Mwanafunzi wa darasa la 3 auawa na baba wa kambo kwa kupigwa
Mtoto Baraka Deogratias mwenye umri wa miaka tisa ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Kitunda jijini Dar es Salaam,amedaiwa kuuawa na baba yake wa kambo baada ya kumpiga kwa kosa la kutosahishiwa baadhi ya madaftari yake ya shule na kusababisha mtoto huyo kupoteza maisha. ITV ilifika nyumbani kwao marehemu Baraka Deogratias ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Kitunda,na kukuta ndugu jamaa na marafiki wakiwa katika msiba huo,ambapo mama mzazi wa marehemu Baraka Bi Veronica Jeremiah amesema siku ya Jumamosi ya tarehe 5 Octoba 2013 saa 2 usiku mume wake bwana Masaka Limbu alifika nyumbani na kuanza kukagua madaftari ya watoto wawili ambao ni Pita masaka ambaye ni mtoto halali wa mtuhumiwa na Baraka Deogratias ambaye ni mtoto wa kambo ... Wakiwa chumbani na baba yao alisikia kilio cha mtoto wake ambaye hakuzaliwa na mume huyo akilia kwa uchungu lakini alipofika alikuta hajiwezi na alipomkimbiza katika zahanati