UVUMILIVU NI SOMO LA MAISHA, UPO TAYARI KUJIFUNZA?


Kuna mtu mmoja alishawahi kusema hivi, “Mwonekano wako ni halisi unapojionyesha wakati wa mambo magumu, huwezi kuwa zaidi ya hivyo katika utu wako”. Ukiendelea kuwahukumu watu wengine kutokana na tabia zao huwezi ukaona kitu kizuri ndani yao. Badala ya kumwona mfanyakazi mwenzako ni mtata, msumbufu, katili , hana utu, jaribu kumwona mtu huyo kama mwema na anahitaji kueleweka. Tafuta kitu kizuri ndani yake na uweze kwenda naye kwa hicho kizuri.
Ingawa mambo kama hayo yamejengeka kwa muda mrefu kutokana na wapi mtu huyo alizaliwa, maisha gani amepitia na mambo gani yameikabili familia yake akiwa mtoto, kama wazazi kupigana, kutoonyeshwa upendo kwa wazazi wake mwenyewe hivyo kuathirika na vitu vingi.
Unapojaribu kuchukuliana na udhaifu wa mtu mwingine na jinsi alivyo unahitaji uvumilivu. Fikiria kwamba kuna mfanyakazi unataka abadiLike kutokana na tabia zake, je yuko hapo kukufundisha nini? je wanakupa mwangaza gani na wewe kujiona kwenye kioo? Mara nyingine ni watu ambao unatakiwa kujifunza kutokana na jinsi walivyo na utagundua mambo mengi ambayo ulikuwa huyajui hasa kuhusu wewe mwenyewe.
Mfano, kama unasimamiwa na mtu ambaye ujuzi wake ni mdogo kuliko wa kwako, somo ambalo linatakiwa kukaa akili mwako ni namna ya kuchukuliana naye na uvumilivu. Badala ya kulalamika na kumwona hafai kumbuka tu ya kwamba ‘sisi sote hujitaidi kufanya kazi kwa namna tunavyoweza kwa wakati fulani’. Kuna wakati mwingine ninapenda msemo huu ‘naomba uwe mvumilivu kwangu, Mungu bado hajamalizana nami’ kwasababu wote hatujakamiliaka tunahitaji kuendelea kujifunza kila wakati.
Wakati tumekatishwa tamaa na watu wengine kazini kwetu ama kwenye taaluma zetu, tunatakiwa kujifunza kwa kiasi, kumbuka ulikotoka, halafu jitazame sasa na wapi unaelekea na unafanya nini kwa matatizo unayopata eneo la kazi. Jifunze kuvumilia na kusamehe. Kama ni sababu ya kitaaluma unatakiwa kujifunza ujuzi usiokuwa nao ili kujiboresha, kusaidia wengine wasioweza kama wewe hapo kazini kwa kuwafundisha ili waweze kujifunza na kuwa na mazingira mazuri ya kikazi hapo.
Somo la maisha ni zaidi ya masomo ya darasani, hivyo unatakiwa kujifunza kila siku. Vyuo vyetu havina wanataaluma wanaosaidia kisaikolojia, wengi wamekuwa wakitusaidia kufaulu masomo ya darasani na kwenye mahusiano. Tunahitaji watu wanaoweza kusaidia fikra za watu kuondokana na mtizamo hasi, uliojengwa na maisha ya mtu aliyopitia. Hutaweza kuwasaidia watu wengine kazini kwako kama huna uvumilivu wa kuweza kuwasaidia wafanye kinachotakiwa kufanyika.

Comments

Popular posts from this blog