Tumekwishaa! Poda Zadaiwa Kusababisha Kansa
Boniphace Ngumije na Gladness Mallya, RISASI Mchanganyiko
DAR ES SALAAM: Kuna neno moja tu
linaloweza kusemwa kwa sasa, kuwa tumekwisha, baada ya kubainika kuwa
poda iliyotumika kwa miaka mingi nchini, ambayo ni maarufu kama
Johnson’s Baby Powder inadaiwa kusababisha kansa ya kizazi inayoleta
maafa ikiwemo vifo.
Taarifa zilizopatikana kupitia mitandao
ya internet, zinadai kwamba kampuni inayotengeneza poda hiyo ya Johnson
and Johnson ya Marekani, Februari 25, mwaka huu ilihukumiwa kulipa faini
ya kiasi cha dola milioni 72 (sawa na shilingi bilioni 144) katika
Mahakama ya Missouri kama fidia kwa mwanamke mmoja aliyefariki dunia kwa
kansa ya kizazi iliyotokana na matumizi ya vipodozi hivyo.
Familia
ya mwanamke huyo, Jacqueline Fox ilitakiwa kulipwa kiasi hicho cha
fedha baada ya mahakama kuridhika kuwa ugonjwa na kifo chake kilitokana
na matumizi ya vipodozi hivyo kwa zaidi ya miaka 35, akitumia poda
pamoja na losheni ya bidhaa hiyo.
Kampuni hiyo ya Johnson & Johnson
ilikabiliwa na tuhuma kwamba kwa miongo mingi, kwa lengo la kufanya
biashara zaidi, haikuwaonya wateja wake kuwa miongoni mwa viungo
vinavyotengeneza bidhaa hiyo, vinasababisha kansa. Zaidi ya kesi 1000
zimefunguliwa huko Missouri na 200 New Jersey, zote zikiilalamikia
bidhaa hiyo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu
Fox, aliyeishi Birmingham, Alabama,
alisema alitumia Baby Powder na losheni kwa kiwango kikubwa kwa takriban
miaka 35, kabla ya kugundulika kuwa na kansa miaka mitatu iliyopita.
Alifariki Oktoba mwaka jana akiwa na umri wa miaka 62.
Jere Beasley, ambaye ni wakili wa
familia ya Fox, alisema kampuni hiyo ilitambua kuwa inawaongopea wateja
wake na mamlaka zinazohusika na vipodozi, wakati akizungumza na
waandishi wa habari.
Msemaji wa kampuni hiyo, Carol Goodrich, alionyesha masikitiko yake kwa hatua hiyo, akisema kwa miaka yote, walitambua kuwa ni jukumu lao kuhakikisha afya na usalama wa walaji wa bidhaa zao.
“Tunaumia pamoja na familia ya mlalamikaji, lakini siku zote tuliamini bidhaa zetu ni bora kutokana na ushahidi wa kisayansi.”
Msemaji wa kampuni hiyo, Carol Goodrich, alionyesha masikitiko yake kwa hatua hiyo, akisema kwa miaka yote, walitambua kuwa ni jukumu lao kuhakikisha afya na usalama wa walaji wa bidhaa zao.
“Tunaumia pamoja na familia ya mlalamikaji, lakini siku zote tuliamini bidhaa zetu ni bora kutokana na ushahidi wa kisayansi.”
Ushahidi wa kisayansi unaoonyesha kiungo
kinachosababisha kansa katika vipodozi hivyo siyo jambo la kificho,
kwani kimemo kimojawapo kilichopatikana kutoka kwa mshauri wa kitaalamu
aliyeajiriwa na kampuni hiyo kilisema ‘mtu yeyote atakayepinga uhusiano
wa matumizi ya talc (kiungo hicho) na kansa ya kizazi ni sawasawa na mtu
anayepinga hadharani uhusiano kati ya uvutaji sigara na kansa’.
Gazeti hili lilikwenda hadi ofisini kwa
Mkemia Mkuu wa serikali ili kutaka kujua kama wana taarifa hizo, lakini
ofisa aliyeomba hifadhi ya jina lake kwa vile siyo msemaji, alisema
kiutaratibu, kazi hiyo inapaswa kufanywa na Mamlaka ya Chakula na Dawa
(TFDA).
Msemaji wa Mamlaka hiyo, Gaudensia
Simwanza alikiri kusajiliwa kwa vipodozi hivyo hapa nchini, lakini
akasema bado hawana taarifa za kuwepo kwa watu walioathirika kutokana na
matumizi ya poda hizo.
“Dawa ambazo zimesajiliwa hapa kwetu
zinatokea Afrika Kusini na Ufaransa, hazitoki Marekani. Kabla ya
kusajili, huwa tunafanya mawasiliano na mamlaka husika huko inakotoka
(FDA) ambao wanatueleza wamepaki kiasi gani na ubora wake.
“Tunaisajili dawa baada ya kupokea
banchi ya kwanza, sasa baada ya hapo mwagizaji anaendelea kuileta tu,
sasa kwa maelezo yako, itabidi tuingie kazini kuangalia kama bidhaa ina
ubora unaotakiwa au la, baada ya hapo tutakuwa na la kusema,” alisema.
Alisema watakusanya upya sampo za bidhaa
hizo na kuzipeleka maabara ili zichunguzwe kwa mara nyingine. Endapo
zitakutwa na madhara zitapigwa marufuku na pia kuwasiliana na taasisi
husika Marekani ili kuwataarifu juu ya hilo pamoja na kuwasiliana na
kiwanda kinachozalisha bidhaa hizo.
source:GPL
source:GPL
Comments
Post a Comment