JPM Kubadili Noti Kuwakomoa Walioficha Mabilioni Majumbani
Rais
John Magufuli amewataka watu walioficha fedha majumbani kuziachia
ziingie kwenye mzunguko vinginevyo anaweza kuamua kuzibadili ili wakose
mahali pa kuzipeleka.
Amesema watu hao wamekuwa na utaratibu wa kutoa fedha zao katika benki na kuzificha kwa kuogopa kuwa atabaini kiasi walichonacho, hivyo akawataka kuachana na tabia hiyo kwa sababu fedha hizo ni mali yao.
Amesema watu hao wamekuwa na utaratibu wa kutoa fedha zao katika benki na kuzificha kwa kuogopa kuwa atabaini kiasi walichonacho, hivyo akawataka kuachana na tabia hiyo kwa sababu fedha hizo ni mali yao.
Akizungumza katika mkutano wa 14 wa mwaka wa wahandisi uliofanyika
katika Ukumbi wa Mlimani City jana, Rais Magufuli aliyetumia dakika 73
kuzungumza na wahandisi hao na kueleza mikakati na changamoto
zinazoikabili Serikali ukiwamo wizi na ufisadi, alisisitiza;
“Huu ujumbe ni kwa wale wanaoficha fedha, waziachie na wajiandae, naweza kuamua baada ya siku mbili tatu nabadilisha fedha na hizo zilizofichwa katika magodoro ziozee huko. Ni nafuu mzitoe mziweke katika mzunguko zikafanye kazi,” alisema.
“Huu ujumbe ni kwa wale wanaoficha fedha, waziachie na wajiandae, naweza kuamua baada ya siku mbili tatu nabadilisha fedha na hizo zilizofichwa katika magodoro ziozee huko. Ni nafuu mzitoe mziweke katika mzunguko zikafanye kazi,” alisema.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa na
mawaziri, naibu mawaziri, makatibu wakuu na wahandisi kutoka ndani na
nje ya nchi, Rais Magufuli alisema katika utawala wa Serikali ya Awamu
ya Tano hakuna fedha za bure.
Alibainisha kuwa kipindi cha nyuma,
fedha zilikuwa nyingi mitaani kwa sababu baadhi ya watu walikuwa wakiiba
fedha za Serikali, huku akitoa mfano wa jinsi mabilioni ya fedha za
watumishi hewa yalivyotafunwa, jambo alilosema sasa limedhibitiwa.
“Nyinyi wahandisi ni wachapa kazi,
huu ndiyo wakati wa kutajirika.Tumieni nafasi hii maana watu walizoea
kupata fedha za bure. Waliokuwa wanatafuta dili katika wizara hawapati
kitu na sasa nikijua mtendaji wa Serikali umepiga dili utaondoka tu,” alisema.
“Fedha za bure hazipo na ndiyo
maana thamani ya nchi na fedha yetu imeanza kuongezeka na mfumuko wa bei
umeshuka mpaka asilimia 5.1.”
Alisema wakati fulani akiwa anatoka mkoani Geita, mfuko wa saruji ulikuwa unauzwa Sh26,000 lakini sasa unauzwa Sh16,000.
“Wanaoficha fedha ni wachache. Watu
watapata fedha za kutosha kwa kufanya kazi. Wafikirie kufanya uwekezaji
wa viwanda vyao na nyinyi wahandisi muwe namba moja.”
Changamoto na mikakati ya serikali yake
Alisema licha ya Serikali kuamua kutoa
mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kutoka 87,000 hadi 137,000,
imebainika kuwa wilaya moja mkoani Arusha ina wanafunzi hewa zaidi ya
10,000 na wilaya nyingine iliyopo Mwanza ina wanafunzi hewa zaidi ya
8,000.
Kuhusu mapato ya Serikali, alisema
baada ya kuingia madarakani yalipanda kutoka Sh800 bilioni hadi Sh1.3
trilioni lakini wakati hayo yanafanyika, Serikali imebaini wafanyakazi
hewa zaidi ya 16,500 na kusema hiyo ndiyo Tanzana aliyoikuta.
Rais Magufuli pia alieleza mikakati ya
kununua meli mbili, kujenga reli ya kisasa, kukarabati viwanja vya
ndege na kufafanua sababu za Serikali kununua ndege mbili aina ya
Bombadier Q400, ambazo zimeshalipiwa asilimia 40.
