MBUNGE WA CHADEMA IRINGA MJINI AMFAGILIA RAIS KIKWETE KATIKA KUHAKIKISHA KATIBA MPYA INAPATIKANA.
Mbunge wa jimbo la Iringa Mjini,Mh.Peter Msingwa amefanya mkutano hapo jana katika viwanja vya Mwembetogwa, mkoani humo.Mkutano huo ambao ulikuwa wa kufungia mwaka 2013 ,Msigwa pia aliutumia mkutano huo kwa kuwapongeza baadhi ya mawaziri ambao utendaji kazi wao unaonekana kuwa mzuri,akiwemo Waziri wa Wizara ya Maji na Naibu Wake ,Waziri wa Ujenzi na Waziri wa Mazingira ambao wameonesha msimamo wa kweli katika kuwatumikia wananchi . katika hatua nyingine mbunge Msigwa amemshukia aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema,Zitto Kabwe na kusema kuwa anatafuta umaarufu binafsi kuliko kukijenga chama chake na kuwa hana nia njema na CHADEMA,hivyo amewataka Wanachadema wa jimbo la Iringa mjini kutomsikiliza huku akibainisha kuwa Mwanachama na Kiongozi mzuri ni yule ambae anafanya kazi ya kuk...