Posts

AFYA YA NELSON MANDELA BADO TETE

Image
Taarifa kutoka Ikulu ya Afrika Kusini zinasema kuwa hali ya kiafya ya rais mstaafu Nelson Mandela sio nzuri na kuwa imezorota katika saa 48 zilizopita. Baada ya kumtembelea hospitalini, mwanawe mkubwa wa kike Makaziwa, alisema hali inaonekana kuwa mbaya lakini akaongeza kuwa Mandela anaweza kuwasikia jamaa zake wanapomuita huku akijaribu kufungua macho yake. Makaziwe amesema “Nimekasirishwa sana. Kwa sababu Mandela ni kiongozi mashuhuri duniani, haimaanishi utu wake udhalilishwe pamoja na kuvuka mipaka kuingilia mambo yake binafsi. Hapa naona kuna ubaguzi wa rangi, huku vyombo vingi vya kimataifa vikivuka mipaka, ni kama ndege aina ya Tai au Vulture wanaosubiri Simba kumla mnyama aliomuwinda kisha wakimbilie mzoga. Wamevuka mipaka ya maadili. Wakati hayati Margaret Thatcher alipokuwa mgonjwa mbona sikuona, ukaribu wa vyombo vya habari kiasi ninachokiona kwa banangu? Ni kwa sababu hii ni nchi ya kiafrika. Wanahisi kuwa hapa wanaweza kuvuka mipaka w

CHUO KIKUU HURIA TANZANIA KITAMTUNUKU PhD RAIS OBAMA

Image
Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT),kimepanga kumtunuku Rais wa Marekani, Barack Obama Shahada ya Heshima ya Uzamivu kwa kutambua mchango wake kwa jamii husasani kwenye maendeleo ya kukuza uchumi. Akizungumza na waandishi wa habari jana,Makamu Mkuu wa chuo hicho,Profesa Tolly Mbwete alisema tuzo hiyo imethibitishwa na Baraza Kuu la Chuo hicho baadaye kupitishwa na Mkuu wa OUT, Dk Asha Rose Migiro. “Tumeangalia vigezo vyote muhimu ambavyo mtu anastahili kupewa tuzo kama hii na tukaridhika kuwa Rais huyo anastahili kutunukiwa,” alisema Profesa Mbwete. Kwa mujibu wa Profesa Mbwete, Rais Obama anakuwa mtu wa tano kutunukiwa tuzo hiyo baada ya kutanguliwa na Mwalimu Julias Nyerere, Rais wa kwanza mweusi wa Afrika ya Kusini, Nelson Mandela, Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Benjamin Mkapa. Alisema hadi sasa OUT imetoa shahada saba za heshima, ambapo kati ya hizo mbili walitunukiwa mwanataaluma kutoka Mareka

FILAMU MPYA YA AUNT EZEKIEL YAZUILIWA BAADA YA KUWA NA VIPANDE VYENYE KUCHOCHEA NGONO

Image
SERIKALI kupitia bodi ya filamu nchini imemkalia kooni mwigizaji, Aunt Ezekiel na kumtaka aondoe baadhi ya vipande vya sinema yake mpya iitwayo Scola vinginevyo haitaruhusiwa kuingia mtaani. Taarifa kutoka ndani ya bodi hiyo inayosimamia maadili ya sinema za Kitanzania, imeeleza kuwa Aunt aliipeleka  filamu hiyo ili ikakaguliwe kama zilivyo taratibu lakini bahati mbaya ikagundulika kuna ‘sini’ tatu ambazo zilitoka nje ya maadili ya mtanzania. “Kuna vipande vitatu ambavyo kimsingi vimevuka matakwa ya maadili ya Kitanzania hivyo hakuna jinsi, lazima avitoe kama anataka kuiingiza sokoni sinema hiyo,” kilieleza chanzo makini ndani ya bodi hiyo kilichoomba hifadhi ya jina. Kabla ya mwandishi wetu hajazungumza na Aunt, alimpata rafiki wa karibu na staa huyo ambaye alifafanua kuwa rafiki yake (Aunt) amekaliwa kooni na bodi hiyo lakini bado yupo katika mazungumzo kuona kama anaweza kuruhusiwa aendelee.   “Amejaribu kuwasihi ili kama kuna uwezekano iingie m

