Posts

DALADALA YANUSURIKA KUINGIA BUCHANI MWENGE

Image
Daladala lenye namba za usajili T 741 AEG baada ya kuhama njia na kuparamia mtaro uliopo jirani na bucha eneo la Mwenge. Daladala lenye namba za usajili T 741 AEG linalofanya safari zake kati ya Temeke na Mwenge asubuhi hii nusura liingie katika bucha iliyopo maeneo ya Mwenge jijini Dar katika barabara iendayo Afrika Sana.  Daladala hilo lilisaidiwa na mtaro uliopo mbele ya bucha hiyo baada ya dereva wake kushindwa kuliongoza na kuhama barabara.  Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwa eneo la tukio, daladala hilo halikuwa na abiria na hakuna mtu aliyejeruhiwa. JIUNGE NASI KWA KUBOFYA LIKE FACEBOOK PAGE KWA HABARI MOTO MOTO

SAKATA LA MADAWA YA KELEVYA, RIPOTI KAMILI HII HAPA

Image
Na Mwandishi Wetu WATANZANIA ambao idadi yao inaweza kupita mamia, wameshanyongwa nchini China kutokana na kupatikana na hatia ya kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya. Ripoti maalum ya madawa ya kulevya, iliyofanyiwa kazi na gazeti hili kwa kukusanya taarifa ndani ya nchi, Afrika Kusini na China kwenyewe, inaweka hadharani siri ya mamia ya Watanzania kunyongwa. Katika ripoti hiyo, inaonesha kwamba mataifa ya Afrika Kusini na Uganda, yapo mstari wa mbele kuripoti taarifa za raia wao kunyongwa China lakini Tanzania imekuwa ikisuasua. “Huu ukimya wa serikali yetu, unafanya wengi kukosa taarifa sahihi, matokeo yake wanajiingiza kwenye biashara hiyo haramu ambayo mtu akikamatwa tu China na akikutwa na hatia lazima anyongwe,” alisema Joel Mabruki, mfanyabiashara wa nguo na simu kati ya Tanzania na China. Mabruki aliongeza: “Kama serikali yetu ingekuwa na utaratibu wa kutangaza kila Mtanzania anayenyongwa China, pengine vijan...

BINTI ABAKWA NA KUCHOMEKWA MIWA SEHEMU ZA SIRI

Image
Mdada mwenye miaka 9  mkazi wa kijiji kimoja nchini brazil,mapema wikiendi  hii amebakwa karibu na shamba la miwa na watu wanaoaminika kuwa ni watumiaji wa madawa ya kulevya...  Baada  ya  kumbaka, vijana  hao  walimchoma  na  miwa  katika  sehemu  zake  za  siri  na  kumsababishia  maumivu  makali  yaliyomfanya  apoteze  maisha...

WANAJESHI WENGINE WATATU WA TANZANIA WAFARIKI DUNIA HUKO SUDANI, MAPIGANO MAKALI YAIBUKA HUKO KONGO KATI YA SERIKALI NA WAASI WA M23

Image
WINGU zito limetanda kwa askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), katika nchi za Sudani Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).    Wakati Watanzania wakiendelea kuomboleza vifo vya wanajeshi saba wa jeshi hilo waliopoteza maisha katika Jimbo la Darfur, Sudani kwa kushambuliwa na waasi, nchini DRC yamezuka mapigano makali baina ya waasi na majeshi ya Serikali.     Mapigano hayo yameripotiwa kuibuka kati ya Wanajeshi wa Serikali na waasi karibu na mji wa Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Msemaji wa wapiganaji wa waasi wa M23, ameliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) kuwa ndege za kivita za Serikali zimefanya mashambulio ya anga katika maeneo yao usiku wa kuamkia jana. Umoja wa mataifa kwa upande wake umesema uko tayari kutumia nguvu, kuwalinda raia ikiwa wapiganaji hao wa M23 wataingia katika mji wa Goma. Raia wakimbia mapigano Wakati huo huo, mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu,...

RAGE: MKUTANO MKUU SIMBA AGOSTI 20

Image
WEKUNDU wa Msimbazi Simba “Taifa kubwa” wanatarajia kufanya mkutano mkuu wa wanachama Agosti 20 mwaka huu jijini Dar es salaam ili kujadili mambo mbalimbali yahusuyo maendeleo ya klabu hiyo. Mwenyekiti wa klabu ya Simba ambaye ni mbunge wa Tabora mjini, Alhaji Ismail Aden Rage amesema kwa kawaida mkutano huo ulitakiwa kufanyika Agosti 5 kwani mwaka jana ulifanyika tarehe hiyo, lakini wamelazimika kusogeza mpaka tarehe tajwa ili kuepukana na mwezi mtukufu wa Ramadhan. (HM) Rage alisema katika mkutano wa mwaka huu kutakuwa na ajenda mbalimbali ambazo zitajadiliwa na wanachama halali wa klabu hiyo. Mwenyekiti huyo alisema ajenda ya kwanza itakuwa ni kujadili taarifa ya ukaguzi wa fedha za klabu, na baada ya kujadiliwa kwa ajenda hiyo, watajadili ya pili ambayo ni mipango endelevu ya klabu hiyo. Rage aliendelea kueleza kuwa ajenda ya tatu ni Taarifa ya klabu itakayosomwa na katibu mkuu Evodius Mtawala, baada ya hapo wanachama wa...

