TANZANIA YA KWANZA AFRIKA MASHARIKI KATIKA USAFIRI WA MABASI YAENDAYO KASI – PINDA
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Majadiliano wa Kutangaza Mradi wa Mabasi yaendayo haraka kwenye ukumbi wa Mlimani City jijiniDar es salaam Juni 3, 2014. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Hawa Ghasia(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri Mkuu,, Mizengo Pinda akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia nchini, Bw. Philippe Dongier baada ya kufungua Mkutano waMajadiliano wa kutangaza Mradi wa Mabasi yaendayo haraka kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam Juni 3, 3014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi za kwanza katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kuingia kwenye ubia nasekta binafsi katika mradi mkubwa wa usafirishaji abiria. Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Juni 3, 2014) wakati akifungua Mkutano wa Majadiliano yenye lengo la kuutangaza mradi wa mabas