'Magaidi wa Tanga' Watiwa Mbaroni.....Mwili wa Mwanajeshi wa JWTZ Aliyeuawa katika Mapigano hayo Waagwa
Serikali imetoa taarifa rasmi kuhusu uhalifu uliotikisa mkoani Tanga, ikisema hali ni shwari na umma wa Watanzania upuuze taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikitia hofu. Aidha, imesema watu kadhaa wanashikiliwa wakihusishwa na uhalifu huo. “Tunawashikilia ila mpaka sasa siwezi kukueleza idadi yao na kwamba ni wa kikundi cha ugaidi au la. Hao watu tunafanya nao mahojiano ili kuweza kuelewa kama wanahusika kwenye tukio hilo,” alisema Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Juma Ndaki. Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Ndaki alisema hali katika kitongoji cha Majimoto, Amboni na mkoa wa Tanga kwa ujumla iko shwari. “Tunaendelea kufanya uchunguzi kubaini hao wahalifu pamoja na silaha zilizoibwa,” alisema. “Tunaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano wao hasa wanapoona watu wenye majeraha au wanaowahisi kwamba ni wahalifu ili nasi tuweze kuwachunguza kama wanahusika kwenye tukio hili”, alisema. Ingawa Kamanda hak