HALI YA MZEE MANDELA YAWAACHA MIDOMO WAZI MARAFIKI ZAKE

Image
Mzee Nelson Mandela. Mke wa Nelson Mandela amesema hana wasiwasi na afya ya mumewe kama alivyokuwa wiki moja iliyopita. “Anaendelea kupokea matibabu vizuri,” amesema Graca Machel. Hata hivyo kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 94 anaelezwa kuwa katika hali mbaya, ikiwa ni wiki ya tano sasa hospitalini.  Juzi Rais Jacob Zuma alisema mpambanaji huyo dhidi ya ubaguzi wa rangi wa watawala wachache weupe wa Afrika Kusini “ameendelea kuwa mpiganaji imara hivi sasa kama ilivyokuwa miaka 50 iliyopita.” Alilazwa tangu Juni 8 kutokana na matatizo ya mapafu. Wiki jana, Zuma alikanusha madai kuwa Mandela hivi sasa hajitambui. Watu wengi ambao wamemwona tangu hapo wamekuwa wakisema anajitambua na ana hisia.   BBC imeripoti kuwa Graca amekuwa pembeni mwa kitanda cha Mandela muda wote hospitalini hapo-Medi-Clinic, Pretoria-na amekuwa akijitenga na mgogoro wa kisheria ndani ya familia ya kiongozi huyo ambao umewekwa hadharani katika wiki chache zi...

ANGALIA PICHA ZA NDEGE YA MH.RAIS JAKAYA KIKWETE WA TANZANIA

Image
Hii ndio Ndege ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inatambulika kama 5H - ONE Posted by Phars Nyanda at 09:58 AM No comments: Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook Read more: http://phars.blogspot.com/#ixzz2Z5vn0MkQ

JWTZ KUONGEZA NGUVU ZAIDI DARFUR BAADA YA VIFO VYA ASKARI WAKE SABA...

Image
  Mkurugenzi wa Habari na uhusiano wa Jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ), Kanali Kapambala Mgawe alipokuwa akizungumzia kuuawa kwa askari 7 wa Tanzania na wengine 14 kujeruhiwa na waasi Darfur Sudan juzi. Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), linatarajia kuongeza nguvu ya kujilinda, wakati wa kulinda amani katika Jimbo la Darfur nchini Sudan, ili kujikinga na mashambulizi kama la juzi, ambalo lilisababisha askari wake saba kupoteza maisha. Msemaji wa JWTZ Kanali Kapambala Mgawe, alisema hayo jijini Dar es Salaam jana, wakati akizungumzia shambulio hilo, lililosababisha pia majeruhi wengine 14. Kauli hiyo imetolewa wakati Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais Jakaya Kikwete akiungana na Watanzania wote na hasa maofisa na wapiganaji wa JWTZ na familia za wafiwa, kuomboleza vifo vya vijana hao hodari wa Tanzania. Kanali Mgawe alisema mawasiliano yanafanyika kati JWTZ na Umoja wa Mataifa (UN), kuhusu uwezekano w...

MIKAKATI YA KUMKAMATA FREEMAN MBOWE YAANZA...POLISI WAMVAMIA USIKU WA MANANE...

Image
KUNDI la polisi wenye silaha za moto juzi usiku walivamia nyumbani kwa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, kwa nia ya kumkamata. Askari hao wanaokisiwa kufikia saba, wakiwa na silaha nzito katika gari la wazi waliwasili nyumbani kwa Mbowe majira ya saa saba na nusu usiku na kuwaamuru askari wanaolinda nyumbani kwake kumtoa Mbowe nje ili waonane naye. Walinzi wa Mbowe walihoji uhalali wa ukamataji huo na kuwataka polisi wawaoneshe hati ya kumkamata, lakini hawakuweza kuionesha, hali iliyozusha wasiwasi kwa walinzi wa kiongozi huyo. Hata hivyo walinzi hao waliwaambia polisi hao kuwa Mbowe ambaye pia ni kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani bungeni alikuwa safarini, jibu ambalo lilipokewa kwa shingo upande na askari hao. Polisi hao baada ya kuona wameshindwa kukamilisha kazi hiyo, waliwaachia walinzi hao namba ya simu 0754-085600 ya Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Ernest Kimola, wakiwaagiza kuhakikis...

ASILIMIA 7 YA WATU WAZIMA TANZANIA WANA KISUKARI...

