Msalaba wa ajabu wamshangaza mama Kanumba


IMG_0497Mama wa staa wa sinema za Bongo, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa akiwa makabulini.
DAR ES SALAAM: Jambo limezua jambo! Baada ya hivi karibuni barua yenye ujumbe mzito kukutwa kaburini kwa aliyekuwa staa wa sinema za Bongo, marehemu Steven Kanumba, limezuka  jipya ambapo kitu kilichopo kaburini kinachodaiwa ni msalaba (kilichozungushiwa duara pichani) kimemshangaza mama wa Kanumba, Flora Mtegoa.
Kitu hicho cha chuma chenye umbo la pembe tatu katikati kikiwa na alama ya msalaba, kwa juu kuna picha ya Kanumba, chini kuna maandishi ya DJ na katikati maandishi ya RIP SCK kilizua gumzo hivi karibuni kwenye kumbukumbu ya marehemu kutimiza miaka 4 ambapo baadhi ya watu waliohudhuria Makaburi ya Kinondoni alikozikwa walipigwa butwaa.
Baadhi yao walisema chuma hicho kilitengenezwa kwa mfano wa alama mojawapo ya imani ya Freemason ambayo baada ya kifo chake, kuna watu walihusisha kifo hicho na imani hiyo.
IMG_0439Muonekano wa msalaba huo ukiwa juu ya kabuli la marehemu Kanumba.
“Duh! Jamani hebu angalieni kile chuma,  mimi nimekuwa nikikiona kila mara ila sijui ni nini maana kwenye makaburi mengine hakuna. Ukiangalia vizuri kimetengenezwa kama alama ya Freemason ya bikari lakini kati kama msalaba.
“Inawezekana yale yaliyozungumzwa wakati wa kifo cha Kanumba ni kweli kwamba alikuwa Freemason ndiyo maana watu walikuwa wengi sana kwenye msiba,” alisikika msanii mmoja akijadiliana na mwenzake makaburini hapo.
Baada ya  kutokea kwa gumzo hilo, gazeti hili lilimtafuta mama Kanumba na kumuuliza ambapo alisema hata yeye hajui aliyeweka kitu hicho na hafahamu kina maana gani bali huwa anakiona tu hapo kaburini na kimekuwa kikimshangaza.
“Sijui chochote kuhusiana na hicho kitu na huwa nakiona tu lakini sijui aliyepeleka pale na sijui kiliwekwa lini maana ni muda mrefu kila nikienda nakiona, mwenyewe nashangaa sana,” alisema mama Kanumba.
Mdogo wa Kanumba ambaye enzi za uhai wake alikuwa akifanya naye kazi kwa karibu, Seth Bosco yeye alipoulizwa alikiri kufahamu aliyeweka chuma hicho na sababu yake.
“Haa! Hicho chumba hakihusiani na Freemason. Aliyeweka ni dogo mmoja ambaye alikuwa ni mshkaji sana wa marehemu Kanumba (hakumtaja jina).
“Huyo dogo alikuwa kwenye idara ya masoko pale Steps na aliweka tangu mwaka 2012 mara tu baada ya Kanumba kuzikwa,” alisema Seth.
Alipoulizwa aliyekuwa Katibu wa Bongo Muvi wakati Kanumba anakufa, William Mtitu  alisema:
“Ukiondoa ukatibu wa Bongo Muvi mimi nilikuwa pia katibu wa mazishi ya Kanumba. Vitu vingi nilikuwa naratibu hiki kitu nimekuwa nikikiona muda mrefu lakini huwa sijui ni nini na kwenye makaburi mengine hakuna.
“Familia itakuwa inajua maana wakati wa kujenga kaburi wao ndiyo walilisimamia. Kile kitu kinashangaza sana kwani siyo msalaba wala nini na ni vigumu kujua zile alama zinamaanisha nini.”

Comments

Popular posts from this blog