Posts

HOFU YATANDA: BINTI ALIYEZIKWA AIBUKIA KWAO

Image
Witness Obed (21) aliyefariki dunia Aprili 12 mwaka huu na kuzikwa kwenye makaburi ya nyumbani kwao Kijiji cha Nanja, mkoani Arusha na kuibuka akiwa hai tena. HOFU  ya ushirikina imetikisa Mkoa wa Arusha kufuatia tukio la hivi karibuni ambapo mwanafunzi wa Chuo cha Kompyuta jiji hapa, Witness Obed (21) aliyefariki dunia Aprili 12, mwaka huu na kuzikwa kwenye makaburi ya nyumbani kwao Kijiji cha Nanja, Kata ya Moshono wilayani Arumeru, Arusha kuibuka akiwa hai. Binti huyo aliibuka kwao hivi karibuni akiwa mpole na kuwafanya baadhi ya watu, wakiwemo wazazi wake kutimua mbio kwa hofu. Watu kutoka maeneo mbalimbali jijini hapa  wamekuwa wakimiminika nyumbani kwa wazazi wa binti huyo kwa lengo la kumshuhudia kwa vile ndugu walishaamini kuwa, mpendwa wao huyo alishakufa na alizikwa. Umati wa watu ukiwa katika hali ya mshangao kutokana na tukio hilo. UWAZI LATIA TIMU NYUMBANI Baada ya kusikia taarifa hizo, Uwazi lilifunga safari mpaka eneo la t...

ANGALIA PICHA MAJAMBAZI WALIOUWAWA TEMEKE

Image
Mwili wa jambazi mwingine ukiwa umeharibika vibaya baada ya kipigo kikali kutoka kwa wananchi wenye hasira. Mwili wa mmoja wa majambazi ukiwa chumba cha kuhifadhia maiti 

HII NDO JEURI YA PESA YA H-BABA ...CHEKI GARI JIPYA LA KIFAHARI

Image
  Maisha ya mastar wetu wa Kitanzania yanazidi kukua zaidi na kuwapelekea kumiliki baadhi ya vitu vya gharama,baada ya baadhi ya wasanii kuonyesha magari yao,hili ndilo gari sasa analotembelea mume wa Frola Mvungi hit maker wa Mpenzi Bubu,Poteza na hit zingine H.baba. Mbali na muziki H.baba amesema kuwa vyanzo vingine vya mapato ni pamoja na bidhaa zake za pipi alizozizindua miezi michache iliyopita zinazopatikana Mwanza pekee pamoja na uigizaji wa filamu mbalimbali za Kitanzania. Hii gari aina yake ni Mr s ambalo buti yake iko kwa mbele sehemu ambayo ipo engine yake,hapo chini nimekuwekea bei kama uki google ingawa kwa pesa za Kitanzania ni zaidi ya Milioni 70 kwa bado kuisafirisha na ushuru.

ANGALIA PICHA MATESO ANAYOPATA HUYU.MSAADA WAKO UNAHITAJIKA

Image
MWANAFUNZI wa kidato cha nne nchini Burundi, Miburo Anne Mony (17), raia wa nchi  hiyo amesema anakwenda kufia kwao baada ya madaktari ya Hospitali ya Taifa Muhimbili kumwambia ugonjwa wake wa kansa umecheleweshwa hivyo si rahisi kutibika. HAJUI ATARUDIJE NYUMBANI Akizungumza na mwandishi wetu huku akibubujikwa machozi ndani ya Wodi Na. 24, Sewa Haji, Muhimbili, mwanafunzi huyo wa kike ambaye hajui Kiswahili wala Kingereza vizuri alisema hajui atarudije kwao Burundi kwa kuwa hana fedha baada ya kuishiwa. Aliongeza kwamba alikuwa na matarajio kuwa angepata matibabu hapa Tanzania baada ya huko kwao kushindikana. UGONJWA ULIVYOANZA “Ugonjwa huu ulianza kama uvimbe nikiwa kidato cha kwanza, ulikuwa ikiwasha kupita kiasi, ulizidi kuvimba kwa kasi ya ajabu, nikakatisha masomo kwa vile nilianza kupata maumivu makali mno. “Mama alianza kuhangaika kwa kunipeleka katika hospitali mbalimbali kule kwetu Burundi bila mafanikio. “Mama yangu ni mkulima, hana...

TAIFA STARS YATUA DAR KUPEPETANA NA MALAWI, TFF YAWAOMBA MASHABIKI KUFURIKA UWANJANI

Image
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam TIMU ya Taifa ya Tanzania chini ya kocha mkuu, Mholanzi, Mart Nooij inatarajia kujipima ubavu katika mechi ya kimataifa ya kirafiki jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam  dhidi ya timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) kuanzia majira ya saa 11:00 jioni. Taifa Stars iliyopiga kambi yake mjini Tukuyu jijini Mbeya inatarajia kuwasili asuhubi hii majira ya saa 4:00 katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ndege ya Air Tanzania. Wapinzani wa Taifa stars tayari wapo jijini Dar es salaam kwa ajili ya mechi hiyo muhimu kwa makocha  kuangalia uimara wa timu zao kabla ya kwenda kucheza mechi za mashindano.

