ACHANWA NA NYEMBE NA KUTEMBEZWA UMBALI WA MITA 300 BILA NGUO UKO KIHONDA- MOROGORO
Aliyekatwa nyembe.
MWANAMKE mmoja,
Rehema Juma (21) ambaye ni mke wa mtu, mkazi wa Mtaa wa Msamvu B, Kata
ya Kihonda Maghorofani mkoani Morogoro amechanwa na nyembe mwilini na
baadaye kutembezwa bila nguo mtaani mchana kweupe akituhumiwa kufumwa na
mume wa mtu.Tukio hilo la aina yake ambalo lilivuta umati mkubwa, lilitokea Julai 5, mwaka huu saa 10 jioni katika Mtaa wa Msamvu B.Mashuhuda
wa tukio hilo walipohojiwa na paparazi walidai kuwa kwa muda mrefu,
Zaitun Ally (30) ambaye pia anaishi kwenye mtaa huo alikuwa akimshutumu
Rehema akidai anatembea na mumewe, hivyo akaamua kutega mtego bila
mafanikio.“Zaituni
baada ya kushindwa kuwanasa leo aliamua kumuita Rehema nyumbani kwake
na kudai amewafuma na mumewe hivyo kumchana nyembe baadaye kumvua nguo
na kumtembeza bila nguo mtaani hadi nyumbani kwake umbali wa mita 300
mchana kweupe,” alisema mmoja wa mashuhuda hao aliyejitambulisha kwa
jina la Ashura Ally.
Paparazi alifika nyumbani kwa Rehema na kumkuta akiwa amefungwa bendeji sehemu za mwili wake na alipoulizwa alifafanua:
“Ni kweli tukio hilo limetokea lakini siwezi kuzunguma peke yangu, twende kwa mama mkwe Mtaa wa Ngerengere.”
paparazi
na Rehema walipofika kwa mkwe wa mtuhumiwa, Lilian Julius Sechonge
ambaye ni mjumbe wa serikali za mtaa wa Ngerengere na kutakiwa
kuzungumzia tukio hilo alikuwa na haya ya kusema:
Mtuhumiwa wa tukio hilo.
“Ni
kweli Rehema ni mkwe wangu kwa mwanangu aitwaye Godfrey Sechonge
anayeishi naye hadi sasa, Julai 5, mwaka huu mwanangu huyo alikuja na
akaniambia mkewe anatembezwa bila nguo.
“Nilifika eneo la tukio na kumkuta mkwe wangu yuko uchi huku akivuja damu mwili mzima.
“Aliniambia
amecharangwa viwembe na Zaituni akimshutumu kutembea na mumewe,
nilimchukua mwanangu na kumkimbiza polisi ambapo tulipewa PF3 na
kufunguliwa jalada namba MOR/RB/4009/2014.”
Naye Rehema alipozungumzia kisa
hicho alisema siku ya tukio saa 4 asubuhi, Zaituni alimtuma mwanaye
nyumbani kwake na kumuomba aende kwake (Zaituni).
“Nilipofika
kwake aliniingiza ndani na kuniwekea kisu shingoni huku mwanaye
akinirekodi na simu yake, akaniuliza nimetembea mara ngapi na mumewe!
“Alitaka kujua pia amenihonga
shilingi ngapi, kwa hofu ya kuchinjwa nilikubali kwamba nilitembea naye
mara moja na alinipa shilingi elfu tano. “Baada ya kusema hivyo
akaniachia, nikarudi nyumbani.
Saa
kumi aliniita tena, nilipofika nikamkuta yuko na mumewe na watoto wao,
akaniuliza unamjua huyu? Nikamwambia simjui, akatoa simu na kufungua
mahojiano, mumewe alipojaribu kumpora, akamchanja na wembe.
Mtuhumiwa akihojiwa.
“Ghafla
akahamia kwangu na kuanza kunichanja kwa wembe huku nikipiga kelele na
akanivua nguo kisha akanitoa nje na kunipeleka kwangu nikiwa na nguo ya
ndani tu,” alisema Rehama.
Akizungumza na paparazi diwani wa
kata hiyo, Lydia Mbihaji alisema tangu aanze kuongoza watu hajawahi
kukutana na tukio kama hilo ambalo aliliita ni la kinyama.
Tayari Rehema amelifikisha sakata hilo polisi na Zaituni alikamatwa
na kuwekewa dhamana na mumewe akisubiri kuburuzwa mahakamani wakati
wowote.
Baada
ya kudhaminiwa, paparazi aliwashuhudia Zaituni na mumewe wakizungumza
na Rehema ambapo inadaiwa wanataka ipatikane suluhu kabla kesi haijaanza
kuunguruma mahakamani.
Comments
Post a Comment