AJALI ZACHUKUA UHAI WA WATU 34, 9 MANYARA, 9 LINDI, 13 SINGIDA NA 3 SAME

News Alert: watu 9 wafariki dunia na 30 kujeruhiwa katika ajali mkoani lindi leo

 Baadhi ya abiria ambao walikuwemo katika basi hilo wakiwa wametoka bila kujeruhiwa
BASI Likiwa limeanguka na maiti bado zilikuwa hazijatolewa chini
Kamishna msaidizi wa Jeshi la Polisi mkoa wa Lindi,Renatha Mzinga akisimamia zoezi la kuinua basi hilo kwa ajili ya utoaji wa Maiti  9 za ajali hiyo

Na Abdulaziz Video, Lindi
Watu 9 wakiwemo watoto 2 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 30
kujeruhiwa vibaya baada ya basi la abiria la Alhamdulilah linalofanya
safari zake kutoka jijini Dar kwenda mkoani Mtwara kupinduka katika
kijiji cha Mambulu Manispaa ya Lindi. 


 Ajali hiyo iliyotokea mchana leo baada ya basi hilo kupishana na lori
na kupoteza mwelekeo na kupinduka hali ilichangiwa na mvua iliyokuwa
ikiendelea kunyesha.


 Hadi ninatoka eneo la tukio marehemu hao hawakuweza kufahamika kwa
haraka kutokana na kukatika viungo na tayari majeruhi na maiti wote wamefikishwa hospitali.


Kamanda wa polisi wa mkoa wa Lindi,George Mwakajinga ambae
alikuwepo katika eneo la ajali hiyo hakuweza kuongea lolote kutokana na kutingwa na harakati za kuokoa majeruhi wa Ajali hiyo
Taarifa zaidi za majeruhi hao pamoja na maiti zilizotambuliwa tutawajuza

Ajali leo zachukua uhai wa watu 3 Same; 

9 Manyara; 9 Lindi; 13 Singida
MANYARA: Woinde Shizza kutoka Arusha ameandika kwenye blogu yake kuwa watu 9 wamefariki dunia hivi punde huku mmoja akinurusika baada ya kufukiwa na kifusi wilayani Karatu, Mkoa Manyara wakati wakichimba mchanga katika eneo ambalo lilikuwa limezuiwa na Serikali, lakini watu hao wameanza tena kuchimba hivi karibuni.



KILIMANJARO: Katika taarifa ya habari ya Radio Sauti ya Injili, Moshi jioni hii, imeripotiwa kuwa watu watatu wamepoteza uhai huku wengine 30 wakiachwa na majeraha mbalimbali wakati basi la kampuni ya Hood lenye namba T.497AHD walilokuwa wamepakia kutokea Iringa kuelekea Arusha, lilipopata ajali majira ya saa 11 jioni kwa kuacha njia na kuanguka katika eneo la Nkwini, huko Makanya-Hedaru katika barabara ya Same-Mombo wilayani Same mkoani Kilimanjaro.

Majeruhi wawili hali zao zimeelezwa kuwa mbaya hivyo kuwahishwa katika hospital ya rufaa ya KCMC. Majeruhi wengine wawili walitibiwa katika kituo cha afya cha Hedaru wakati miili ya marehemu waliotajwa na Robert Boaz (Kamanda wa 

Polisi mkoani Kilimanjaro), kuwa ni Stephano Kasimba, Fadhili Kasimba na Aziza Mdee, imehifadhiwa katika hospitali ya Same ambako majeruhi wengine 25 wanaendelea na matibabu.

Walionurusika kifo wamesema basi hilo halikuwa katika mwendo ila dereva wake aliyetajwa kwa jina la Baraka Juma, alionekana kuwa mchovu na huenda ajali hiyo imetokana na usingizi uliomkumba dereva huyo ambaye ametoroka baada ya ajali hiyo kutokea.

LINDI: Taarifa ya TBC Taifa iliyosomwa saa mbili usiku huu inasema kuwa, watu 9 wakiwemo watoto 2 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la abiria la Alhamdulilah linalofanya safari zake kutoka jijini Dar kwenda mkoani Mtwara kupinduka chana wa leo katika kijiji cha Mambulu huko katika manispaa ya Lindi, wakati likipishana na lori kabla ya kupoteza mwelekezo na kupinduka wakati mvua kali ikinyesha.
SINGIDA: Imeripotiwa katika taarifa ya TBC saa saba mchana na mbili usiku uu kuwa jumla ya abiria 13 wakiwemo watatu wa familia moja, wamefariki dunia mkoani Singida leo baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Noah T.730 BUK, kugongwa na lori aina ya Scania T.687 AXB.
Ajali hiyo ya mbaya iliyoacha miili ikiwa haitamaniki, imetokea leo mwendo wa saa moja asubuhi katika barabara kuu ya Singida-Dodoma kwenye eneo la kijiji cha Isuna tarafa ya Ikungi wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
Kamanda wa polisi mkoa wa Singida, SACP, Geofrey Kamwela, amesema gari hilo aina ya Noah lilikuwa likitokea Itigi kuelekea Singida Mjini huku lori lililokuwa likitokea Mwanza kupitia Singida kuelekea Dar es Salaam, wakati likipishana na Noah hiyo, lilihama upande wake na kuifuata Noah upande wa kushoto na kuigonga na kuiburuza: “...baadhi ya watu wanadai kuwa huenda dereva wa lori alisinzia na kusababisha lori hilo kuhama upande wake na kufuata Noah. Uchuguzi utakapokamilika tutatoa taarifa hiyo,” amesema.
Hadi sasa miili ya marehemu iliyokwishakutambuliwa na ndugu zao ni pamoja na Omari Shaaban (44) na mkewe Salma Omari  na mtoto wao Nyamumwi Omari (10) wote wakazi wa Itigi Mjini. Haji Mohammed (29) (Msisi), Mtunku Rashidi (68) (Sajaranda), Salehe Hamisi (28) (Sajanranda), Samir Shaban (20)  (Puma), Mwaleki Nkuwi (35) (Ikungi), Athumani Kalemba (38) na Ramadhan Mkenga (Sajaranda).
Miili ambayo haijatambuliwa imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa, mjini Singida.
Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa mjini Singida, Dk. Banuba Deogratius amekiri kupokea miili ya watu 13, wawili kati yao wakiwa ni watoto.
Katika ajali hiyo, abiria watatu walinusurika na kupata majeraha madogo.


Comments

Popular posts from this blog