Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (katikati), akiongozwa polisi kuingia kwenye gari baada ya kutokea vurugu meza kuu, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Goba, Kinondoni Dar es Salaam, ambazo alidai zilipangwa kwa makusudi na viongozi wa Chadema kwa lengo la kumvulugia ziara yake ya kuwaelezea wananchi utekelezaji wa Ilani ya CCM katika suala la upatikanaji wa maji ya uhakika jijini Dar es Salaam ifikapo Septemba, mwakani. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG Gari lililombeba Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla, likilindwa na polisi lililopokuwa linaondoka baada mkutano wa hadhara kuvunjika kulikosababishwa na vurugu ambazo waziri alidai kuwa zilipangwa kwa makusudi na wafuasi pamoja na viongozi wa Chadema waliokuwa wakirumbana na viongozi wa CCM, katika Kata ya Goba, Kinondoni, Dar es Salaam. Makalla alikuwa katika ziara ya kukagua miradi ya maji katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani. Makalla akijadiliana na maofisa wa CCM na P...