BAADA YA WAFANYA KAZI WA SAMSUNG KUPATA KANSA, HATIMAYE KULIPWA NA KAMPUNI
Kampuni
kubwa duniani ya vifaa vye elektroniki, Samsung inasema kuwa itawalipa
fidia wafanyakazi wake waliougua Saratani kutokana na kufanya kazi
katika viwanda vyake.
Kampuni
hiyo iliomba radhi kwa kesi ya muda mrefu kati yake na wafanyakazi hao
waliokuwa wanadai fidia na badala yake kukubali kujiondoa katika kesi
hiyo huku ikikubali kuwalipa fidia wagonjwa hao.Hatua
ya Samsung kukubali kuwalipa wafanyakazi hao inaleta matumaini katika
kukamilika kwa mvutano huo ambao ulionekana kukwama kwa muda mrefu
Lakini
afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo, Kwon Oh-hyun nusura kukiri kuwa
kulikuwa sababu ya wafanyakazi hao kupatwa na Saratni ilichangiwa na wao
kufanya kazi katika kiwanda cha Samsung. Wengi walipata Saratani ya
damu au Leukaemia.
Bwana
Kwon alisema wafanyakazi kadhaa katika viwanda vyetu walipatwa na
Saratani ya damu na kuugua magonjwa mengine yasiyokuwa na tiba ambayo
yalisababisha baadhi yao kufariki.''
Akiongea
na wandishi wa habari, Bwana Kwon alisema kuwa Samsung inatumai kuwa
itaweza kumaliza kesi hii na kuweza pia kuwapa afueni wagonjwa na
familia zao.
Hata
hivyo kampuni hiyo kubwa zaidi duniani ya simu za Smartphone haikusema
idadi ya watu watakaolipwa fidia ingawa inaarifiwa ni watu 40
waliowasilisha malalamiko hayo huku kesi ikiendelea kwa zaidi ya miaka
sita.
Comments
Post a Comment