Posts

"GEREZANI KUMENIFANYA NIMJUE MUNGU VIZURI SANA"....HII NI INTERVIEW YA LULU MICHAEL

Image
Kwa mara ya kwanza muigizaji wa filamu, Elizabeth Michael aka Lulu jana alifanya interview ya kwanza tangu atoke gerezani January mwaka huu.  Lulu aliye na muonekano wa ‘udada’ zaidi alihojiwa jana kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV kinachoendeshwa na Zamaradi Mketema.   Katia interview hiyo, Lulu aliongea masuala mengi kuhusu maisha yake ya sasa, mipango yake na mengine lakini akidai kuwa hatopenda kuongelea suala la uhusiano wake na Kanumba kwakuwa anahisi bado hajawa tayari ila muda ukifika atafunguka mengi. Haya ni baadhi ya masuala aliyoyazungumza. Kuhusu uzinduzi wa filamu yake mpya Foolish Age Ninaplan kufanya uzinduzi kwaajili ya movie yangu, lengo kubwa la kufanya uzinduzi ni kwamba kwanza nitajiskia vizuri kukutana na ‘okay these are my fans’ kukutana nao sehemu moja. Kuna vitu sitaweza kuongea kwenye interview ntahitaji kuviongea mwenyewe kama mwenyewe.  Nitahitaji watu waone baadhi ya vitu vilivyopo kwenye movie. Movie inaitwa Foolish Age. Nitai...

NDUGU WATAZAMAJI TUNAOMBA RADHI KWA PICHA ZA AJALI HII MBAYA

Image
AJALI ZAENDELEA KUTUMALIZA WATANZANIA.....  Ajali hii ilitokea jana jioni  tarehe 02/07/2013, baada ya gari dogo lililokuwa linatokea maeneo ya Ubungo kwenda uelekeo wa Buguruni kumgonga mwenda kwa miguu aliyekuwa anavuka barabara katika maeneo Gereji (garage)... Damu ilimtoka kwa wingi sana mara baada ya ajali katika maeneo ya kichwani, na hapo ilipotokea ajali kuna kivuko cha waendeo kwa miguu Darubini Leo

MACHANGUDOA WAULAANI UJIO WA OBAMA....WANADAI HAUKUWA NA PESA IKILINGANISHWA NA ULE WA BUSH

Image
  Katika hali ilisiyokuwa ya kawaida,  machangudoa wameulalamikia ujio wa Rais Barack Obama kwa kile kinachodaiwa  kuwa  haukuwa na faida yoyote kwa kukosa dili za pesa. " Tumesikitishwa sana na ujio wa Obama kwani tulikuwa tumejipanga kupiga hela ndefu sana . "Bahati mbaya watu  wake tuliokuwa tunategemea kuwanasa walikuwa busy na wale  wa  mikoani  walizuiwa" Walisema akina dada hao.   Machungudoa hao wanadai  kuwa  kipindi cha Bush alipokuwa Rais ambaye alikaa nchini karibu wiki moja walinufaika sana ambapo wengi wao walijenga majumba kwa pesa za ziara ya Bush .

MAMA WA MIAKA 52 AKAMATWA KWENYE CHUMBA CHA MTIHANI AKIMFANYIA MTIHANI BINTI YAKE

Image
  Mwanamke mmoja mfaransa (52) amejikuta mikononi mwa polisi wa jiji la Paris katikati ya mwezi june, baada ya kukamatwa kwenye chumba cha mtihani akimfanyia mtihani wa Kiingereza mwanae mwenye umri wa miaka 19, huku akijiweka kisichana zaidi wasimshutukie. Ripoti kutoka nchini humo zinasema mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la Caroline D aliingia kwenye chumba cha mtihani akiwa amevaa skin jeans na viatu aina ya Converse ili aonekane kama mwanae. Lakini jicho makini la msimamizi wa mtihani lilimnasa mama huyo kwa kuwa msimamizi alikua tayari alishamuona mwanae wakati anafanya mtihani wa Philosophy, kwa hiyo akamshtukia mama huyo kwa muonekano wake na sura yake ya kiutu uzima. Msemaji wa Polisi wa Paris alisema mwanamke huyo alikiri makosa yake ya udanganyifu na kusema kuwa kiukweli yeye alikuwa anaweza zaidi Kiingereza zaidi ya mwanae. Mwanamke huyo anakabiriwa na mashtaka ya udanganyifu na anaweza kulipa fine isiyopungua £7,000. Lakini pia binti...

