Manji Ajitoa Yanga Rasmi

MANJI.jpgMwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji.
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Yanga, Yusuf Manji, amesitisha kuendelea na zoezi la kuikodisha timu na nembo ya klabu hiyo na kuwaambia wasaidizi wake, wasitishe mipango yote ya maendeleo waliyokuwa wameanza kuifanya.
Manji amewaambia wasaidizi wake kusitisha maandalizi ya Ligi ya Vijana ya Matawi ya Yanga, lakini amewaambia waandae siku rasmi ambayo atazungumza na vyombo vya habari na kuwaomba radhi Wanayanga ambao wamemuunga mkono muda wote.
MANJI AKILONGA BAADA YA KUPIGA KURAYusuf Manjiakiongea na wanahabari.
Habari za uhakika ambazo Championi Jumatano limezipata, zinasema Manji alizungumza na wasaidizi wake jana mchana ikiwa ni dakika chache baada ya TFF kufanya mkutano na waandishi wa habari na kusema hawatambui suala la Yanga kuikodisha timu na nembo kwa Kampuni ya Yanga Yetu Ltd, kwa miaka 10.
“Leo alionekana ni kama mtu aliyekata tamaa au asiyefurahishwa na jambo. Amewaita wasaidizi wake na wamefanya kikao, hakikuwa kirefu sana.
“Amewaambia ameamua kuachana na masuala ya kuikodisha Yanga, pia amesema ameona ni vizuri kuachana na masuala ya mpira.
“Kilichomuudhi ni wale wasiotaka mchakato wa mabadiliko Yanga, lakini hawatoi hoja za msingi,” kilieleza chanzo.
“Wasaidizi wake walikuwa wameanza mchakato wa kutengeneza mfumo wa Ligi ya Vijana ya Matawi ambao ungeigharimu Yanga yetu takribani Sh milioni 280 kwa ajili ya vifaa, uendeshaji na kadhalika.
yangaaa-5
“Lakini kuna suala amelizungumzia la uchaguzi, hilo sijaelezwa vizuri. Huenda Yanga wakaitisha uchaguzi tena ili kuchagua viongozi yeye atakapotangaza kujiuzulu rasmi.
“Anaweza kufanya hivyo, yaani kutangaza kujiuzulu na kutangaza uchaguzi, pia kuwaomba radhi wanachama na mashabiki waliomuunga mkono muda wote.”
Juhudi za kumpata Manji zilianza jana saa 7 mchana baada ya kupata taarifa hizi; lakini ilishindikana.
Mmoja wa wasaidizi wake alipopigiwa, alituma ujumbe mfupi: “Nipo kwenye kikao, nitafute baadaye.”
Alipopigiwa Manji saa 9 alasiri, akapokea, ilikuwa hivi:
Championi: Hallow
Manji: Nani mwenzangu?
Championi: Tunafuatilia kuhusiana na uamuzi wako wa kujiuzulu Yanga, tunataka kujua ni kwenye klabu au zoezi la kukodisha pekee.
Manji: Tafadhali niacheni, kuweni kama binadamu. Nimechoka jamani, kuweni waungwana na mimi ni binadamu. Mniache nipumzike (simu ikakatwa).
yanga
Baadaye mmoja wa wasaidizi wake alipiga simu akitaka kujua alikuwa anatafutiwa kipi. Alipoulizwa suala la kujiuzulu kwa Manji, akasema:
“Sasa ndugu yangu unataka kuniingiza matatizoni, nafikiri tuache atangaze mwenyewe, naomba nipokee simu nyingine.” Kisha akakata simu.
Manji ambaye aliiongoza Yanga kwa misimu minne, mitatu ikifanikiwa kuwa bingwa Tanzania Bara, Kombe la FA na kucheza robo fainali ya Kombe la Shirikisho, ndiye kiongozi kipenzi cha Yanga wengi hasa wanaovutiwa na mafanikio ya timu yao.
Juhudi za kuendelea kumpata ili kuzungumza naye na kupata kila kitu kuhusiana na hili, zinaendelea.
Suala la kutaka kuikodisha timu ndiyo limezua zogo, huku wachache wanaopinga wakishindwa kuanika sababu hasa za msingi zinazowafanya wapinge.

Comments

Popular posts from this blog