yao

Mimi Dr. Reginald Mengi naahidi kumpenda Jacqueline Ntuyabaliwe katika shida na raha hadi kifo kitutenganishe
Ilikuwa ni furaha, upendo wa dhati na shangwe pomoni.
Baada ya miaka kadhaa ya uhusiano thabiti na uliokuwa umetawaliwa na upendo usio kifani, Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Limited, Dr. Reginald Mengi na Miss Tanzania, 2000, Jacqueline Ntuyabaliwe wamefunga ndoaWawili hao wamebahatika kupata watoto wawili mapacha pamoja. Watoto hao wa kiume nao waliungana na wazazi wao kushuhudia wazazi wao wakibadilisha viapo vya ndoa.

Watoto mapacha wa Dr. Mengi na K-Lynn wakiwa wamebeba pambo maalum lililoandikwa maneno ya Kiingereza yanayomaanisha ‘Karibu Bibi Harusi’
Dr. Mengi na Jacqueline anayefahamika pia kwa jina la K-Lynn, walifunga ndoa mwishoni mwa mwezi uliopita katika harusi iliyofanyika nchini Mauritius.

Bibi Harusi Jacqueline Ntuyabaliwe akitembea kwa hatua za kinyonga kujongea mbele ya mashahidi na tayari kwa kusema ‘Yes I do’
Harusi hiyo ya aina yake ilihudhuriwa na watu takriban 50 ambao wengi wao ni ndugu na marafiki zao wa karibu.
Mr. and Mrs. Mengi wakiwa kwenye picha ya pamoja na wana familia wa pande zote mbili. Nyuso hizi zinaonesha furaha ilivyotawala sherehe hiyo

Mr and Mrs Reginald Mengi wakiwa na nyuso za furaha pamoja na watu wao wa karibu
Ndoa hiyo imefungwa ikiwa ni miezi minne tu baada ya Mengi kumchumbia rasmi Jacky kwenye sherehe ya siku yake ya kuzaliwa (K-Lynn) iliyofanyika December mwaka jana mjini Dubai.

Dr. Mengi na mke wake Jacqueline wakiwa wamewashika mikono watoto wao mapacha wakati wakitembea kwenye moja ya fukwe za bahari ya Hindi nchini Mauritius ilikofungwa ndoa yao
Kwa mujibu wa watu wao wa karibu waliohudhuria, sherehe hiyo ilitawaliwa na furaha ya hali ya juu.

Dr. Reginald Mengi akimsaidia mke wake Jacqueline kukata keki ya harusi

Bibi harusi, Jacqueline na marafiki zake wa karibu wakiwa kwenye furaha kubwa baada ya kiapo cha wanandoa
Congratulations to the newlyweds!

Comments

Popular posts from this blog