Meli ya Mizigo Yazama Unguja

boti
Zoezi la uokoaji likiendelea eneo ilipozama meli ya MV Happy.
Meli ya mizigo iitwayo MV Happy iliyokuwa ikitokea jijini Dar es Salaam kwenda Zanzibar imezama leo asubuhi kwenye Bahari ya Hindi eneo la Chumbe, Unguja.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo ni kwamba meli hiyo ilianza kuzama majira ya saa 10 alfajiri na kufikia saa moja asubuhi ilikuwa imezama kabisa ndani ya maji.
boti 2
Wananchi wakishuhudia zoezi la uokoaji.
Mpaka sasa hakuna vifo vilivyoripotiwa bali mizigo iliyokuwemo kwenye meli hiyo ndiyo iliyozama.
Taarifa zaidi zitaendelea kuwajia kupitia tovuti hii.

Comments

Popular posts from this blog