WATANZANIA WAISHIO MIKOANI WAPIGWA MARUFUKU KWENDA DAR WAKATI WA ZIARA YA RAIS OBAMA

Image
Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe amewashauri watu walioko mikoani kusitisha safari za kuja Dar es Salaam wakati wa ziara ya Rais wa Marekani, Barrack Obama kutokana na wingi wa wageni katika jiji hilo. Ugeni huo pamoja na ule wa viongozi kumi na moja kutoka nchi mbalimbali duniani watakaohudhuria mkutano wa kimataifa wa Smart Partnership utakaofunguliwa kesho na Rais Jakaya Kikwete kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, umesababisha kuimarishwa kwa ulinzi katika maeneo mbalimbali hasa katika hoteli za kitalii ambazo zimeanza utaratibu wa upekuzi kwa wageni wake. Akizungumza na katika mahojiano na Redio ya Clouds jana, Membe alisema jiji limefurika kwa wingi wa wageni.   “Hoteli na nyumba za wageni zimefurika wageni na magari mengi yamekodiwa. Kwa ujumla, huduma za kijamii zitakuwa shida,” alisema.   Rais Obama na mkewe Michelle watawasili nchini Jumatatu na tayari wapambe na maofisa usalama kutokana Marekani wameanza

ULINZI WA RAIS OBAMA JIJINI DAR NI BALAA....MITAMBO MBALIMBALI YA MAWASILIANO IMEFUNGWA UWANJA WA NDEGE WA KIA

Image
Maandalizi ya ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama nchini yanazidi kupamba moto huku maofisa wa usalama wa Marekani wakipiga kambi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Aidha, kutokana na ujio huo, Serikali imeagiza mashirika yote ya ndege kubadili ratiba zao za safari Julai Mosi, siku ambayo Rais huo atatua nchini. Jana, waandishi wetu walishuhudia pilikapilika za kuimarisha ulinzi katika uwanja huo jambo ambalo uongozi wa uwanja huo jambo wamelieleza kwamba halijawahi kutokea. Ulinzi haujawahi kutokea Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Moses Malaki alisema jana kwamba ratiba za uwanjani hapo zitabadilika kutokana na uzito wa ugeni huo. Alisema kwa kawaida anapokuja kiongozi mkubwa wa kitaifa katika uwanja huo hakuna ndege inayoruhusiwa kutua kwa kipindi cha nusu saa. “Ni kweli hali hiyo pia itakuwapo atakapokuja Rais Obama na safari za ndege zitabadilika

WATANZANIA WAISHIO MIKOANI WAPIGWA MARUFUKU KWENDA DAR WAKATI WA ZIARA YA RAIS OBAMA

Image
Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe amewashauri watu walioko mikoani kusitisha safari za kuja Dar es Salaam wakati wa ziara ya Rais wa Marekani, Barrack Obama kutokana na wingi wa wageni katika jiji hilo. Ugeni huo pamoja na ule wa viongozi kumi na moja kutoka nchi mbalimbali duniani watakaohudhuria mkutano wa kimataifa wa Smart Partnership utakaofunguliwa kesho na Rais Jakaya Kikwete kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, umesababisha kuimarishwa kwa ulinzi katika maeneo mbalimbali hasa katika hoteli za kitalii ambazo zimeanza utaratibu wa upekuzi kwa wageni wake. Akizungumza na katika mahojiano na Redio ya Clouds jana, Membe alisema jiji limefurika kwa wingi wa wageni.   “Hoteli na nyumba za wageni zimefurika wageni na magari mengi yamekodiwa. Kwa ujumla, huduma za kijamii zitakuwa shida,” alisema.   Rais Obama na mkewe Michelle watawasili nchini Jumatatu na tayari wapambe na maofisa usalama kutokana Marekani wameanz

SHILOLE AMTIMUA MDOGO WAKE BAADA YA KUJAZWA MIMBA AKIWA MIKONONI MWAKE

Image
STAA wa sinema za Kibongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ (pichani) amemtimua mdogo wake aliyekuwa akiishi naye aitwaye Mary baada ya kunasa ujauzito.   Chanzo makini kilicho karibu na staa huyo kimepenyeza habari kuwa, Shilole alifikia maamuzi hayo baada ya kumuonya binti huyo aachane na mwanaume aliyemjaza mimba hiyo lakini hakusikia hivyo akaona bora amtimue.   “Kamtimua baada ya kumuonya mara nyingi bila mafanikio akaona isiwe tabu bora aepuke aibu,” kilisema chanzo hicho. Alipoulizwa kuhusiana na ishu hiyo, mdogo huyo wa Shilole alikiri kutimuliwa na sasa amehamishia makazi kwa jamaa yake anayefahamika kwa jina la Tonny Montensi anayeishi Sinza, jijini Dar.

