Lulu adaiwa kulipiwa mahari
= Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Dar es Salaam: Wakati akikanusha vikali
taarifa mbaya za kuzushiwa kifo mwishoni mwa wiki iliyopita na watu
ambao alisema hajui lengo lao, habari ya heri ni kwamba, staa wa sinema
za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, (pichani) anaelezwa kuwa kwenye
shamrashamra za ndoa baada ya kudaiwa kulipiwa mahari na mfanyabiashara
maarufu jijini Dar (jina linahifadhiwa kwa sasa).
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini
ambacho ni mtu wa karibu wa Lulu, hivi karibuni mrembo huyo alilipiwa
mahari hayo kwa siri kwa kuwa mwanaume huyo hakutaka mambo hayo yafike
kwenye vyombo vya habari.
“Sasa mimi nawapa habari motomoto kuwa
Lulu amelipiwa mahari na mwanaume wake wa sasa lakini ishu nzima ilikuwa
kwa siri sana,” kilidai chanzo hicho na kuongeza:
“Shughuli nzima ilifanyika nyumbani kwa
Lulu (Mbezi-Beach, Dar) na sasa kinachoendelea ni taratibu za harusi
lakini jamaa (huyo mwanaume) hataki iwe na mbwembwe.
Lulu akiwa katika pozi.
“Ndiyo maana Lulu sasa hivi ametulia
siyo kawaida yake. Hata kwenye viwanja vya bata na shughuli za mastaa
haonekani kwa sababu anafanya mazoezi ya kukaa nyumbani kama mke wa
mtu.”
Habari hizo zilidai kwamba, Lulu
ataolewa ‘soon’ kwani maandalizi yamepamba moto kimyakimya chini ya
usimamizi wa mama yake, Lucresia Karugila.
Baada ya kunyaka madai hayo, Amani lilizungumza
na Lulu ili kumpongeza kwa kuchumbiwa na kulipiwa mahari kisha kusikia
neno lake juu ya ishu hiyo ambapo tofauti na matarajio ya mwanahabari
wetu, msanii huyo alikasirishwa na habari hizo huku akiweka wazi kuwa
mambo mengine katika maisha yake ni ya binafsi na kwamba siyo kila kitu
anaweka wazi kwa watu wengine.
“Hayo ni mambo binafsi, kwenye maisha
yangu siyo kila kitu cha kuweka wazi kwa watu,” alisema Lulu kisha
akakata simu kwa hasira.
Comments
Post a Comment