Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Jumanne Sagini (kulia) akizungumza jambo. Dar es Salaam. Serikali imetangaza ajira mpya za walimu 31,056 wanaotakiwa kuanza kazi kuanzia Mei Mosi, mwaka huu. Mbali na walimu, pia imetangaza ajira kwa mafundi sanifu wa maabara 10,625 ambao pia wataanza kazi sambamba na walimu hao.Akizungumza jana, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Jumanne Sagini alisema Serikali imetenga Sh9 bilioni kwa ajili ya posho za kujikimu na nauli kwa walimu na mafundi sanifu maabara. Alisema kiasi cha fedha kilichotengwa ni posho ya siku saba na fedha za nauli ambazo zinatakiwa kulipwa na halmashauri ambazo ndiyo mwajiri. Alisema posho hizo zinatakiwa kulipwa ndani ya siku saba na kwamba isizidi siku 14 tangu kuripoti kwa mwalimu katika kituo cha kazi. “Hatutapenda kusikia malalamiko kutoka kwa walimu hao, halmashauri zijipange kuwapokea waajiriwa wao wapya,”