BREAKING NEWZZ MSANII MWINGINE TENA ''RECHO'' AFARIKI DUNIA ASUBUHI HII

Image
Msanii wa Bongo Movie, Rachel Haule 'Recho' (pichani), amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es slaaam. Habari zilizotua Global na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Nyerere, zimesema kuwa Recho alikwenda Muhimbili jana kujifungua ambapo mara baada ya kujifungua mtoto alifariki na yeye hali yake kuwa mbaya, ilibidi ahamishiwe ICU ambako hali ilizidi kuwa mbaya na baadae kufariki dunia. Kifo cha Recho kimekuja ndani ya wiki moja baada ya kufariki kwa msanii mwingine wa Bongo Movi Adam Kuambiana Jumamosi iliyopita, kifo hiki kimeleta mstuko mkubwa kwenye tasnia ya ya filamu za kibongo. Habari na picha zaidi zitawajia baadae.  PICHA: Makatab za GPL

VIATU VYA KANUMBA VYAKOSA MVAAJI, BONGO MOVIE NA WATAYARISHAJI FILAMU WALALAMA

Image
Wasambazaji wa filamu wanasema hakuna mauzo tena ya filamu toka kifo cha marehemu Steven Kanumba, wanalalamika kuwa mauzo yameshuka sana hadi hata wengine kuachana na biashara hiyo na kuamua kufanya biashara nyingine zinazowalipa. Inawezekana maneno yao yakawa sahihi au si sahihi, kutokana na hali halisi ya mfumo wa tasnia ya filamu ulivyo hasa katika idara ya mauzo, sasa kila mtu anajaribu kutafuta sehemu gani ya kuangukia ndio tunasikia wakisema kuwa toka kifo cha Kanumba hakuna mauzo ya filamu. Hayati Steven Kanumba Mtayarishaji na mwigizaji Nyota Swahiliwood Kanumba akiwa katika pozi Umati wa watu siku ya mazishi ya Kanumba Hayati Kanumba akiwa na mwigizaji wa kimataifa Ramsey Noah kutoka Nigeria Enzi za uhai wake Kanumba the Great Ni kweli hakuna ubishi kuwa Kanumba alikuwa na mvuto wa kipekee katika tasnia ya filamu Bongo lakini hatuna mbadala wake? Ambaye anaweza kuvaa viatu vyake na kuifanya tasnia ya filamu ifanye vizuri kam...

PICHA ZA VIJANA WA MBWA MWITU NA PANYA ROAD WALIOKAMATWA NA JESHI LA POLISI BAADA YA KUWA TISHIO KWA WANAINCHI KWA MDA MREFU

Image
Hawa ndio viongozi wa panya road na mbwa mwitu ambao tayari wameshakamatwa  Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanya msako wa nyumba kwa nyumba, mtaa na maeneo yaliyoathirika kwa hofu ya vijana ambao ni vibaka maarufu kama Mbwa mwitu au Panya Road.  Msako huu uliofanyika ndani ya masaa 24 hadi alfajiri ya tarehe 26/5/2014 kwa lengo la kuwaondolea hofu na uhalifu dhidi ya makundi ya vijana wadogo wasio na ajira ambao uliibuka hivi karibuni.         Maeneo yaliyoathirika ni Kigogo, Magomeni, Tabata, maeneo yote yanayozunguka mto Msimbazi, maeneo ya Mbagala nk.  Msako huu unaendelea kufanywa na askari wa vikosi maalum ambao wamepewa kazi ya kuhakikisha kuwa vikundi hivyo haviibuki tena na vinatokomezwaa kabisa kwa  kuwakamata wale wote wanaojihusisha na vitendo vya kuvamia kwa mkundi wananchi ambao hawana hatia Kamishna kova ambaye amezungumza na wanahabari muda mfupi uliopita  Kati ya watuhumiw...

TAZAMA PICHA NYINGINE ZA HARUSI YA KIM KARDASHIAN na KANYE WEST

Image
Hii ni mara ya tatu kwa Kim kuolewa ila kwa Kanye West hii ni mara ya kwanza. Hatimaye wawili hao walifunga pingu za maisha mnamo siku ya Jumamosi May 24 pande za Fort di Belvedere ndani ya Florence, Italy.                                      Baadhi ya wana familia na marafiki walikuwepo ila ni wale ambao Kanye West kweli aliwahitaji, na baadhi yao hawakufika. Jay Z na Beyonce wa waliingia mitini. Hongera kwao kanye west na kim kwa kufunga ndoa tukiamini kwamba safari hii kweli KIm yupo kwenye mapenzi ya kweli.

Mtumishi wa idara ya Afya Afia Gesti

Image
Mwili wa Marehemu Munuo ukitolewa katika Gesti hiyo Mwili wa Marehemu Munuo ukiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Kahama Mtumishi wa idara ya Afya katika halmashauri ya mji wa kahama, Mkoani Shinyanga, Jeremiah Munuo (50) amekutwa amefariki dunia katika nyumba moja ya kulala wageni mjini Kahama.  Taarifa kutoka jeshi la polisi wilayani humo zimesema kwamba Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo katika nyumba hiyo iitwayo KK Lodge iliyopo jirani na ofisi za Halmashauri ya Mji wa Kahama.  Taarifa zimesema watumishi wenzake walikwenda kumuona leo majira ya saa 6 mchana baada ya simu yake kuita bila kupokelewa kwa muda mrefu.  Jesh la polisi wilayani Kahama limefika katika eneo la tukio na kumkuta marehemu Munuo ambaye alikuwa na miezi 3 tu tangu ahamishiwe katika halmashauri hiyo akiwa na Fedha taslimu shilingi 596,000 na simu nne za mkononi.  Mwili wa marehemu Munuo umepelekwa kuhifadhiwa katika chumba cha ku...