MILIONI 15 ZAHITAJIKA KWA MGANGA WA KIENYEJI ILI KUMRUDISHA KATIKA HALI YA KAWAIDA BAADA YA MAITI KUFUFULIWA UKO MKURANGA PWANI

Image
BINTI aitwaye Nuru Omari anayedaiwa kufariki dunia mwaka 2010 ameibuliwa hivi karibuni wilayani Mkuranga, Mkoa wa Pwani na mganga akiwa hai kwenye banda kuukuu. Binti Nuru Omari aliyeibuliwa. Tukio hilo limetokea kwenye Kijiji cha Kalole, Tarafa ya Kisiju, walayani humo. Kwa mujibu wa baba wa binti huyo, Omari Salum, mwaka 2010 ndugu wa mkewe aitwaye Nyasenene aliyekuwa akiishi Charambe Mbagala, jijini Dar alifika nyumbani kwake na kuwaomba wampe mtoto wao kwa ajili ya kwenda kufanya kazi za ndani ‘hausigeli’. Kijumba alimokuwa Nuru. Baada ya binti huyo kufanya kazi kwa muda mfupi aliugua malaria, baba mtu akapewa taarifa  na kufika Dar kwa ajili ya kumuona mwanaye  aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar. Mzee huyo amesema alikwenda Muhimbili na kufanikiwa kuzungumza machache na mwanaye huyo ambapo alikuwa akilalamikia maumivu ya tumbo.   Ndugu na majirani waliofika kumtazama Nuru. Mzee huyo alisema ilibi

MIKOROGO YAMUATHIRI WEMA SEPETU APOTEZA MVUTO....MICHIRIZI YAANZA KUPANDA USONI

Image
Matumizi mabaya ya vipodozi yameanza kumuathiri  wema  Sepetu  ambaye  ni  miss Tanzania  2006.. Wema  ambaye umri wake bado  haujamtupa  , hivi  sasa  anakabiriwa na tatizo la  ngozi  kutokana  na michirizi  kusambaa  mwili mzima  hasa  mapajani....  Kamera  zetu  si  mara  ya  kwanza  kumshuhudia  Mrembo  huyu  akizingirwa  na  uzee  kwani  miezi  kadhaa  nyuma  tuliwahi andika  habari  inayofanana  na  hii  lakini  ikielezea  zaidi  michirizi  ya  mapajani.... Tofauti  na  hivyo, hivi  sasa  michirizi  hiyo   imekimbilia  kifuani  na  mabegani  hali  inayoashiria  kwamba  siku  si  nyingi  itahamia  usoni... "Ukweli  Wema  Sepetu  sasa  amebaki sura  tu,mwili  umemtupa  kabisa .Nadhani  hii  yote  inatokana  na  matumizi  mabaya  ya  mikorogo" ...alisema  shuhuda  mmoja  akimtazama  Wema sepetu  aliyekuwa  jaji  katika  shindano  moja  la  umiss  jijini  Dar Baada  ya  kumsikia  shuhuda  huyo  akimtoa  kasoro  mrembo  huy

MWIGULU NCHEMBA NA MSIGWA NUSURA WATWANGANE NGUMI BUNGENI

Image
Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa na mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba jana nusura wachapane makonde baada ya kutupiana maneno ya kashfa, wakituhumiana kuhusika na mlipuko wa bomu uliotokea Jumamosi iliyopita mkoani Arusha. Tukio hilo lilitokea katika viwanja vya Hoteli ya St Gasper nje kidogo ya mji wa Dodoma, walipokwenda kwa ajili ya kuhudhuria semina ya wabunge wapambanaji na Ukimwi, ambapo baadhi ya wabunge wa Chadema walihudhuria, baada ya kutoonekana mjini humo tangu Juni 17 mwaka huu. Wabunge hao wa Chadema hawakuhudhuria kikao chochote cha Bunge kutokana na kwenda mkoani Arusha kwa shughuli mbalimbali, kutokana na mlipuko wa bomu uliotokea katika mkutano wao wa kuhitimisha kampeni zake za uchaguzi mdogo wa udiwani katika viwanja vya Soweto, Juni 16 jijini humo. Malumbano hayo yanatokana na Nchemba kuituhumu Chadema kuhusika na mlipuko huo, Juni 20 mwaka huu wakati a

