Posts

MUHUMBILI YAPATIWA MSAADA WA MASHINE YA KISASA YA DIGITAL YA X-RAY

Image
Mkuu wa Idara ya Mionzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Flora Lwakatare akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu matumizi ya mashine mpya ya X-ray ya digitali.  Dk Lwakatare amesema mashine hiyo ina uwezo wa kupiga picha na kutumwa nje ya nchi kwa ajili ya ushauri wa kitaalamu zaidi. Mashine hiyo haihitaji chumba cha kusafishia picha wala dawa za kusafishia. Mkuu wa Idara ya Mionzi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Flora Lwakatare akitoa maelezo kuhusu idadi ya wagonjwa waliopata huduma ya kipimo cha CT Scan baada ya mashine hiyo kukamilika. Pichani ni misaada ya shuka 200, neti 150 na Televisheni nne ikipokelewa leo  katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH). Pichani ni misaada ya shuka 200, neti 150 na Televisheni nne ikipokelewa leo  katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH). ……………………………………………………………………………… Hospitali ya Taifa  Muhimbili (MNH) imepata mashine mpya na ya kisasa ya Digital X-ray ambayo wataalamu wake ...

NEC YATAOA TAMKO KUHUSU UCHAGUZI WA WABUNGE ARUSHA MJINI NA HANDENI

Image
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu uchaguzi wa wabunge unaotarajiwa kufanyika Tarehe 13/12/2015 katika jimbo Handeni na Arusha Mjini, (kushoto) ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura Bw.Clarence Nanyaro kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi.  Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva(ambaye hayupo katika picha) leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waaandishi wa habari kuhusu taratibu zitakazo tumika katika uchaguzi wa wabunge katika jimbo la Arusha na Handeni.

MAGUFULI ATAJWA HUKO SWEDEN KUWACHONGANISHA MARAIS WENZAKE NA WAPIGA KURA WAO

Image
Dagens Nyheter ni gazeti kubwa kushinda yote nchini Sweden, ndio 'Daily News' lao kwa maana ya jina la gazeti. Katika toleo lake la Ijumaa Desemba 4, habari za John Magufuli zimepamba pia gazeti hilo. Amemwagiwa sifa, na ikaandikwa pia, kuwa Magufuli amewaweka katika wakati mgumu marais wenzake wa nchi jirani kwa vile wapiga kura wao wameonyesha wivu wao kwa Watanzania kupata Rais wa aina ya Magufuli. Hata hivyo, kwenye gazeti hilo, imeandikwa pia, kuwa hata kabla ya kuingia milango ya Ikulu, Magufuli tayari ameshajipatia maadui wakiwamo wa ndani ya chama chake kwa hatua zake anazozichukua, hususan za kubana matumizi ya Serikali.  Habari nzima  unaweza kuitazama kupitia Website ya Hilo gazeti kwa kubofya link hii hapa .Imeandikwa kwa lugha yao. link: http://www.dn.se/nyheter/varlden/president-skaffar-fiender-nar-han-later-kvasten-ga/ Tafsiri ya maelezo waliyoandika  kwa Kiingereza ni kama inavyosomeka hapa chini...... The newly elected Pr...

SAKATA LA MANJI NA COCO BEACH, TAMKO KALI LATOLEWA,WAFUNGUKA MAZITO,HATUA KALI KUCHUKULIWA

Image
JUKWAA HURU LA WAZALENDO TANZANIA (JUHWATA) TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Ndugu waandishi wa habari, Jukwaa limewaalika hapa katika muendelezo wake wa kuunga mkono juhudi za Mh. Rais wetu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mh. -Dr. John Magufuli. Hivi karibuni mh. Rais ameongoza mapambano makubwa ya kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi na kuwachukulia hatua wale wote ambao wamehusika kuliingizia taifa hasara ya mabilioni ya shilingi yaliyopotea. Tunaunga mkono juhudi hizi za Rais wetu na tunamuhakikishia kuwa Jukwaa linamuunga mkono na kwamba tunaomba azidishe kasi zaidi ili wale wote waliokwepa kodi wakamatwe, walipe na kufikishwa katika vyombo vya sheria bila huruma yoyote. Ndugu waandishi wa habari, leo tumewaita hapa dhumuni kuu likiwa ni kuzungumzia uporaji wa maeneo ya wazi yanayotumiwa na wananchi hasa wanyonge. Uporaji huu unafanywa na baadhi ya wafanyabiashara wenye tamaa ambao hutumia nguvu zao za kiuchumi kuwarubuni na wakati mwingine kuwahonga viongozi wetu wachache seri...

RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA KATIBU MKUU WIZARA YA UCHUKUZI, AVUNJA BODI YA MAMLAKA YA BANDARI (TPA) LEO

Image
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha kwa waandishi wa habari, ripoti Bandari ya Dar es salaam iliyobaini mianya ya ukwepaji kodi ikiwemo ya Makontena 2,387 yaliyopitishwa kati ya Machi na Septemba mwaka jana. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari, Ofisini kwake jijini Dar es salaam leo. RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amevunja bodi ya Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) pamoja na kutengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka, Mwenyekiti wa Bodi ya Bandari Profesa Joseph Msambichaka pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Bandari, Awadh Massawe. Kuvunjwa kwa bodi hiyo kunatokana na utendaji mbovu wa Mamlaka hiyo kwa muda mrefu na kitendo cha kutokuchukua hatua katika vyanzo husika. Akizungumza  na waandishi wa Habari  Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam leo, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kute...

KATIBU MKUU TAMISEMI AKAGUA MIUNDOMBINU YA MFUMO WA MABASI YAENDAYO HARAKA

Image
  Katibu Mkuu Ofisini ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw. Jumanne Sagini (kushoto) akimweleza jambo Mwenyekiti wa Kampuni ya UDA-RT, Bw. Robert Kisena wakati alipofanya ziara kwenye miundombinu ya mfumo wa Mabasi yaendayo haraka kabla kipindi cha mpito hakijaanza mwezi ujao mwisho mwa wiki. UDA-RT ndiyo kampuni itayotoa huduma ya usafiri katika kipindi hicho na tayari imeshanunua mabasi 140. Katibu Mkuu Ofisini ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw. Jumanne Sagini (kushoto) akikagua miundombinu ya mfumo wa mabasi yaendeyo haraka na kuli ni Mwenyekiti wa Kampuni ya UDA-RT, Bw. Robert Kisena wakati alipofanya ziara kwenye miundombinu ya mfumo wa Mabasi yaendayo haraka kabla kipindi cha mpito hakijaanza mwezi ujao mwishoni mwa wiki. UDA-RT ndiyo kampuni itayotoa huduma ya usafiri katika kipindi hicho na tayari imeshanunua mabasi

KORTINI KWA TUHUMA NJAMA ZA KUTAKA KUMUUWA MWENYEKITI WA NEC JAJI LUBUVA

Image
WATU wawili wakiwemo Mwanasheria na Mwalimu, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka ya kula njama za kumuua Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva na familia yake. Washitakiwa hao, Mwalimu Samwel Gikaro (30) na Mwanasheria Angela Mbonde (32) walifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba. Wakili wa Serikali, Hellen Moshi alidai kati ya Oktoba 23 na Novemba 16, mwaka huu katika maeneo tofauti Dar es Salaam na maeneo mengine nchini, washitakiwa na wengine ambao hawajafika mahakamani, walikula njama za kumuua Jaji Lubuva na familia yake. Washitakiwa walikana mashitaka na upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo unaendelea na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa. Wakili wa upande wa utetezi, Moses Kaluwa ambaye alifika mahakamani hapo kwa niaba ya Wakili Peter Kibatala, aliiomba mahakama itoe dhamana kwa washitakiwa kwa kuwa mashi...

BREAKING NEWZZZ!!!! ABOUBAKAR KASONGO MPINDA ‘CLAYTON’ AFARIKI DUNIA

Image
King Kiki (kulia) akiimba sambamba na Aboubakar Kasongo Mpinda ‘Clayton’ enzi za uhai wake. Aboubakar Kasongo Mpinda ‘Clayton’ akiwa na Issa Nundu (kulia). Na Sifael Paul Habari zilizoufikia mtandao huu jioni hii zinaeleza kuwa mwanamuziki mkongwe katika tasnia ya muziki wa dansi nchini mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Aboubakar Kasongo Mpinda ‘Clayton’ amefariki dunia nyumbani kwake, Kinondoni jijini Dar. Kwa mujibu wa wanamuziki waliofanya naye kazi kwa muda mrefu, Kasongo ambaye alifanya kazi na bendi nyingi kama Maquis du Ziare akiwika na Nyimbo za Angelo, Mwana Malole, Nasononeka, Baharia, Siri ya Mkoko na zingine kibao amefariki dunia baada ya kuumwa kwa muda mrefu akisumbuliwa na Kisukari hivyo taratibu za mazishi zinaendelea kufanywa na familia yake. Katika siku za mwishoni, Kasongo aliitumikia Bendi ya Bakulutu kabla ya kujiunga katika Bendi ya Bana Maquis ikiwa chini ya Tshimanga Kalala Asssosa.

