Roma, Italia
Kiongozi
Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amewashangaza makahaba wa
zamani 20 alipowatembelea katika ziara ya kushitukiza kwenye makazi yao
yenye ulinzi mjini Roma. Papa Francis alizungumza na wanawake hao,
ambao baadhi yao walisafirishwa kutoka Afrika na maeneo mengine ya
Ulaya, kwa muda wa zaidi ya saa moja.

Wanawake
hao waliokolewa kutoka kwenye madanguro walikokuwa wametekwa na
mwanamume aliyekua akiwauza kama makahaba na sasa wamepewa makazi na
ulinzi katika jengo la ghorofa linalomilikiwa na kanisa katoliki katika
Mji Mkuu wa Italia.

Papa
Francis mwenye umri wa miaka 79 amekua akirejelea mara kwa mara kwamba
biashara ya kuwasafirisha binadamu “ni uhalifu dhidi ya binadamu”.

Papa
Francis aliketi na wanawake hao, wakiwemo wanaigeria saba, waromania
sita na wanne kutoka Albania, na kusikiliza habari zao kuhusu namna
walivyo lazimishwa ukahaba, ulisema utawala wa Vatican.

Wengine watatu katika kundi hilo wanatoka Italia, Tunisia na Ukraine.

Wote
pamoja walikua na umri wa takriban miaka 30 na ”walinyanyaswa sana
kimwili” na sasa wanaishi chini ya ulinzi, umesema uongozi wa Vatican.

Kwa
ahadi za ajira, wanaofanya biashara ya kuwasafirisha binadamu huwaleta
wanawake Italia na nchi nyingine za Ulaya magharibi , lakini baadae
huwalazimisha kuingia ukahaba.

Papa
Francis aliwatia moyo makahaba hao wa zamani “kuwa thabiti” wakati
wanapoanza maisha mapya kwa usaidizi wa kituo cha Papa Pope John XXIII.
Comments
Post a Comment