POLISI TANZANIA KUPATA MAFUNZO YA UPELELEZI NCHINI UTURUKI
Na Tamimu Adam, Jeshi la Polisi Jeshi la Polisi la Uturuki limetoa ufadhili wa masomo kwa askari kumi na saba ( 17) wa Jeshi la Polisi Tanzania kupata mafunzo mbalimbali yakiwemo ya upelelezi wa wahalifu na mbinu za uchunguzi wa kimaabara pamoja na usimamizi na uendeshaji wa gari la matukio yatakayochukua muda wa mwezi mmoja nchini Uturuki. Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya jinai nchini (DCI) Kamishina Robart Manumba aliyasema hayo jana wakati wa kikao cha kazi kilichofanyika Makao Makuu ya Polisi. Alisema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya maboresho yanayolenga kuwaongezea askari weledi na kuwajengea uwezo wataalamu wa Maabara ya uchunguzi ya Polisi juu ya mbinu mbalimbali za kiuchunguzi na upelelezi pamoja na matumizi sahihi ya vifaa vya kiupelelezi. Aliongeza kuwa mafunzo hayo yatasaidia wataalamu wa Maabara ya uchunguzi ya Polisi kuweza kufanikisha kuwakamata wahalifu na kutambua uhalifu uliotendeka kwa haraka, hivyo, ku