WASANII BONGO MOVIE WATIWA MBARONI KENYA
Msanii nyota wa filamu Bongo, Hisan Muya ‘Tino’.WASANII nyota wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ na Hisan Muya ‘Tino’ hivi karibuni walitiwa mbaroni katika mji wa Kilifi ulio mbele ya Mombasa nchini Kenya baada ya kukutwa wakipiga picha za filamu yao bila kuwa na kibali.
Hata
hivyo, waigizaji hao baadaye waliachiwa, ingawa hali ilikuwa ngumu
kidogo kwa Tino, ambaye polisi wa Kenya walidai hakuwa Mtanzania, bali
ni raia wa Somalia.
Dude
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema liliwatokea kutokana na
mazoea ya huku nyumbani ambako hufanya shughuli zao za kupiga picha za
filamu zao bila kuhitaji kibali.
“Yaani
tumepata aibu ya mwaka, kwani tulienda kushuti bila kuomba kibali
kutokana na mazoea ya huku kwetu Bongo, tulipekuliwa sisi na gari letu,
baada ya hapo kibali kikaletwa nikaachiwa lakini Tino waliendelea
kumshikilia wakisema ni Msomali mpaka mkuu wa shirikisho la filamu
Mombasa alipokuja kuokoa jahazi, ukweli Kenya hakufai,”alisema Dude.
Comments
Post a Comment