HALI YA MANDELA NI TETE...ASHINDWA KUFUMBUA MACHO KWA SIKU KADHAA

Image
Mzee Nelson Mandela ameendelea kuwa katika hali mbaya hospitalini jana baada ya kubainika kwamba gari la wagonjwa lililombeba Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini kwenda hospitali limeharibika. Gari hilo la wagonjwa mahututi liliharibika wiki mbili zilizopita wakati Mandela alipokuwa akikimbizwa kwenye hospitali moja mjini Pretoria, na kumwacha 'njiapanda' kwa dakika 40. Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini alihamishiwa kwenye gari jingine la wagonjwa la hospitali ya kijeshi kumalizia safari iliyobaki ya dakika 50 kati ya Johannesburg na Hospitali ya Moyo ya Medi-Clinic. Msemaji wa Rais Mac Maharaj alisema: "Tahadhari zote zimechukuliwa kuhakikisha kwamba hali ya kiafya ya rais wa zamani Mandela haiathiriki na tukio hilo." Madaktari wanaomtibu Mandela waliridhika kwamba hakupata maumivu yoyote katika kipindi hiki, aliongeza Maharaj. Taarifa ya jana kuhusu afya ya Mandela inaonesha kwamba kuna mabadiliko kidogo katika hali ya shuj

MAAJABU: MTOTO AZALIWA NA MAKALIO MATATU, MAMA YAKE ALIA AKIOMBA MSAADA

Image
Maajabu  ya  uumbaji  yamemfanya  mama  mzazi  wa  Xiao Wei  ambaye  ni  mchina amwage  machozi  akiomba  msaada  wa  kunusuru  maisha  ya  mwanae   mwenye  umri  wa  miezi  7 aliyezaliwa  na  makalio matatu... Kalio  la  tatu  lipo  kama  mkia  mfupi, wenye  urefu  wa   sentimita  8  ( 8 cm ), katikati  ya  makalio  mengine  mawili. Akiongea   kwa  uchungu, mama  mzazi  wa  mtoto  huyo  amedai  kuwa  kwa  muda  mrefu  amekuwa  akiwaomba  madaktari  wafanye  upasuaji  wa  tako  hilo  lakini  wao  wamekuwa  wakimjibu   kuwa  hiyo  si  kazi  nyepesi  kama  anavyodhani.... "Tukilikata  litaota  tena, hivyo  hatutakiwi  kukurupuka  na  badala  yake  tutakiwa  kupata  muda  wa  kupitia  vitu  vingi  ukiwemo  mrija  wa  uti  wa  mgongo  ambapo  kalio  hilo  limejiegesha" ...Alisema  daktari  mmoja  akimjibu  mama  huyo

"TUNAJIANDAA KUIPINDUA NCHI ENDAPO SERIKALI HAITAWASHUGHULIKIA WATU WALIOFICHA MABILIONI USWISWI"...ZITTO KABWE

Image
Zitto  Kabwe  amefunguka  na  kudai  kuwa  kwa  sasa  wanajiandaa  kufanya  mapinduzi  ya  nchi   endapo   watu  walioficha    mabilioni  uswiswi    hawatashughulikiwa  ipasavyo.... Suala la baadhi ya Watanzania kuhifadhi mabilioni ya fedha nchini Uswisi limechukua sura mpya, baada ya tume maalumu kuwahoji vigogo 200 wakiwamo wabunge, wanasiasa na wafanyabiashara.    Habari zilizopatikana zinaeleza kuwa tume hiyo inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema tayari imeshafanya kazi hiyo kwa miezi miwili sasa.   Tume hiyo maalumu iliyoundwa na Serikali kwa Azimio la Bunge lililotolewa mwishoni mwa mwaka jana, inatarajiwa kukamilisha uchunguzi huo wakati wowote kuanzia sasa na kuwasilisha ripoti hiyo katika kikao kijacho cha Bunge. Zitto  Kabwe  anatoa  angalizo  katika  hatua  hiyo  ya jaji Werema   kwa  kusema  kuwa  hatua  hii  isiwe  "zima  moto"   na  daganya  toto  ili  kuwafumba  macho

