KONDA WA DALADALA ACHINJWA KAMA KUKU,UNYAMA WA KUTISHA

konda auawa kiamara (1)Amonike Isdori ‘Dulla’ enzi za uhai wake.
Na Waandishi Wetu, UWAZI
DAR ES SALAAM: Zama za mwisho! Kijana aliyefahamika kwa jina la Amonike Isdori ‘Dulla’ (22) mkazi wa Makondeko- Golani, Kimara jijini Dar ambaye ni kondakta wa daladala, hivi karibuni alichinjwa kama kuku na watu wanaodaiwa kuwa ni walinzi shirikishi (sungusungu).
konda auawa kiamara (5)Bibi wa marehemu akilia kwa uchungu.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea usiku wa siku ya Idd Mosi, majira ya saa 7 usiku ambapo marehemu inadaiwa alikuwa akirejea nyumbani kutoka kwenye sherehe za sikukuu, ndipo alipokutana na watu hao walioanza kumpiga kwa madai alikuwa mwizi.
Akizungumza kwa majonzi na waandishi wetu, mama mdogo wa Amonike, Janeth alisema; “Siku ya tukio niligongewa mlango usiku na kundi la watu kama 15, ambao sikuwafahamu wakadai wao ni sungusungu na wamemkamata mwanangu kuwa ni mwizi.
konda auawa kiamara (2)“Walikuwa wamemfunga Amonike kamba miguu na mikono huku utosini akiwa na jeraha kubwa na ametapakaa damu. Niliwaambia mwanangu siyo mwizi kwani hawakuwa na kidhibiti chochote, wakaondoka naye, nilipoanza kuwafuata wakanipiga na ubapa wa panga na kuniambia nitulie.
konda auawa kiamara (3)“Niliwaomba kama kaiba basi wampeleke polisi, wakakubali, lakini asubuhi nikaletewa taarifa kuwa wamemuua mwanangu kwa kumchinja kama kuku eneo la Golani Darajani,” alisema Janenth huku akilia.
Waandishi wetu walifanikiwa kuzungumza na viongozi wa eneo alilochinjiwa Amonike, lakini kila aliyeulizwa alikana kuwa eneo hilo si lake.
 “Kuanzia eneo la tukio, msiba ulipo siyo eneo langu kuna mwenyekiti mwingine, ila nashangaa wananilalamikia mimi, sijui kitu kiukweli, tukio hilo nimelisikia kama ulivyolisikia wewe,” alisema mmoja wa viongozi hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Mtoi.
konda auawa kiamara (4)Hata hivyo, wananchi wa Mtaa wa Makondeko wanamtuhumu kiongozi huyo wa Mtaa wa Golani kuwa amekuwa akihusika kwa kuwabeba sungusungu ambao wamekuwa wakifanya mauaji mtaani hapo mara kwa mara.
konda auawa kiamara (6)Alipotafutwa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Christopher Fuime alisema hakuwa na taarifa za tukio hilo na kuahidi kulifuatilia. Jalada la tukio hilo lilifunguliwa katika Kituo cha Polisi Kimara kwa kumbukumbu namba KIMARA/9898/2016- MAUAJI.
konda auawa kiamara (7)Aidha, wananchi wa eneo Makondeko wameiomba serikali kuangalia kwa undani suala hilo kwani kuuawa au kuchinjwa kwa vijana wa mtaa huo limekuwa ni suala la kawaida kwani kuna vijana wawili pia walishauawa. Amonike alizikwa Julai 9, mwaka huu katika Makaburi ya Golani, Kimara jijini Dar.

Comments

Popular posts from this blog