Watu 3200 wakusanyika na kupigwa picha za utupu!
Hull, Uingereza
WATU zaidi ya 3200 wamekusanyika
na kusherehekea utamaduni wao wakiwa kwenye huku wakiwa wamevua nguo
zao zote (utupu) katika Mji wa Hull, Uingereza ikiwa ni tukio la
kusherehekea mji huo kama Mji wa Utamaduni.
Katika tukio hilo lilitokea Jumamosi
ambapo washiriki walijipaka miili yao rangi ya bluu-baharina kisha
kupigwa picha wakiwa katika maeneo mashuhuri jijini humo kama sehemu ya
mradi uliopewa jina Sea of Hull.
Mradi huo unatekelezwa na mpiga picha Spencer Tunick na unadhaminiwa na taasisi ya Sanaa ya Ferens Art Gallery.
Picha
zilizopigwa siku ya tukio hilo, zitawekwa na kuoneshwa kwa umma wakati
wa tamasha ya sanaa ya 2017 itakayoendelea kwa mwaka mmoja.
Tunick,
anayetoka New York, amewahi kupiga picha za watu wengi wakiwa uchi
Sydney Opera House, Place des Arts mjini Montreal, Mexico City na mjini
Munich nchini Ujerumani Germany.
“Mavazi ni Sanaa ya mtu mwingine,” anasema.
“Fashoni ni Sanaa. Kwa kuondoa hilo (mavazi), nitakuwa nafanya kazi na usawa na maumbile katika umaridadi wake.”
Comments
Post a Comment