NGONO KINYUME NA MAUMBILE ZAONGEZEKA TANZANIA ....WENGI WAO WANAFANYA KUONDOA MIKOSI

Image
Taasisi ya Kupambana na Ukimwi Nchini (Tacaids) imesema tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa vitendo vya ngono kinyume na maumbile vinazidi kuongezeka. Hayo yalisemwa jana na Dk. William Kafura, katika mkutano wa sita wa Chama cha Wabunge cha Kupambana na Ukimwi (Tapac). Alisema hiyo inatokana na imani za kishirikina kwamba wakifanya vitendo hivyo watapata bahati kwa kupandishwa vyeo. “Lazima tukubali tatizo lipo na tulitafutie suluhisho, utafiti upo umefanywa na Muhimbili, umefanywa na chuo kikuu cha Dar es Salaam, umefanywa na Tasisi ya Utafiti ya Ifakara,” alisema. Alisema pia wafanyabiashara wanaamini kwa kufanya vitendo hivyo watajirika wakati wanawake wanaamini kuwa watazidi kupendwa. Kwa upande wake Mwenyekiti wa TACAIDS, Dk. Fatuma Mrisho, alisema utafiti uliofanyika nchini unabainisha kuwa wanawake hawana uelewa wa kutosha juu ya kujikinga na maambukizi ya ukimwi. Akizungumzia suala la kujikinga na ugonjwa wa Ukimwi Dk. Mrisho alisema kuwa wanaume wana uelewa

KAULI YA MWIGULU KUHUSU BOMU LILILORUSHWA ARUSHA

Image
MWIGULU NAYE ADAI KUWA BOMU LILIRUSHWA NA CHADEMA...."KAMA SIO WAO, MCHUKUA VIDEO ALITAARIFIWA NA NANI KWAMBA BOMU LITARUSHWA???" Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Mwigulu Nchemba  amesema bungeni leo kwamba Chadema ilipanga kufanya shambulio la bomu kwenye mkutano wa Soweto jijini Arusha. Amesema hakuna jambo ambalo Chadema wamewahi kupanga wakashindwa. “Itakuaje mtu amechukua mkanda wa tukio la umwagaji wa damu bila kutikisika au mchukuaji kukimbia, haiwezekani- hiyo walipanga. “Inakuaje amechukua mkanda wa video kama mkanda wa harusi, yaani kama mkanda wa sendoff.? Amehoji Mwigulu huku wabunge wa CCM wakimuunga mkono kwa kupiga meza bungeni. Mapema wiki hii katika mkutano wa Chadema, mtu mmoja asiyefahamika alirusha bomu kwenye mkutano wa Chadema na kusababisha watu wanne  kufariki dunia na wengine 68 kujeruhiwa na kupelekwa katika Hospitali ya Mt Meru, Arusha.

"EDWARD LOWASSA ANAHUSIKA NA KUTEKWA KWANGU PAMOJA NI KIPIGO NILICHOPEWA"...NASSARI

Image
Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari amemtuhumu Mbunge wa Monduli Edward Lowassa kwamba anahusika na kipigo alichokipata kutokana na chuki aliyonayo kwake. Aidha amemtuhumu Spika wa Bunge, Anne Makinda kwamba naye ni miongoni mwa watu wanaomchukia pamoja na viongozi wengine wa Bunge, kwa kuwa hakuna kati yao aliyempigia simu au kumtumia ujumbe wa kumjulia hali kutokana na kipigo alichopata ambacho kimemsababishia maumivu makali. Akizungumza jana akiwa kwenye chumba alicholazwa katika Taasisi ya Tiba ya Magonjwa ya Mifupa na Ufahamu Muhimbili (Moi), Nassari alidai Lowassa ambaye amewahi kuwa waziri mkuu kabla ya kujiuzulu, amemchukia tangu alipomshinda mkwewe Sioi Sumari, kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge uliofanyika Aprili mwaka jana. Nassari aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Selian ya jijini Arusha kabla ya kuhamishiwa MOI, alidai kupigwa na kuchaniwa nguo na Green Guard wakati alipokuwa katika jitihada zake za kuhesabu kura kwenye

