Posts

MAGUFULI AZUNGUMZA NA WAJUMBE WA JUMUIYA YA WAZAZI YA CCM

Image
Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli akiingia kwenye Ukumbi wa Karemjee kuzungumza na Wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi CCM. Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wajumbe hao. Dkt. Magufuli amewaomba wajumbe hao kufanya kazi kwa uadilifu na kuihubiri Amani ya nchi yetu ili maendeleo bora yaweze kupatikana. Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Abdalah Majura akizungumza katika mkutano huo. Wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi Taifa wakimshangilia Mgombea wa CCM-Dkt. John Magufuli.   Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Ushindi Adam Malima. Mgombea wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe hao.

NJEMBA Yafanyiwa KITU MBAYA Mbele ya Mkewe!

Image
  Akiminyiwa kichapo. Richard Bukos Hii kali! Njemba mmoja ambaye jina halikupatikana amekula kipigo mbele ya mkewe ambaye alifanikiwa kukimbia baada ya kudaiwa kufanya jaribio la kuingia kwenye onesho la Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ kwa kutumia tiketi feki, Ijumaa lina kisa na mkasa. Tukio hilo lililoshuhudiwa na mwanahabari wetu lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Ukumbi wa Club East 24 iliyopo Mikocheni jijini Dar ambapo jamaa huyo alifika kwa Bajaj, akiwa na mrembo matata aliyetinga viatu virefu vya mchongoko na kigauni kifupi. Wawili hao walishuhudiwa wakisogelea getini kwa mikogo huku wakiwa wameshikana viuno ambapo nuksi ilianzia pale walipowafikia wasimamizi wa getini na kuwaonesha tiketi. Katika hali ya kushangaza, ghafla jamaa huyo alishtukia akilambwa kofi la uso na baunsa wa Kampuni ya Black Ninja aliyefahamika kwa jina moja la Hamidu na kuanza kuhojiwa alikoipata tiketi hiyo. Wakati akijiandaa kujibu, yule mwanamke aliyekuwa naye

DK. SLAA KUJIUNGA NA UZINDUZI WA UKAWA JANGWANI”

Image
Wakati ambapo vyama vya upinzani vinatarajia kuzindua kampeni zake katika uwanja wa Jangwani kesho na kumnadi mgombea wake wa urais, Edward Lowassa, duru zinaeleza kuwa huenda Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa akahudhuria uzinduzi huo.Mmoja kati ya viongozi wa Chadema ambaye alinukuliwa na gazeti moja kubwa nchini huku akitaka jina lake lisitajwe, alisema kuwa zipo taarifa za chinichini ndani ya chama hicho zinazoeleza kuwa Dk. Slaa ataibuka Jangwani kesho“Zipo taarifa za chinini kuwa Dk. SSlaa atahudhuria uzinduzi, hatujui zina ukweli kiasi gani na atashiriki kama Katibu Mkuu au mgeni mwalikwa, kama atahudhuria, atatusaidia sana na asipokuja suala lake litaendlea kuwachanganya wafuasi wa Chadema,” alinukuliwa kiongozi huyo wa Chadema.Haijafahamika kama taarifa hizo ni za kweli au la kwa kuwa hata uamuzi wa kumkaribisha Edward Lowassa kujiunga na Chadema ulifanywa kuwa siri kubwa kwa viongozi wachache sana takribani miezi mitatu kabla. Hata viongozi wengine wa

SOMA MAGAZETI YOTE YA LEO IJUMAA HAPA

Image
. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . .

NEC YAKABIDHI POLISI MAJINA YA WATU 52,078 WALIOJIANDIKISHA ZAIDI YA MARA MBILI KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

Image
 Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Kailima Ramadhan (kushoto), akimkabidhi Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Benedict Wakulyamba orodha ya majina 52,078 ya watu waliojiandika katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa BVR zaidi ya mara mbili Dar es Salaam leo, kwa ajili ya uchunguzi na baadae hatua za kisheria zichukuliwe kwa wahusika.  Masanduku ya BVR yakiwa yamehifadhiwa Bohari ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.  Mkurugenzi wa Idara ya Daftari la mpiga kura, Dk. Sisti Cariah (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu hatua waliyoifikia kuhusu daftari hilo na shughuli mbalimbali zinazoendelea kufanywa na NEC kuelekea uchaguzi mkuu.  Mtaalami wa Tehama wa NEC, Fatuma Mkanguzi akiwaelezea wanahabari jinsi mfumo wa Tehama unavyofanyakazi.  Fundi, Francis Skale akiwa kazini.  Mafundi wa NEC wakiendelea na kazi.  Mtaalamu wa mfumo wa ulinzi wa NEC, Adolf Kinyelo akitoa maelekezo ya jinsi ya mfumo huo una