Posts

BABA AMNYONGA MWANAE MWENYE UMRI WA MWAKA MMOJA NA MIEZI SABA KISHA KUACHA UJUMBE TUTAFUTE PESA KWANZA NIITE J.M A.K.A GAIDI

Image
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI     MTOTO MWENYE UMRI WA MWAKA MMOJA NA MIEZI SABA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA HENRY JUMA MKAZI WA MIGOMBANI ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUNYONGWA SHINGO KISHA KULAZWA KITANDANI NA BABA YAKE MZAZI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JUMA VENANCE. TUKIO HILO LA KUSIKITISHA LIMETOKEA MNAMO TAREHE 22.03.2014 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI HUKO KATIKA KATA YA MIGOMBANI, TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA YA MOMBA AMBAPO BAADA YA UHALIFU HUO, MTUHUMIWA ALIFUNGA MLANGO KWA NJE NA KUFULI NA KUTOKOMEA MAHALI KUSIKOJULIKANA. WAPELELEZI PAMOJA NA RAIA WALIPOVUNJA MLANGO NA KUINGIA NDANI WALIKUTA MAITI YA MTOTO HUYO IKIWA KITANDANI. KATIKA CHUMBA HICHO WALIKUTA UJUMBE WA MANENO MENGI YALIYOANDIKWA NA MTUHUMIWA, BAADHI YA MANENO HAYO NI:- “ UNYAMA UNYAMANI, TUTAFUTE PESA KWANZA NIITE J.M A.K.A GAIDI” .  JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. M

STENDI KUU YA MABASI MOSHI,WAMILIKI WA MABASI MADOGO WAGOMA KUTOA HUDUMA

Image
Kituo kikuu cha mabasi yaendayo sehemu mbalimbali ndani ya mkoa wa Kilimanjaro na Arusha ikiwa haina gari baada ya wamiliki wa magari yaendyo maeneo hayo kugoma kutoa huduma. Kutokana na mgomo huo ndipo madereva wa magari hayo na makondakta wakaamua kugeuza stendi hiyo uwanja wa mpira wa miguu likapigwa mbungi kati ya madereva na makondakta. Ndipo askari walipoamua kuingilia kati na kuzuia mchezo huo uliokuwa hauna waamuzi wala milingoti ya kufunga magoli. Ulinzi ukaimarishwa zaidi.   Baadhi ya makondakta na madereva wa magari hayo wakatiwa mikononi. Hata hivyo hatua ya kukamatwa kwa madereva na makundakta kiliwatia hasira wapiga debe wakaamua kulipopoa gari la polisi kwa mawe na kuvunja kioo cha nyuma kama inavyoonekana hapa. Abiria walilazimika kupanda gari la kusafirisha magazeti.Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii ,Moshi

ANGALIA NAFSI ZA KAZI MPYA KUTOKA MASHIRIKA MBALIMBALI

Image
GENDER AND NUTRITION SPECIALIST Apply before:  31 Mar 2014 COMPANY:  TANZANIA HORTICULTURAL ASSOCIATION (TAHA) Location >  Arusha  Position Type >  Full Time  Organization Type >  Parastatal POSITION DESCRIPTION: From the Daily News of 20th March Tanzania Horticultural Association (TAHA) is an apex private sector member based organization mandated to devefe,p and promote the horticultural industry (flowers, fruits, vegetables, spices, herbs and horticultural seeds) in Tanzania. TAHA's goal is to improve the growth and competitiveness of horticultural industry in the country for social and economic gains. TAHA is an effective voicing platform representing value chain actors (fanners, processors, exporters and service providers) in the industry. TAHA is looking for qualified candidates for fill the below vacancies: Gender and Nutrition Specialist The Association is looking for a dynamic and experienced Gender and Nutrit

MTALII ALIYEKWAMA KILELE CHA MAWENZI MLIMA KILIMANJARO AOKOLEWA.

Image
Mtalii  Jeanne Traska kutoka Ujerumani Bi.Jeanne Traska kutoka Ujerumani na Muongoza Wageni Athumani Juma wakiwa katika Lango la Marangu pamoja na vifaa mbalimbali walivyokwama navyo katika kilele cha Mawenzi Mlimani Kilimanjaro mara baada ya kuokolewa. Kikosi cha Uokoaji katika Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro kimefanikiwa kumuokoa mtalii Bi. Jeanne Traska (32) kutoka Ujerumani  pamoja na muongoza wageni Athuman Juma ambao jana walikwama katika kilele cha Mawenzi  Mlimani Kilimanjaro. Kikosi cha Uokoaji cha TANAPA kiliweza kufika eneo la  kilele cha Mawenzi na kwa kutumia mbinu za uokoaji za kisasa kabisa kiliweza  kuwanasua majira ya kumi na moja jioni. Licha ya hali mbaya ya hewa iliyotokana na mawingu mazito katika eneo hilo, Kikosi cha Uokoaji cha TANAPA kiliweza kukabiliana na hali hiyo na kuweza kuwanasua na kisha kuwapeleka katika kituo cha Horombo majira ya saa mbili usiku ambapo walichukuliwa na gari kupitia njia maalum ya uokoaji na kufika katika Lango

BREAKING NEWSS:::WATU WAWILI WAUAWA KANISANI KENYA

Image
  Baadhi ya waumini wa Kanisa la Joy Jesus wakiwa nje ya kanisa baada ya shambulio hilo. WATU wawili wameuawa wakati wengine kumi wakijeruhiwa baada ya mtu mmoja aliyejihami kwa bunduki kuwafyatulia risasi ndani ya kanisa la Joy Jesus huko Lokoni, karibu na Mombasa nchini Kenya. Maafisa wa polisi katika wilaya ya Likoni iliyopo kusini mwa Mombasa wamesema kuwa jambazi huyo alilivamia kanisa hilo na kuanza kuwafyatulia risasi waumini hao kiholela. Bado haijafahamika kama muuaji huyo ana uhusiano na vikundi vya kigaidi

TATIZO LA HARUFU MBAYA UKENI

Image
Tatizo la uchafu ukeni Leo tutazungumzia tatizo linalowasumbua wanawake wengi, tatizo la kutokwa na uchafu unaotoa harufu mbaya sehemu za siri. Kitaalamu hali ya mwanamke kutokwa na majimaji yenye rangi nyeupe au ya njano,  ni hali ya kawaida na wala siyo tatizo endapo majimaji hayo siyo mazito sana na wala hayatoi harufu mbaya. Lakini endapo majimaji yanayotoka yapo katika hali ya ute mzito wenye rangi nyeupe au kahawia, yanatoa harufu kali na yanawasha, basi hiyo ni ishara ya ugonjwa uitwao Vaginosis. Majimaji au ute unaoteleza kutoka sehemu za siri ni njia inayowezesha viungo vya uzazi vya mwanamke kujisafisha na kuutoa uchafu wa seli zilizokufa na mabaki ya damu ya hedhi nje ya mwili. Pia huvikinga viungo vya uzazi dhidi ya maambukizi ya bacteria au fangasi wanaoleta magonjwa. Kwa kawaida huwa hayatoi harufu na huwa na rangi nyeupe au ya njano. Pia huwa na asidi ya Lactic ambayo huzuia kuzaliana kwa vijidudu vya maradhi na huzalishwa kwenye tezi za B