POMBE SI MAJI WAHENGA WALISEMA.....MWANAMKE AVUA NGUO NA KUCHEZA UCHI BAADA YA KUZIDISHA POMBE HUKO MBAGALA ZAKHEIM

Image
DADA mmoja ambaye jina lake halikuweza kujulukana mara moja aliuacha hoi umati wa watu waliokuwa kwenye baa moja hivi (jina kapuni) huko mbagala Zakheim mara baada ya kuvua nguo zote na kubaki uchi wa mnyama na hivyo kusababusha hali ya taharuki katika maeneo hayo.     Chanzo cha habari  kinadai kuwa dada huyo alifika maeneo hayo akiwa vizuri kabisa... Uchafu wake  ulianza baada ya yeye kunywa bia nyingi  mithiri ya mtu mwenye kiu ya maji .Pombe  ilipopanda kichwani, mrembo huyo alianza kukata mauno ovyo na  kusaula nguo mojamoja  mpaka  alipoyaanika na makalio yake..

PICHA ZA MAZISHI YA WAHANGA WA MLIPUKO WA BOMU HUKO ARUSHA

Image
  Picha za Mazishi ya mwenyekiti wa BAWACHA kata ya Sokoni I Judith William Moshi, aliye fariki kwa mlipuko wa bomu kwenye viwanja vya Soweto jijini Arusha siku ya kufunga kampeni za chaguzi ndogo tarehe 15.06.2013..

MTOTO AFANYIWA UPASUAJI KUONDOA MIGUU MIWILI YA ZIADA

Image
Mtoto wa miezi miwili wa kiume nchini Namibia amefanyiwa upasuaji wa aina yake baada ya kuwa amezaliwa akiwa na miguu minne.   Andrew Palismwe, anayetokea Caprivi, anaendelea vizuri na matibabu baada ya kufanyiwa upasuaji uliochukua masaa tisa kuondoa miguu miwili kwenye Hospitali ya watoto ya Red Cross War Memorial  iliyoko mjini Cape Town, Afrika Kusini. Mtoto huyo sasa anaendelea kupata nafuu kwenye Hospitali ya Windhoek Central nchini Namibia, imeripotiwa. Alizaliwa akiwa na miguu miwili ya ziada chini ya tumbo lake Aprili 6. Hali hiyo inadhaniwa kuwa ni matokeo ya mapacha ambao hawakukamilika.   Daktari wa Hospitali ya Windhoek Central, Clarissa Pieper alisema: "Hii ni hali ambayo mapacha wameungana pamoja na kufuatia mimba ya mapacha ambayo hawakutengana kabisa, lakini kuunda watoto wawili wanaokua ndani ya kila mmoja. Katika suala hili, mtoto mwingine hauendelea kikamilifu."   Mama wa Andrew, Ruthy Mutanimiye alisema katika hospitali hiyo kw

KAULI YA DAKTARI KUHUSU KUMRUHUSU NASSARI JOSHUA"NI MUONGO NA NI MNAKI KWANI APEWA KIBALI KISHA ASEMA.......

Image
UONGOZI wa hospitali ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) ya Selian jijini Arusha umekanusha vikali taarifa zilizotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Chadema John Mnyika kuwa serikali ilipeleka maafisa wa usalama hospitalini hapo kwa lengo la kumdhuru mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari pamoja na majeruhi wa mabomu waliolazwa katika hospitali hiyo na kusema ni uzushi mtupu. Mnyika alisema kufuatia kitendo hicho mbunge Nassari alipiga kelele (yowe) akiwa katika korido ya wodi namba 14 aliyokua amelazwa ili kuomba msaada baada ya maafisa hao wa usalama waliokua wamevalia mavazi ya kitabibu na kubeba vifaa vya kitabibu kumtundikia drip aliyohisi ilikua na lengo la kumdhuru ambayo aliitoa na kuitupa. Mnyika alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya mahakama kuu kanda ya Arusha wakati akisubiri wabunge wanne wa chama chake pamoja na wafuasi wao waliohusika na mkusanyiko usio halali katika viwan