AKAMATWA NA MENO YA TEMBO 2 YENYE UZITO WA KILO 15 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 22
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri
Kidavashari akionenyesha mbele ya waandishi wa habari Ofisi kwake meno
ya tembo vipande 2 yenye thamani ya shilingi 22 hapo jana aliyokamatwa
nayo mtuhumiwa Batromeo Mtongwa hapo machi 8 katika kijiji cha kilida
katika tarafa ya mamba wilaya ya Mlele ambapo pia mtuhumiwa huyo
alikamatwa na gobole 1 na risasi 14.
Mkazi wa
kijiji cha mirumba kata ya kibaoni wilaya ya Mlele SAI LUPONJE (63)
akiwa katika kituo cha Polisi mkoa wa katavi akielezea jinsi watoto wake
wawili walivyomuua kitungulu Luhende (65) na kwisha kumtupa porini
baada ya watoto wake wawili kukasirishwa na kitendo cha mama yao huyo
kuwa na mahusiano ya kimapenzi na kitungulu Luhende ambae alikua ni
hawara yake wa muda mrefu mauaji hayo yalitokea wiki iliyopita katika
kijiji cha Milumba.
mkazi wa
kijiji cha kilida tarafa ya mamba wilaya ya mlele Patromeo Mtongwa (58)
akiwa katika kituo cha polisi cha mkoa wa Katavi baada ya kukamatwa na
meno mawili ya tembo yenye uzito wa kilo 15 yenye thamani ya shilingi
milioni 22 na gobole moja pamoja na risasi 14 mtuhumiwa alikamatwa hapo
machi 7 mwaka huu majira ya saa mbili usiku nyumbani kwake katika kijiji
cha kilida.
Na Walter Mguluchuma Mpanda Katavi
Mtu
mmoja aliyefahamika kwa jina la Bathromeo James Mtongwa 58Mkazi
wa Kijiji cha Kilinda Tarafa ya Mamba Wilaya ya Mlele Mkoa wa
Katavi amekamatwa akiwa nameno vipande viwili vyenye uzito wa kilo 15
vyenye thamani ya shilingi milioni 22 pamoja na Bunduki moja aina ya
Gobore na Risasi 14
Kwa
mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Kamishina
mwandamizi msaidizi mtuhumiwa huyo alikamatwa hapo machi 7 mwaka
huu majira ya saa mbili na nusu usiku
Alisema
mtuhumiwa alikamatwa kufutia taarifa ambazo ambazo zililifikia jeshi la
polisi pamoja na askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi kupata taarifa
kuwa mtuhumiwa anamiliki nyara za Serikali kinyume cha sheria
ambapo taarifa hizo zilipatikana hapo machi 6 kutoka kwa Raia wema
Alifafanua
ndipo siku hiyo ya tukio majira ya saa mbili usiku polisi wakiwa na
Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi walifika kwenye kijiji hicho
cha Kilinda nyumbani kwa mtuhumiwa Batromeo na kufanya upekuzi
nyumbani kwa mtuhumiwa na kufanikiwa kukamata risasi 14
Kidavashari
alieleza wakati askari hao wakiendelea na upekuzi kwa kushirikiana na
uongozi wa kijiji walilitilia shaka eneo moja la nyumba hiyo ya
mtuhumiwa kutokana na eneo hilo kuonekana kuwa limechimbwa
Alisema
ndipo askari walipoamua kuchimba eneo hilo na baada ya kufukua kwa
kitambo kidogo walifanikiwa kukuta meno ya Tembo vipande viwili vyenye
uzito wa kili 15 yenye thamani ya shilingi milioni 22 yakiwa yamefukiwa
ardhini kwenye shimo
Baada
ya kukamatwa kwa maneno hayo ya Tembo polisi walianza kumhoji
mshitakiwa kwa kumtaka awaelekeze sehemu ambayo amekuwa akiifadhi
Silaha ambayo amekuwa akiitumia kwenye matukio ya ujangili
Kidavashari
alieleza baada ya mahojiano mtuhumiwa aliweza kueleza kuwa bunduki
ambayo amekuwa akiitumia kwenye matukio ya ujangili ameifisha kwenye
eneo linaloitwa King’anda lililopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya
Katavi
Alisema
siku ya tarehe 8 machi majira ya saa nane mchana mtuhumiwa
aliwaongoza Askari Polisi na Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi na
kuwapeleka katika eneo la King’anda ndani ya Hifadhi ya Katavi na
aliweza kuwaonyesha silaha hiyo Bunduki aina ya Gobore ikiwa
imeifadhiwa kwenye kichaka
Mtuhumiwa
anatarajiwa kufikishwa Mahakamani wakati wawote mara baada ya
upelelezi wa tukio hili utakapo kuwa umekamilika mapema iwezekanavyo
pia jeshi la polisi Mkoa wa Katavi lanatowa wito kwa wananchi
kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa kutowa taarifa za
watu wanaojihusisha na uwindaji haramu wa rasilimali za Taifa ili
kulinda na kuhifadhi rasilimali zetu kwa manufaa ya vizazi vijavyo
Na Katavi yetu Blog
Comments
Post a Comment