Posts

Rais Museveni anaongoza matokeo ya awali Uganda

Image
Rais Museveni akitumbukiza kura yake katika kisanduku. MATOKEO ya awali ya Uchaguzi Mkuu nchini Uganda yaliyotangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (EC), Eng. Badru Kiggundu leo asubuhi yanaonyesha Rais Museveni anaongoza kwa kupata kura 1,362,961 sawa na asilimia 61.75 huku mpinzani wake wa karibu Kizza Besigye akifuatia kwa kupata kura 738,628 sawa na asilimia 33.47 na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu Amama Mbabazi mpaka sasa yeye ana kura 41,291 sawa na asilimia 1.87. Kizza Besigye  naye akitumbukiza kura yake kwenye kisanduku. Matokeo hayo ni kutoka katika vituo 6,448 kati ya 28,010 vilivyotumika kupigia kura. Jumla ya watu 15,277,198 walijiandikisha kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka huu.

Mama amcharanga viwembe mwanaye!

Image
Majeraha aliyoyapata baada ya kujeruhiwa na viwembe. Stori: Joseph Ngilisho, Ijumaa Arusha: Ukatili wa watoto haukubaliki! Mama mzazi aliyetajwa kwa jina moja la Anna, mkazi wa Oysterbay maeneo ya Unga-Limited jijini hapa anadaiwa kumcharanga kwa viwembe mwanaye wa kumzaa mwenye umri wa miaka kumi anayesoma shule ya msingi (jina la mtoto na shule yanahifadhiwa). Tukio hilo la kusikitisha lilijiri mapema wiki hii nyumbani kwa mama huyo maeneo ya Oysterbay hivyo kumlazimu Diwani wa Kata ya Themi, Melance Kinabo kushirikiana na polisi kumkamata mzazi huyo kutokana na kitendo alichomfanyia mwanaye na kumwachia majeraha makubwa. Kwa mujibu wa mshuhuda wa tukio hilo, mama huyo anayefanya kazi kwenye moja ya viwanda vilivyopo Unga-Limited, anadaiwa kumfanyia mwanaye ukatili huo huku kisa kikielezwa ni kitendo cha mtoto huyo kukataa kuchota maji. Ilielezwa kuwa, mtoto huyo kwa sasa anapatiwa matibabu kwenye zahanati moja iliyopo Unga-Limited jijini hapa kufuatia majeraha ya ...

MAGAZETI YA LEO IJUMAA TAREHE 19.02.2016

Image

MAGAZETI YA UDAKU LEOTAREHE 19/02/2016

Image

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANILEO TAREHE 18/02/2016

Image

MKUU WA WILAYA AMBEBA MWANDISHI WA HABARI MGONGONI.

Image
Mkuu wa wilaya ya Iringa Kasesela akiwa amembeba mwandishi wa habari mgongoni.Ikiwa ni eneo la tukio la mafuriko yaliyotokea juzi mkoani humo. source:thechoice

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA BAADHI YA MAKUNDI YALIYOSHIRIKI NAYE KWENYE KAMPENI YA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2015

Image
Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akisalimia katika mkutano wa Rais John Pombe Joseph Magufuli na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016. Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan  akisalimia katika mkutano wa Rais John Pombe Joseph Magufuli na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.  Rais John Pombe Joseph Magufuli akiongea na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 18, 2016.  Rais John Pombe Joseph Magufuli akiongea na baadhi ya makundi yaliyoshiriki naye kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 aliowaita kuwashukuru Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi February 1...

RAIS MAGUFULI AZUNGUMZA NA WASANII IKULU

Image
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Msanii wa Kundi la Orijino Komedi, Lucas Mhavile, maarufu kwa jina la Joti katika mkutano kati ya Rais John Magufuli na Wasanii uliofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Februari 18, 2016.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)