MTOTO WA MIEZI MINNE ATUPWA AKIWA HAI MAENEO YA BAMAGA

Image
  Huyu ndiye malaika wa Mungu aliyetelekezwa maeneo ya bamaga nje ya chuo cha ustawi wa jamii karibu na TBC hapa akiwa amebebwa na mmoja wa mfanyakazi wa ITV baada ya wasamaria wema kumleta ITV... Anayeonekana kwa nyuma ni mmoja wa vijana waliomuokota mtoto huyo  Baadhi ya wafanyakazi wa ITV wakimshangaa mtoto aliyetupwa. mchomeblog

HUU NI UJUMBE WA RAY C AKIWASHUKURU MASHABIKI WAKE KWA KUMUOMBEA MPAKA AMEPATA AHUENI TENA

Image
  Mwanadada Ray C leo hii kupitia ukurasa wake wa instagram ameachia ujumbe huu kwaajili ya mashabiki zake na kuwashukuru kwa support yao.

"NIMETEMBEA KWA WAGANGA WA KIENYEJI NA KUGUNDUA KUWA MTU ALIYENIROGA NI MSANII MWENZANGU"...STEVE NYERERE

Image
  Makubwa  yameibuka baada ya msanii  Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, kufungua kinywa na kusema kuwa ugonjwa wake si bure bali amepigwa kipapai. Akizungumza na mwandishi  wetu,Steve alisema kuwa kufuatia kusumbuliwa na ugonjwa wa ajabu kwa kipindi kirefu sasa na madaktari kushindwa kuelewa kila walipompima, staa huyo anaamini kuwa amerogwa na msanii mwenzake.   “Nimetembea kwa wataalamu wa mambo ya asili na kugundua hilo, sasa ninalazimika kuamini katika imani za kishirikina ingawa ni kitu ambacho muda mrefu nilikuwa nikikipinga sana  lakini kwa hili ninaamini kweli nimechezewa na ndiyo maana niko hivi hadi sasa,” alisema Steve bila ya kupepesa macho.   “Nashindwa kumtaja mhusika wa tukio hili kwa sasa ila mwenyewe atakuwa anajua ni kwa kiasi gani nimemgundua, nimejua kwamba wasanii hatupendani hata kidogo na wala hakuna anayependa mafanikio ya mwingine.   “Ipo siku nitamtaja ila leo ngoja niishie kusema kwamba nimechezewa na namshukuru Mungu kw...

"NAWACHUKIA SANA WASANII WA BONGO MOVIE MAANA NI WEZI WA WAUME ZA WATU"...AMANDA

Image
   MSANII wa filamu za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ amesema anawachukia sana wasanii wa kike wa Bongo Movie kutokana na tabia zao za kuchukuliana mabwana. Amanda alisema wasanii wengi wa filamu wana tabia za kuibiana mabwana kitendo ambacho kinamkera na kusababisha kuwachukia kwani wanavyofanya siyo heshima na inawaharibia sifa kwa jamii pamoja na kuichafua tasnia yao kwa jumla.    “Nawachukia na ndiyo maana sitaki kuwa na rafiki Bongo Movie kwa sababu wamekuwa na tabia mbaya sana mifano halisi ipo lakini siwezi kuitaja,” alisema. Mbali na hivyo, Amanda alisema kuna wasanii wawili wa kike walikuwa marafiki sana hata kwenye mitandao walikuwa wakiitana mawifi lakini hivi sasa hawaivi, kisa  kunyang’anyana bwana

MAMILIONI YA PESA ALIYOINGIZA DIAMOND KWENYE SHOW ZA MWEZI ULIOPITA ....

Image
  Staa wa Kesho, Diamond ameendelea kupiga hela kwa show nyingi zinazomfuata kila kukicha. Wingi wa show hizi unazidi kumfanya kuwa miongoni mwa wasanii wachache wa Tanzania wenye pesa nyingi zaidi. Tumejaribu kuangalia baadhi ya show alizofanya mwezi huu, atakazofanya mwishoni mwa mwezi huu na mwezi ujao ili kukadiria ni kiasi gani anaweza kuwa ameingiza. Baadhi ya show tunafahamu ni kiasi gani aliingiza huku zingine tukikadiria kutokana na jinsi anavyochaji.   Show ya nchini Comoro 22 June Katika show hii alisema alilipwa si chini ya dola 25,000 za kimarekani ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 38.   Show za Usiku wa wasafi Tabora 28 na 29 June Mara nyingi katika show za ndani Diamond hachukui si chini ya shilingi milioni 10 kwa show mbili huenda akawa amelipwa zaidi ya shilingi milioni 15. Show ya Tigo Mwanza 30 June Katika show za makampuni kama hizi Diamond hulipwa si chini ya shilingi milioni 10.   Kili Music Tour 2013...

