MADEREVA DALADALA WAGOMA KUINGIA BARABARANI

MADEREVA wa daladala Manispaa ya Morogoro wamegoma asubuhi hii wakidai kukamatwa hovyo na matrafiki na hakuna daladala linalofanya safari yoyote katika manispaa hiyo.
Madereva hao wanadai wameamua kugoma kutokana na kamatakamata ya askari wa usalama barabarani, ambapo wamesema daladala moja kwa siku linaweza kukamatwa hadi mara nne na wakihoji wanaambiwa ni makosa tofauti.

Waliongeza kuwa wamepeleka malalamiko yao ngazi mbalimbali za serikali mkoani Morogoro bila mafanikio.
Mgomo huo umewaathiri zaidi wanafunzi ambao wapo katika mitihani ya nusu muhula ambapo baadhi yao walilazimika kutembea kwa miguu huku wengine wakirudi nyumbani kujipanga.
Ili kuongeza uzito katika mgomo huo, madereva hao wametoa tahadhari kwa wamiliki wa mabasi ya Abood kutojaribu kupeleka mabasi yao barabarani kama ambavyo wamekuwa wakifanya pindi ukitokea mgomo ndani ya manispaa hiyo.

Comments

Popular posts from this blog