“Hizi ndege hazili mafuta, kasi
yake nzuri, zinatua uwanja wowote hata wa changarawe. Wapo wanaoziponda
eti hazina kasi, kama unataka kasi kapande za jeshi,” alisema huku akicheka.
Huku akieleza jinsi wahandisi wa nje
wanavyotekeleza miradi kwa gharama kubwa, alisema katika bajeti ya mwaka
2016/17, Serikali ilitumia Sh100 bilioni kwa ajili ya kukarabati
viwanja saba vya ndege vya lami, lakini wapo waliotumia Sh105 bilioni
kujenga barabara ya kuruka na kutua ndege katika Uwanja wa Ndege Mwanza,
fedha ambazo ni nyingi.
“Uwanja wa ndege Dar es Salaam
unaokarabatiwa sasa, zimejengwa njia tatu (za kuruka ndege) na lile
jengo (la abiria) lakini zimetumia Sh650 bilioni na gharama hizo
zimewekwa na wahandisi. Tunahitaji kufanya uchunguzi, maana gharama hizi
ni kubwa sana, kwa nini Watanzania tunachezewa hivi?” alihoji na kuongeza, “Ni bora wangepewa wahandisi wa Tanzania wakala hizi hela.”
Alisema wahandisi wazawa wanaweza
kujipanga na kupata tenda ya kujenga reli ya kisasa, kujenga bomba la
gesi kutoka Tanga kwenda Uganda na hata kujenga viwanja vya ndege.
Wizi unavyofanyika sekta ya madini
Alisema katika sekta ya madini, nchi
inaibiwa na kutoa mfano jinsi dhahabu inavyochimbwa wilayani Kahama,
kisha wahusika kuchukua mchanga na kwenda nao nje ya nchi kwa ajili ya
kusafishwa.
“Kinachosafishwa huko nje
hatujawahi kukiona, wahandisi mmekaa kimya. Kuna uhakika gani katika
kontena kama hakuna kilo 200 za dhahabu ambazo wameziyeyusha na
kuzichanganya na mchanga? Hivi wahandisi tumeshindwa kuweka utaratibu wa
kubaini kilichomo katika mchanga? Tunashangilia mtu anasafirisha
mchanga na sisi tunakubali kuwa wanasafirisha mchanga, mchanga unaondoka
na viongozi wetu hata majeshi yetu na polisi unasindikiza mali yako.”
Alisema suala hilo pia linapaswa kuwa
changamoto kwa viongozi na wanasiasa na akahoji sababu za kila mgodi wa
dhahabu kuwa na uwanja wa ndege,
“Tena hizi ndege wakati mwingine zinaruka moja kwa moja. Sisi Watanzania ni watu wa ajabu sana.
“Nasikia Profesa Muhongo (Sospeter –
Waziri wa Nishati na Madini) atatoa mada katika mkutano huu, atueleze
kwa namna gani mchanga wetu utaacha kupelekwa nje? Katika vitu
vinavyoniumiza ni pamoja na hili. Haya mamchanga tuyashike tuangalie
kilichomo humo ndani. Tanzania tumechezewa na kuibiwa mno, nipo
serikalini najua. Kila mahali ni dili, ukigeuka huku dili, ukienda huku
dili, kila mahali ni dili tu,” alisema.
Siri ya kuteua wahandisi wengi serikalini
Rais Magufuli alisema, wakati akiomba
kura katika kampeni za Uchaguzi Mkuu uliopita, alinadi mkakati wa
kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda, lakini hakuwahi kusema watu
watakaomsaidia kwa sababu aliamini wahandisi hawatamtupa mkono katika
kufanikisha hilo.
Huku akifichua siri ya kujaza
wahandisi katika serikali yake, alisema taaluma hiyo ni muhimu katika
maendeleo ya nchi na kuwataka kuwatumia viongozi hao kujenga uchumi wa
Taifa, ikiwa ni pamoja na kuanzisha viwanda.
“Tusipotumia wahandisi kamwe
tusizungumze kuhusu maendeleo ya nchi yetu, tusahau. Nimeteua wahandisi
kutekeleza mambo kwa niaba ya wahandisi. Mnatumika kujenga uchumi wa
watu wengine. Jipangeni nawaunga mkono, anzisheni viwanda… kampuni zenu
na kupata kazi maana hakuna nchi duniani isiyotaka kujenga watu wake,” alisema. …
Comments
Post a Comment