RAIS KIKWETE AFANYA UTEUZI MPYA,
RAIS
Jakaya Kikwete amemteua Awadh Massawe kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA). Rais alitangaza uamuzi huo Ijumaa
iliyopita wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa bandari mpya ya
Bagamoyo inayotajwa kuwa kubwa katika Afrika.
Akihutubia
katika hafla hiyo, Rais Kikwete alisema yeye alishamaliza uteuzi huo na
kumwambia Massawe afuatilie barua yake rasmi ya uteuzi. Kabla ya uteuzi
huo, Massawe alikuwa akikaimu nafasi hiyo tangu Februari mwaka huu,
huku akitajwa kufanikiwa hadi sasa kufanya mageuzi makubwa katika kuleta
ufanisi katika bandari hapa nchini.
Kabla ya
kukaimu nafasi hiyo, alikuwa Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam. Baada
ya kuwa Kaimu Mkurugenzi, alianzisha mikutano ya wadau yenye lengo la
kurudisha mahusiano yaliyokuwa yameyumba kati ya pande hizo mbili.
Mikutano
hiyo inayofanyika kila Alhamisi ya mwisho ya kila mwezi inalenga
kuhusisha wadau mbalimbali katika majadiliano ya jinsi ya kuboresha
ufanisi katika bandari ya Dar es Salaam.
Mwishoni
mwa Juni mwaka huu, TPA ilifungua ofisi ndogo katika mji wa Lusaka,
Zambia. Mafanikio mengine ya hivi karibuni ni kuanza kwa mfumo mpya wa
malipo kwa njia ya mtandao katika Bandari ya Dar es Salaam.
Inatarajiwa
kuwa baada ya kukamilika kwa ujenzi huo wa bandari ya Bagamoyo
unaotarajiwa kugharimu dola za Marekani bilioni 10, kutaongeza uwezo wa
bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara zinazohudumia tani milioni 12
za mizigo kwa mwaka, makasha 6,000 na kuajiri watu 3,200 na vibarua
1,500
Comments
Post a Comment