BREAKING NEWS : KESI ILIYOKUWA INAMKABILI MWENYEKITI WA CUF IBRAHIM LIPUMBA YAFUTWA RASMI

Image
Professor  Ibrahim Lipumba  alikuwa na kesi pamoja na wafuasi 30 wa CUF katika Mahakama ya Kisutu Dar es Salaam akikabiliwa na mashtaka ya kufanya mkusanyiko bila ya kuwa na kibali cha Polisi. Picha ya January 2015  Prof. Lipumba  akiwa Mahakamani Kesi hiyo ilianza kusikilizwa toka January 2015, ninayo ripoti kutoka kwenye taarifa ya habari ya ITV kwamba  Prof. Lipumba  na watu wote 30 wamefutiwa mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili Mahakamani hapo.

WOLPER AKIVISHWA PETE TU KWISHA HABARI YAKE!

Image
Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper. KUMBE! Waliosema ujana maji ya moto hawakukosea kwani una changamoto nyingi hasa pale unapofikia wakati wa kumtafuta wa kuwa naye maishani yaani mke au mume. Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe anaweza kuthibitisha hilo baada ya uchunguzi kuonesha kuwa ana listi ya wanaume waliomvisha pete za uchumba kisha wakapata walichokitaka, wakaingia mitini. Uchunguzi huo ulibaini kwamba, wanaume wengi wamekuwa wakitumia gia hiyo kumrubuni na kumwachia maumivu makali ya moyo. Katika makala haya tunakuletea listi ya wanaume ambao waliwahi kuwa na Wolper na kumvisha pete za uchumba na wengine kujitambulisha au kumtambulisha kabisa kwa wazazi lakini baada ya kumfaidi wakammwaga na kujikuta akihamia kwa mwingine, jambo ambalo watu wengine ambao ni mashabiki wake wamekuwa wakihoji ana nini mpaka yamkute hayo? ABDALLAH MTORO ‘DALLAS’ Mfanyabiashara huyo aliyekuwa na fedha ‘chafu’ alianzisha uhusiano na Wolper ambapo alimvisha pete ya u...

SHAMSA FORD AMFUNGUKIA NAY WA MITEGO NA KUMWAMBIA MANENO HAYA MAZITO

Image
Staa wa filamu Bongo, Shamsa Ford. KARIBUNI wasomaji wetu wa kolamu hii ambayo tumekuwa tukiwaletea wasanii mbalimbali na kufunguka mambo ambayo yamekuwa yakikutatiza, kwanza napenda kuomba radhi kwa kutomleta mwanadada, Riyama Ally kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu. Leo hii tunaye staa wa filamu Bongo, Shamsa Ford ambaye amefunguka mambo mengi ya kisanaa na kimaisha.   Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ Msomaji: Habari dada Shamsa kwanza nikupongeze kwa kazi nzuri lakini ningependa kujua pale unapokumbwa na skendo huwa unajisikiaje au umeshazoea hayo mambo? Shamsa: Nikiwa kama mzazi huwa najisikia vibaya na bora skendo yenyewe iwe ya kweli ikiwa ya kusingiziwa huwa naumia zaidi. Msomaji: Eti dada nilisikia unatoka na msanii Emmanuel Elibarik ‘Nay wa Mitengo ‘ mliishia vipi au bado mnaendelea kimyakimya? Shamsa: Masuala ya Nay tumeshamalizana, kila mtu yupo bize na maisha yake. Msomaji: Hivi dada maisha yako yapoje baada ya kuachana na baba watoto wako (Dickson)...

Gari la Wema mikononi mwa Rais Magufuli

Image
Hali ni tete! Chanzo kimoja kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kimenyetisha kwamba, kasi ya Rais John Pombe Magufuli ‘JPM’ kuhakikisha hakuna Mtanzania anayekwepa kodi imepamba moto na sasa, imetua kwa mastaa wa Bongo ambapo kuna madai lile gari la kifahari la Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu (pichani) aina ya Range Rover Evogue linachunguzuwa na TRA, Amani limenyetishiwa. SI YEYE TU Kwa mujibu wa chanzo hicho, mbali na Wema, mastaa wengine ambao nao magari yao yako kwenye orodha ya kuchunguzwa mwenendo wa kodi ni Jacqueline Wolper Massawe (Toyota Prado), Kajala Masanja (Toyota Hilux) na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ (BMW X6). MAELEZO YAKO HIVI “Unajua serikali imedhamiria kukusanya kodi. Anachotaka Rais Magufuli ni kila mtu mwenye haki ya kulipa kodi ya kitu fulani, afanye hivyo bila kukwepa. Na hakuna kumuonea mtu. “Sasa bwana…bwana! Huko makao makuu (TRA) hakukaliki, huyo Kaimu Kamishna Mkuu, Phillip Mpango ni mkali balaa, anadhani Magufuli atamzukia wakat...