GEORGE BUSH AMESHAANZA KAZI YAKE ILIYOMLETA... ...MKUTANO WA WAKE WA MARAIS UMEFUNGULIWA NA RAIS KIKWETE

Image
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Mstaafu wa Marekani Mhe George W. Bush na Mkewe Laura na Mama Salma Kikwete wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wake wa marais wa Afrika Mashariki leo July 2, 2013 katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mkutano wa wake wa marais wa Afrika Mashariki leo July 2, 2013 katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam. Wageni wakimsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua mkutano wa wake wa marais wa Afrika Mashariki leo July 2, 2013 katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.  PICHA NA IKULU

RAISI GEORGE BUSH ALIPOKUTANA NA RAIS OBAMA TANZANIA KABLA HAJAONDOKA

Image
  Rais Obama pamoja na Rais Bush walikutana leo Asubuhi katika Ubalozi wa Marekani uliopo jijini Dar es Salaam na kufanya tendo la kutoa heshima zao kwa Walipoteza Maisha pamoja na wale wote walioathirika katika shambulio la Ugaidi katika Ubalozi wao hapa nchini mwaka 1998.

KWA HERI BARACK ABAMA....KARIBU TENA NA SAFARI NJEMA

Image
Rais Barack Obama wa Marekani ameondoka nchini mchana huu kurudi nchini Marekani,baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili hapa nchini iliyoanza jana.... Rais Obama na mwenyezi wake Rais Jakaka Kikwete,leo walifanya ziara ya kutembelea mitambo ya kuzalisha umeme ya Symbion iliopo Ubungo jijini Dar es Salaam na kuzindua rasmi mradi huo.... Tunapenda  kuungana na  Rais Jakaya  Kikwete na  watanzania  wote  wapenda amani katika  kumshukuru Rais wa Marekani Barack Obama kwa  kuichagua  Tanzania... Pia tunawapongeza  watanzania  wote kwa kuonyesha umoja  wetu na hata  kuzika itikadi zetu za kisiasa   na   hata  kupelekea  TV zaidi ya 1000 duniani na radio zaidi ya  3000 duniani  kuitazama  Tanzania..

MAHAKAMA YAWATIA MBARONI WAPENZI WAWILI WALIOAMUA KUTALII WAKIWA UCHI

Image
Njemba moja, Stephen Gough aliyewahi kuwa mwanajeshi amekamatwa na polisi katika Jiji la Portsmouth, Uingereza baada  ya kukutwa na mpenzi wake wakidunda kutalii mitaani wakiwa uchi wa nyama. Mwanamke Melodine Roberts aliyefuatana naye aliachiwa na polisi kwa kuwa mara baada ya kuonywa kuacha tabia hiyo, aliacha lakini mpenzi wake huyo aligoma na hii ni mara ya 14 akifanya hivyo licha ya kufungwa jela huko nyuma.   Baada ya kugoma polisi walimfunga pingu na wakampeleka mahakamani moja kwa moja  ambapo Mwendesha Mashitaka, Simon Jones alisema Gough alikuwa amekiuka sheria na aliwahi kufungwa miaka sita na moja ya makosa yaliyosababisha  afungwe ni kutemba uchi wa mnyama hadharani.   Baada ya maelezo hayo, jaji aliyekuwa akisikiliza shauri hilo, Sarah Munro alisema kuwa kwenda jela kwa mtu huyo ndiyo ilikuwa njia pekee kwake kwa kuwa hilo ni kosa kubwa katika jamii ya Waingereza na ni ukiukwaji wa taratibu za umma wa sehemu hiyo.   Gough...

PICHA ZA MAMIA YA WANANCHI TOKA UBUNGO WAKISUBIRI MSAFARA WA RAIS OBAMA

Image

HUU NDIO UMATI WA WATU ULIOJITOKEZA ASUBUHI KATIKA BARABARA ALIYOPITA OBAMA KWENDA UBUNGO

Image

MKE WA OBAMA ATEMBELEA WAMA FOUNDATION NA KUKUTANA NA MAMA SALMA KIKWETE JIONI HII

Image
Mke wa Rais wa Markani mama Michelle Barack Obama akiwasili katika ofisi za Wanawake na Maendeleo WAMA  jioni hii wakati alipotembelea katika ofisi hiyo na kuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Mwenyekiti wa  WAMA Mama Salma Kikwete katika makao makuu ya taaisis hiyo leo... Rais Barack Obama na Mke wake Michelle Obama wako  katika ziara ya siku mbili ya kikazi nchini Tanzania wakiongozana  na watoto wao jioni hii .... Rais Barack Obama atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete na pia watazungumza na waandishi wa habari Ikulu kabla ya kuendelea na kazi zingine.   Mama Mchelle Obama akielekea katika lango kuu la ofisi za WAMA jioni hii.   Mama Michelle Obama akilakiwa na mwenyeji wake mama Salma Kikwete wakati alipowasili katika ofisi hizo kwa mazungumzo mafupi.   >Mama Michelle Obama akipozi kwa picha na mwenyeji wake mama Salma Kikwete    Wake wa viongozi wakipunga bendera kama ishara ya ku...