Posts

DIAMOND ATOA ZAWADI YA GARI KWA MZEE GURUMO

Image
Msanii mkongwe wa muziki wa dansi, Muhidin Gurumo akijaribu gari dogo alilokabidhiwa na mwanamuziki wa bongo fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond ‘ kutokana na kutambua mchango wake baada ya kustaafu kazi ya muziki. Muhidin Gurumo akipokea funguo ya gari kutoka kwa Diamond Gari alilozawadiwa mzee Gurumo.

DIAMOND NA LINAH WANASWA TENA WAKITOMASANA HADHARANI

Image
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amenaswa na msanii mwenzake, Esterlina Sanga ‘Linah’ wakiwa kwenye mapozi ya kimahaba ambayo yametafsiriwa vibaya.   Katika tukio hilo lililojiri juzikati kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ndani ya Tamasha la Serengeti Fiesta, Diamond alishuhudiwa akiwa amempakata Linah ndani ya basi huku mikono ya jamaa huyo ikishika maeneo nyeti.   Mara baada ya kutimba uwanjani hapo wakitokea hotelini tayari kwa kufanya shoo, Diamond na Linah walibaki kwenye basi wakiwa wamepakatana na hata msichana huyo alipomaliza shoo yake kali mishale ya saa 3: 00 usiku, alirejea mikononi mwa Diamond ambaye alimpachika mapajani. Kwa mujibu wa mashuhuda, kama kweli mchumba wa Diamond, Penniel Mungwilwa ‘Penny’ anakubali mambo kama hayo, basi atakuwa na roho ngumu au moyo wa chuma.   Siyo mara ya kwanza Diamond na Linah kuripotiwa wakiwa wamepozi kimahaba kwani mwaka jana walifanya hivyo wakiwa jijini Mbeya hivyo kutafsir

HAYA NDIO MATUKIO YA UZINDUZI WA "FOOLISH AGE" YA LULU MICHAEL

Image
            MSANII wa Filamu Bongo, Elizabeth Michael 'Lulu', usiku wa kuamkia leo amefanikisha zoezi la uzinduzi wa filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Foolish Age .   Baada ya move hiyo kali ya dakika 120 iliyooesha ukali wa staa huyo kuoneshwa kwa dakika 20 tu na kubakisha zingine 100 kusubiri wateja kuziona majumbani kwao alipanda jukwaani kujitambulisha na kutoa shukrani kwa wamepenzi wa tasnia ya filamu nchini Tanzania kwa muitikio wao alipanda na kuimba wimbo huo wa Yahaya. Akianzia kuimba kiitikio cha wimbo huo akiwa Back Stage, Lulu aliwashangaza watu pale alipomudu vyema wimbo huo kiasi cha mashabiki ‘Mapedeshee’ wakiongozwa na Pedeshee Rich Rich, kupanda jukwaani na kumtunza fedha kibao ambazo hakika zilimpagawisha msanii huyo na mwisho wa wimbo huo alisema mziki unalipa. Tukio la uzinduzi huo lilifanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, na kuhudhuriwa na mastaa kibao wa tasnia mbalimbali hapa Bongo, wakiwemo;

AIBU KWA TANZANIA.....MKUU WA JESHI LA POLISI TANZANIAI INSPEKTA JENERALI SAIDI MWEMA AIBIWA UPANGA WENYE THAMANI YA SH600 MILIONI JIJINI DAR ES SALAAM.

Image
  JESHI la Polisi limeingia katika kashfa nzito baada ya mkuu wake, Inspekta Jenerali Said Mwema, kuibiwa upanga wa dhahabu ambao ni mali ya Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi wa nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO). Upanga huo wenye uzito wa takriban kilo tatu na wenye thamani ya zaidi ya fedha za Tanzania Sh600 milioni, ni kielelezo kwa nchi inayokabidhiwa uongozi wa SARPCCO. Mwaka jana Tanzania ilikuwa mwenyekiti wa SARPCCO, ambapo upanga huo ulikabidhiwa kw a IGP Mwema na Jenerali Magwashi Victoria ‘Riah’ Phiyega, ambaye ni Kamishna wa Taifa wa Polisi wa Afrika Kusini aliyekuwa amemaliza muda wake kwa wakati huo. Hilo ni tukio la pili la wizi la mali zinazohusu ofisi ya IGP, ambapo mwaka jana ndani ya ofisi hiyo kuliibwa kompyuta ndogo (laptop), ikiwa na taarifa muhimu za kipolisi. Hadi sasa hakuna taarifa za kupatikana kwa kompyuta hiyo. IGP Mwema alikabidhiwa upanga huo Septemba 5, 2012, katika mkutano saba wa SARPCCO uliofanyika

ANGALIA PICHA ZAIDI YA 30..KATIKA UZINDUZI WA VIDEO MPYA YA DIAMOND

Image
Hamis Mwinjuna A.k.a Mwana F.A alikuwepo pia kushow Love.... Interiew zinahusika sana sehemu kama hizi.... Sauda wa Bongo Beats ya Star Tv nae akukosekana ndani ya nyumba..... Chege Chigunda Toka TMK nae alikuwepo..... Flowers awakosekanagi sehemu kama hizi....... wakiongozwa na Number One Diva Hamisa hassani Mobeto. Mzee Muhidini Gurumo nae akukosekana ndani ya Nyumba.....Furaha Ilioje kumuona Nguli wa Muziki wa Dansi nchini akiudhuria kwenye kitu chako,binafsi nimefurahi sana uwepo wake ulizidi kuimarisha moyo wangu. Prince Brother Man Dully Sykes akiwasili ndani ya Nyumba pembeni na FloweR Shadee toka Clouds Tv,presenter wa Cloud 9... Shadee & Dully...Mmmmmh....??? Aya sina usemi Kama kawaida...... Sarah A.k.a Shaa nae ndani  Movement zikiendelea na mahojiano mbalimbali kati ya wasanii na presenters wa vituo mbalimbali vya Habari & Blogs kiujumla wa