ANGALIA PICHA KIJANA AUAWA KWA KUPIGWA MAWE NA KUCHOMWA MOTO,MWINGINE ANUSURIKA KUFA,



Kulia ni mwili wa marehemu baada ya kuchomwa moto-kushoto ni Machela  ikiandaliwa  kuupakia  mwili wa kijana aliyeuawa kwa kuchomwa moto

 Kijana  aliyejulikana kwa jina la Mangi  akiwa  ndani  ya  gari, pembeni  yake  ni  maiti  ya  mwenzake
Polisi  wakikagua  makoti  ambayo  kijana  aliyenusurika  alikuwa  ameyavaa

Mtu mmoja anaesadikiwa kuwa ni jambazi ambaye hakufahamika jina anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 25 ameuwawa kwa kupigwa mawe kisha kuchomwa moto na mwingine kunusurika kuuwawa.

Tukio hilo limetokea jana  alfajiri  katika kijiji cha Shibula kata ya Bugongwa wilayani Ilemela Mkoani Mwanza kufuatia tukio la wizi lilotokea usiku wa kuamkia jana katika mtaa  wa  Nyamwilolelwa ambapo pikipiki moja na paneli ya solar ziliibiwa. 
 
Katibu wa Sungusungu katika kijiji cha Shibula John Mashalia amesema kuwa kufuatia tukio hilo waliamua kuweka ulinzi shirikishi kuzunguka vijiji vyote na ndipo walipokutana na kijana huyo aliyeuwawa akiwa na kijana mwingine aliyefahamika kwa jina la Edward Aloyce ambao walidai wanatafuta pikipiki iliyopotea.

Mashalia ameongeza kuwa kata ya Bugongwa imekuwa na matukio ya ujambazi mara kwa mara ikiwa ni pamoja na vitendo vya ubakaji kwa watoto na wanawake.


Kwa upande wake mkaguzi msaidizi wa jeshi la polisi Joyce Kotecha amewataka wananchi wa kata hiyo kuacha kujichulia sheria mkononi na kwamba wawasiliane na uongozi wa kata yanapotokea matatizo ya namna hiyo.
CHANZO MALUNDE BLOG

Comments

Popular posts from this blog