CHADEMA NAO WATOA MAONI YAO UTENDAJI KAZI WA RAIS MAGUFULI.

Image
Wakati Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano, John Magufuli akionekana kuteka hisia za Watanzania wengi, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema hakishtushwi kwani amekuwa akitumia hoja, mikakati na Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho. Akizungumza na gazeti hili, Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu, alisema kuwa wakati wa kampeni Chadema ilieleza jinsi ya kupambana na ufisadi, kuwa na utaratibu bora wa utendaji kazi, uadilifu na uzembe wa watumishi wa umma, mambo ambayo sasa yanafanywa na Dk Magufuli. Hata hivyo, alisema kwa kuwa anachofanya hakikuwamo katika mipango ya Chama cha Mapinduzi (CCM), anaamini atakumbana na changamoto siku zijazo. “Akiomba ushauri tutatoa kwa maana namna gani atekeleze, lakini ni mapema mno kusema kama ana dhamira ya kuyafanya. Pengine anayafanya kwa ajili ya kujitafutia umaarufu wa harakaharaka,” alisema Mwalimu. Mikakati ya Dk MagufulTangu Novemba 5 mpaka sasa, Dk Magufuli ametangaza mikakati kadhaa ya kubana matumizi ya Serikali, ili ...

Rais Dkt.Magufuli akutana na viongozi na wawakilishi wa umoja wa sekta Binafsi nchini

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Viongozi na Wawakilishi wa Umoja wa Sekta Binafsi nchini (Tanzania Private Sector Foundation - TPSF) katika ukumbi wa mkutano wa Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 3, 2015. PICHA NA IKULU

RAIS WA ZANZIBAR DK SHEIN AGEUKWA NA WAPAMBE WALIOMSHAWISHI AGOMBEE URAIS

Image
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umesema baadhi ya wapambe na vigogo waliompigia debe na kumshawishi Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, achukue fomu kuwania urais kwa mara ya kwanza mwaka 2010, hivi sasa wamemgeuka na baadhi yao wanamuona kikwazo kutokana na msimamo wake wa kimapinduzi usioyumba, wala kuogopa vitisho katika kuweka maslahi ya umma mbele. Akizungumza wakati alipokutana na makundi ya vijana wa CCM kutoka majimbo manne visiwani hapa jana ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi wa marudio Zanzibar, Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, alisema watu hao walitarajia Dk. Shein baada ya kuwa Rais angekuwa dhaifu, mwepesi na angekubali kutii na kushiriki usaliti dhidi ya uhuru na mapinduzi kwa manufaa ya wachache, lakini imeshindikana kutokana na Rais huyo kuweka mbele maslahi mapana ya Zanzibar na wananchi wake. "Madalali hao wa kisiasa hawakujua wala kufahamu kama Dk. Shein ni zao la mapinduzi. Laiti kama Dk. Shein asingelelewa, kuandaliwa n...

Aunt amfundisha ulevi Moze

Image
Staawa Bongo Movie, Aunt Ezekiel akiwa na mpenzi wake Moses Iyobo ‘Moze’. STAA wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel juzi kati baada ya kujitwika kilaji a.k.a masanga vilivyo, alijikuta akijigamba waziwazi kumfundisha ulevi mzazi mwenzake, Moses Iyobo ‘Moze’. Akichonga na kona ya Bongo Movie kwa sauti ya kilevi, Aunt alikiri kuwa mnywaji mzuri wa pombe hivyo kwenye maisha yake hategemei kukaa na mume zaidi ya miaka miwili halafu ashindwe kumshawishi kunywa naye pombe kwani huo utakuwa ni uzembe wa hali ya juu. “Nimejitahidi sana kumuwezesha Moze wangu kuanza alau kugusa kinywaji kilaini maana zamani kila nikimpatia pombe lazima akasirike. Nafurahi kuona sasa ameanza kuonjaonja hadi inafikia hatua anamaliza hadi chupa tatu,” alisema Aunt. Kwa upande wa Mose Iyobo alisema kwa sasa anakunywa bia tatu tu!