Posts

MBUGA ZA WANYAMA UNAZOWEZA KUTEMBELEA BURE WIKENDI HII

Image
Siku ya Jumatatu ya Juni 5 itakuwa ni maadhimisho ya ‘Siku ya Mazingira Duniani’ ambayo huadhimishwa na mataifa tofauti duniani ikiwa imebeba kauli mbiu ya ‘Kuwaunganisha Watu na Mazingira Asilia.’ Mapema wiki hii Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba  alitoa taarifa kwa umma kuwa kwa hapa nchini maadhimisho ya siku hiyo kitaifa yatafanyika kijijini Butiama mkoani Mara, mahali alipozaliwa mwasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwl. Julius Nyerere, ikiwa ni kuenzi jitihada zake za kulinda na kuhifadhi mazingira. Katika kunogesha sherehe hizo Waziri huyo amesema kuwa serikali imetoa ofa kwa wananchi kutembelea hifadhi yoyote ya mbuga ya wanyama bila ya kiingilio chochote kwa siku tatu, kuanzia Ijumaa ya Juni 2 mpaka Jumapili ya Juni 4. Alisema kuwa lengo kubwa ni kuona uwepo wa wanyama na kujifunza kuwa mazingira yanahitaji kulindwa zaidi na zaidi. Kauli hiyo ya Waziri imekuja si...

KIASI CHA PESA KILICHOKUTWA NYUMBANI KWA IVAN NCHINI AFRIKA KUSINI

Image
Hiki ndicho kiasi cha pesa kilichokutwa nyumbani kwa IVAN nchini South Africa Hiki ndicho kiasi cha pesa kilichokutwa nyumbani kwa IVAN nchini South Africa Inakadiriwa takribani dola milioni 300 na Rand miioni 600 zimekutwa nyumbani kwa Marehemu IVAN

DAKTARI AELEZA SUMU ILIYOMUUA MUME WA ZAMANI WA ZARI,AFICHUA SIRI NZITO

Image
Stori: Waandishi Wetu  KAMPALA: Imefichuka! Nyuma ya msiba ulioacha historia wa aliyekuwa mzazi mwenza wa staa wa Afrika Mashariki, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, Ivan Ssemwanga ‘The Don’ aliyepatwa na umauti wiki iliyopita akiwa amelazwa kwenye Hospitali ya Steve Biko, Pretoria nchini Afrika Kusini, kuna mengi yanayosemwa, Wikienda liko bega kwa bega na kinachojiri. Miongoni mwa yanayosemwa ni madai ya jamaa huyo kupewa sumu iliyomdhuru moyo hivyo kusababisha kifo chake. MADAI YA SUMU Chanzo cha ndani ya familia ya Ivan kililieleza gazeti moja maarufu nchini Uganda kuwa, Ivan alilishwa sumu na watu ambao hawakuwataja na kwamba mara ya mwisho alikuwa akipata chakula na ndugu zake kabla ya hali yake kuanza kuwa mbaya kisha siku chache baadaye alikimbizwa katika Hospitali ya Steve Biko.Gazeti hilo lilimkariri mtu huyo akieleza kuwa, Ivan hakufa kwa shambulio la moyo wala moyo kushindwa kufanya kazi bali aliwekewa sumu kali kwenye chakula. MAUMIVU MAK...

Maisha Ya Mke wa Deo Filikunjombe Baada ya Miaka Miwili ya Kifo Cha Mumewe

Image
Mkewe  wa Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ludewa mkoani Njombe, marehemu Deo Haule Filikunjombe, Sarah Filikunjombe. STORI: BRIGHTON MASALU NA ANDREW CARLOS, IJUMAA, HABARI MAMA shujaa! Ikiwa imebaki miezi minne na siku kadhaa itimie miaka miwili kutokea kwa kifo cha aliyekuwa kada muaminifu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mbunge wa Jimbo la Ludewa mkoani Njombe, marehemu Deo Haule Filikunjombe, mkewe Sarah Filikunjombe (Pichani) amethibitisha ushujaa kwa kuendelea kupambana na changamoto za kimaisha na kufikia vilele mbalimbali vya mafanikio, Ijumaa limemfungia kazi. Mwishoni mwa wiki iliyopita na mwanzoni mwa wiki hii, kwa siku tatu tofauti, waandishi wetu walijipa kazi ya ziada ya kumtafuta Sarah ili kujua nini kimeendelea katika maisha yake baada ya kuondoka kwa mumewe ambapo walibaini mambo mengi mazuri yenye kutia moyo, ambayo mama huyu licha ya kuonekana sistaduu, ameyafanya kwa ujasiri wa kipekee. IJUMAA NYUMBANI KWAKE Hatimaye Jumanne mchana, gazeti hi...