Flora Mvungi: Sijawahi kutumia ‘Uzazi wa mpango’, ‘Nazaa’ haraka haraka ili niwe huru na Uigizaji baadae




Staa wa Filamu Flora mvungi ambaye pia ni mke wa mwanamuziki H.Baba, amejibu shutuma zinazoongelewa na watu kuwa anazaa haraka haraka mno ambayo ni hatari kwa afya yake.
Kupitia kipindi cha Hatua Tatu cha Times Fm, Flora amesema kila mtu ana maamuzi yake kwa kile ambacho anakifanya na yeye ameamua kuzaa haraka haraka ili akirudi kwenye uigizaji awe huru zaidi na kazi yake.
“Nataka nifikishe watoto wanne, kwa hiyo sasa hivi naenda kupata watatu, nahitaji nikianza kuigiza niwe free zaidi sitakuwa na majukumu ya uzazi tena”
Akijibu swali kama amewahi kutumia au kuzingatia uzazi wa mpango, Flora amedai tangu aanze kujihusisha na uhusiano wa kimapenzi mpaka leo hajawahi kujaribu wala kutumia uzazi wa Mpango.
H.Baba na Flora wamejaaliwa kupata watoto wawili, Tanzanite na Africa huku wakitegemea kupata mtoto wa tatu hivi karibuni

Comments

Popular posts from this blog