Image
Asilimia saba ya watu wazima nchini wanaumwa kisukari huku theluthi moja kati yao, haina uelewa juu ya ugonjwa huo, jambo linalosababisha wafike hospitalini katika hali mbaya. Taarifa hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi.  Aidha, alizungumzia ugonjwa wa shinikizo la damu na kusema theluthi moja ya watu wazima wameathirika na asilimia 10 ndio wenye uelewa wa ugonjwa huo. Dk Mwinyi alisema hayo jana wakati akizindua  gari la  Chama cha Kisukari nchini (TDA) la kutoa huduma ya kliniki kwa wenye kisukari, shinikizo la damu pamoja na magonjwa mengine.  Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa TDA, Dk Kaushik Ramaiya, wapo watoto 900 wenye ugonjwa huo wa umri kati ya miaka minne na  21 na kwamba kwa walio na umri chini ya miaka 15 wako wagonjwa 475. Waziri alisema idadi kubwa ya watanzania wamekuwa hawana utaratibu wa kupima afya zao. Alisema hufika wakati wakiwa kati...

WAKATI NANDO AKIHANGAIKA NA GONJWA LA ZINAA ALOPEWA, FEZA NAYE AMETANGAZA NIA YAKE YA KUZALISHWA NDANI YA JUMBA LA BIG BROTHER

Image
Huenda Jay (mtoto wa kiume wa Feza Kessy) anaweza kupata wadogo zake wa kucheza nao soon. Hiyo ni kutokana na mama yake anayeiwakilisha Tanzania mwaka huu kwenye shindano la Big Brother Africa ‘The Chase’ kumwambia mchumba wake raia wa Botswana, Oneal kuwa angependa azae naye watoto. Wapenzi hao waliopo Ruby House walikuwa wakiongea mipango kuhusu uhusiano wao kwenye chumba cha Rendezvous mjengoni humo.   “Please put a little thought into your answers,” anasikika Oneal akimwambia Feza.   “Natamani tungekuwa na mazungumzo haya bila kamera zozote zinazotuzunguka,” Feza alimjibu Oneal. Lakini baadaye alimjibu, “Nataka furaha na wewe, future, nataka mahaba, nataka watoto, nataka maisha na wewe.”  Hata hivyo Feza amekisema kitu kinachomkwaza toka kwa Mbotswana huyo anayefanya kazi ya UDJ nchini mwao kuwa wanapokorofishana yeye huondoka bila kuyamaliza japo amesema atajaribu kumwelewa.   “I know I am a complex man, I don’t even unders...

SHEIKH MKUU WA WILAYA YA ARUMERU AMWAGIWA TINDIKALI NA KUUMIZWA VIBAYA

Image
Shekhe Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Said Juma Makamba amejeruhiwa vibaya kwa kumwagiwa maji yanayohisiwa kuwa tindikali na watu wasiojulikana juzi usiku akiwa nyumbani kwake jijini Arusha. Shekhe Makamba, ambaye amelazwa katika Wodi ya Majeruhi kwenye Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, amejeruhiwa vibaya maeneo ya usoni, kifuani na mgongoni huku akiendelea na matibabu. Akizungumza kwa tabu, shekhe huyo alisema tukio hilo lilitokea saa 5 usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake kwa Mromboo Arusha, wakati akijiandaa kulala baada ya kutoka kuswali Swala ya Tarawei. Shekhe Makamba ambaye pia ni Imamu wa Msikiti wa Sekei mjini Arusha, alisema baada ya swala hiyo alirejea nyumbani kwake akisindikizwa na vijana wawili ambao walikuwa wakiswali pamoja na kuingia ndani ya nyumba yake ili kulala. Alisema hata hivyo, kabla ya kulala alikwenda kujisaidia katika choo cha nje na kwamba wakati akirudi ili aingie ndani akipitia nyuma ya nyumba ghafla alimuona mtu akiwa...

BENKI YA CRDB YAFUTURISHA WATEJA WAKE MJINI ZANZIBAR

Image
Mkurugenzi wa Masoko , Utafiti na Huduma kwa Wateja  wa  CRDB  ya Benki,  Tully Esther  Mwambapa  akizungumza katika hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake.   Waziri  asiyekuwa na Wizara Maalum  Zanzibar  Machano  Othman Said  akizungumza wakati wa hafla ya kufuturisha wateja wa benki ya CRDB iliyofanyika mjini Zanzibar.  Wadau mbalimbali wakipata futari.  Wafanyakazi wa benki ya CRDB wakijumuika pamoja. Baadhi ya wateja wa benki ya CRDB katika hafla ya kufuturisha. Baadhi ya wateja wa benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo. Waziri  asiyekuwa na Wizara Maalum  Zanzibar  Machano  Othman Said akizungumza katika hafla hiyo. Meneja wa benki ya CRDB tawi la zanzibar, Nassor Uzigo akipata Chai.  Wafanyakazi wa benki ya CRDB wakishiriki katika hafla ya kufuturisha iliyofanyika mjini Zanzibar....