TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI CHUO KIKUU CHA DODOMA (ADMINISTRATIVE STAFF)
Chuo
Kikuu cha Dodoma kinawatangazia waombaji wa kazi mbalimbali kuwa
usahili wa kuandika utafanyika Jumamosi ya tarehe 8 Machi, 2014 na
Jumapili ya tarehe 9 Machi, 2014. Usahili huu utafanyika kuanzia saa
tatu asubuhi katika kumbi za mihadhara ya Skuli ya Sanaa na Lugha kama
ifuatavyo:
Jumamosi tarehe 8 Machi 2014
1. Maafisa Rasilimali Watu na Tawala
2. Maafisa Mipango
3. Madereva
4. Wahudumu
5. Makatibu Muhtasi
6. Wahudumu wa Afya
Jumapili tarehe 9 Machi 2014
1.Wahasibu Wasaidizi
2.Wakaguzi wa Ndani Wasaidizi
3.Watunza Kumbumbu Wasaidizi
4.Wasimamizi wa Mifumo ya Kompyuta Mtandao
5.Wasimamizi wa Maabara
Usahili wa
mahojiano kwa waombaji wa kada zote za afya isipokuwa wahudumu wa afya
utafanyika kuanzia Jumatatu tarehe 10 Machi, 2014. Usahili huu
utafanyika kuanzia saa tatu asubuhi katika jengo la Utawala kwa
utaratibu ufuatao:-
Jumatatu tarehe 10 Machi 2014
1. Mafundi Wasaidizi wa Maabara
2. Mafundi Sanifu Maabara
3. Wasaidizi Kumbukumbu za Afya
4. Wahandisi Vifaa Tiba
5. Mafundi Sanifu - Dawa
6. Mafundi Afya
Jumanne tarehe 11 Machi 2014
1. Wauguzi/Wakunga
2. Maafisa Uuguzi
Jumatano tarehe 12 Machi 2014
Madaktari
Alhamisi tarehe 13 Machi 2014
1.Wauguzi Wahitimu
2.Madaktari Bingwa
Usahili
wa mahojiano kwa waombaji wa kada zote ambazo hazikuorodheshwa hapo juu
utafanyika Jumatatu na Jumanne yaani tarehe 17 na 18 Machi, 2014 kama
ifuatavyo:
Jumatatu tarehe 17 Machi, 2014
1. Wakufunzi wa Michezo
2. Maafisa Sheria
3. Waalimu Wakufunzi
4. Maafisa Ugavi
5. Mafundi Mchundo
6. Wapokezi Wageni
7. Wahandisi Maabara
Jumanne tarehe 18 Machi, 2014
1.Mafundi Sanifu
2.Maafisa Miliki
ANGALIZO:
Siku ya
usahili wasailiwa watatakiwa kuwasilisha nakala za vyeti na vyeti
halisi, vitambulisho au kadi za kupigia kura na picha moja ya pasipoti.
Tarehe za usaili kwa wanataaluma zitatangazwa baadae.
Comments
Post a Comment