ANGALIA MATESO ANAYOPATA MWENZETU,MSAADA WA HARAKAUHAHITAJIKA.
Kwa
kipindi hiki kijana Amos, ambaye anatoka Kata ya Mryaza, amelazwa
Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu, lakini matarajio ya
kupona kwa tiba za hapa nchini hayapo hivyo njia pekee iliyobaki ni
kwenda nchini India kwa matibabu zaidi.
Kijana
Amos Ng’arare Sasi (21) mkazi wa kijiji cha Kizaru wilayani Musoma
Vijijni amepoteza mwelekeo wa maisha baada ya ndoto yake ya kusoma hadi
chuo kikuu kuishia njiani kutokana na matatizo ya ugomjwa wa ajabu ambao
umemtesa kwa kipindi cha miaka 17.
Kwa
kipindi hiki kijana Amos, ambaye anatoka Kata ya Mryaza, amelazwa
Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu, lakini matarajio ya
kupona kwa tiba za hapa nchini hayapo hivyo njia pekee iliyobaki ni
kwenda nchini India kwa matibabu zaidi.
Katika mahojiano na Mwananchi wiki iliyopita akiwa Wodi Namba 21, Sewahaji, Amos alionekana mwenye mawazo kupita kiasi.
“Ndoto
yangu ya elimu itakuwa imeishia hapa. Sitegemei kurudi tena. Wenzangu
niliokuwa nikisoma nao darasa moja, kwa sasa wapo kidato cha nne.
Nilizaliwa nikiwa sina tatizo la aina yoyote kiafya na nililelewa na
wazazi wote wawili. Kwa kweli kwa malezi niliyoyapata, sikuwahi kujiona
tofauti,” anasema.
“Nikiwa
na miaka minne baba alifariki dunia, nikabaki na mama ambaye alitulea
mimi na kaka yangu kwa furaha akijishughulisha na kilimo cha jembe la
mkono,” anasema Sasi.
“Baadaye
tulibaki wawili tu, yaani mimi na mama baada ya kaka kuondoka kwa madai
kuwa anakwenda kutafuta maisha. Ilikuwa mwaka 1998 na mpaka leo
hatujawahi kumuona wala kusikia taarifa zake,” anasimulia Sasi.
Anasimulia
kuwa alipofikisha umri wa miaka minne, usoni kwake kuliota kitu kama
kipele ambacho alisema kilikuwa kinamuwasha sana.
Anaongeza kuwa mama yake alimpeleka hospitali ambako alipewa dawa za kupunguza maumivu tu.
“Nilipofikisha umri wa miaka tisa hali ilizidi kwa mbaya, maumivu na uvimbe ukazidi,” anasema.
“Mama
alinionea huruma akawa halali pale anapoona nalia kutokana na maumivu
makali. Aliamua kunipeleka hospitali ya Musoma lakini hakukuwa na
mabadiliko. Mwaka 2010 alinipeleka Hospitali ya Bugando mkoani Mwanza,
huko nilifanyiwa uchunguzi, lakini ugonjwa haukujulikana.”
Anasema
wakati huo matokeo ya shule ya msingi yalikuwa yametoka naye alifaulu
kwenda kidato cha kwanza, lakini alishindwa kutokana na kuzidiwa na
maumivu.
“Nilirudishwa
nyumbani, nikawa sipati huduma ya aina yoyote. Watu walioniona
walinionea huruma, wengine wakawa hawataki kuniona mitaani. Walinitishia
kuwa nikionekana, nitakamatwa na wachimba madini wanichinje wachukue
viungo wakafanye manbo ya kishirikina wapate madini kwa wingi,”
anabainisha.
“Baadhi ya wananchi walinionea huruma. Walinichangia fedha ili nije Muhimbili nipate matibabu.”
Anasema alifika Muhimbili Septemba, 2011 na madaktari walichukua vipimo na kumwambia arudi mwezi mmoja baadaye.
“Hata
hivyo sikuweza kurudi kipindi hicho kutokana na kukosa nauli. Namshukuru
mbunge wetu Nimrod Mkono na diwani wetu walinisaidia nauli ya kuja.
Nikaja mwezi wa pili mwaka huu. Walinipima kwa mara ya pili na kunieleza
kuwa kuna mshipa wa fahamu unapitisha damu nyingi hivyo natakiwa
kufanyiwa upasuaji nchini India.
“Wakati
fulani ninapata maumivu hadi napoteza fahamu. Nasikitika hali hii huwa
inanikuta nikiwa peke yangu na mama anapenda sana kuja kuniona, lakini
anashindwa kwa sababu ya kukosa nauli.
“Nawashukuru
sana madaktari kwa kuwa karibu nami na kunipa dawa za kupunguza
maumivu. Pia wauguzi wamekua nami kwa kunisaidia na kuniliwaza.
Ninawapongeza ila kinachoniuma ni pale ninapowaona wagonjwa
wanatembelewa na ndugu zao, lakini kwa upande wangu hakuna hata mtu
mmoja,” anasema kijana huyo.
“Nawaomba Watanzania wanisaidie kwa msaada wowote hata kwa kuniombea, ili Mungu anisimamie nipelekwe India nitibiwe.
“Mimi ni kijana mdogo ninayetamani kurudi shule na kufanya shughuli nyingine za maendeleo.”
Kwa atakayeguswa na tatizo la mtoto huyu anaweza kuwasiliana na ofisi za Mwananchi au kupiga simu namba 0688551355.
Comments
Post a Comment