JK AMTAJA MUHUSIKA WA RICHMOND.
Kikwete
aliyasema hayo jana wakati akiwaaga wananchi wa Kigoma katika Uwanja wa
Lake Tanganyika na kumtaka Lissu amtaje mwenye Richmond.
“Endapo Tundu Lissu atashindwa kumtaja mwenye Richmond, nitatoka hadharani na kumtaja mwenyewe,” alisema Kikwete.
Kabla
ya mkutano huo, Rais Kikwete alifungua jengo la Mfuko wa Taifa wa
Hifadhi ya Jamii, (NSSF) ambalo limejengwa kwa Sh7 bilioni.
Akifungua
jengo hilo, aliwaomba wawekezaji na mifuko ya kijamii kuiga mfano wa
NSSF kwa kuwekeza katika sekta ya majengo kwa kuwa yanapendezesha mji.
Kadhalika,
Rais Kikwete alizindua jengo la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) pamoja
na nyumba 36 za bei nafuu zilizopo katika eneo la Mlole, Kigoma Mjini.
Richmond
Suala
la Richmond imekuwa moja ya ajenda za CCM katika kampeni za urais hasa
baada ya Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa aliyejiuzulu wadhifa huyo
kwa kashfa hiyo kuhamia upinzani.
Kila
sehemu ambako mgombea urais wa CCM anakwenda, suala hilo limekuwa
likiibuliwa, huku Lowassa akisema yeye hakuhusika, bali alijiuzulu
kuiokoa Serikali isianguke kwa kuwa ulikuwa uamuzi wa wakubwa.
Mgombea
urais wa CCM, Dk John Magufuli amekuwa akienda mbali zaidi akisema
akichaguliwa ataanzisha mahakama maalumu ya kushughulikia mafisadi
wanaosababisha umaskini nchini.
Bashe ataka mahakama ya mafisadi mapema
Wakati
Magufuli akiahidi mahakama hiyo, mgombea ubunge Jimbo la Nzega Mjini
(CCM), Hussein Bashe alimtaka mgombea huyo jana kuiwahisha mapema
iwezekanavyo akiingia Ikulu la sivyo atakuwa akihoji bungeni kila mara.
Bashe
alisema akipatiwa ridhaa na wakazi wa jimbo hilo kuingia bungeni
hatakuwa mbunge wa “ndiyo mzee” badala yake atakuwa akiisumbua Serikali
mara kwa mara likiwamo suala la kudhibiti ufisadi nchini.
“Umesema
utafungua mahakama ya mafisadi na majizi... nikuhakikishie waziri wako
wa sheria utakayemteua ajue atakutana na mtu anaitwa Bashe, kila
akiingia bungeni nitakuwa namuuliza kila mara upo wapi muswada wa sheria
ya kuanzisha mahakama maalumu ya mafisadi na majizi,” alisema Bashe na
kushangiliwa.
“Ni
lazima tufike mahali Taifa hili tuache kuwa watu wa porojo....Taifa
hili siyo maskini kuna wezi wapo bandarini. Najua saa hizi wanatafuta
biashara nyingine.”
Mgombea
huyo alisema wakati wa mchakato wa kumtafuta mgombea wa urais, kulikuwa
na makundi ndani ya chama akiwamo na yeye lakini baada ya kumpata, Dk
Magufuli tofauti zimekwisha.
Bashe
alikuwa miongoni mwa vinara wa kumuunga mkono mgombea wa urais wa
mwamvuli wa Ukawa kupitia Chadema, Edward Lowassa wakati akiomba ridhaa
ya kuteuliwa na CCM kabla ya kuhamia upinzani.
Hata
hivyo, jana alisema hataihama CCM kwa kuwa yeye na chama hicho
hawakukutana barabarani na kwamba ni muumini wa mabadiliko ndani ya
chama hicho.
Huku
akigusia tuhuma zilizowahi kuvuma za yeye kuwaambia wananchi wamchague
yeye halafu urais wampigie Lowassa, Bashe alisema wanaNzega watampigia
kura Dk Magufuli asilimia zote na zikipungua hazitazidi asilimia tano.
Bulembo amvaa Sumaye
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo amemvaa Waziri Mkuu wa
zamani, Frederick Sumaye na kumtaka aache kuchukua mshahara na kurudisha
walinzi wanaomlinda iwapo ataendelea kukitusi chama hicho kwamba
hakijafanya chochote tangu uhuru.
Akiwahutubia
wakazi wa Nzega jana, Bulembo alisema maisha yote ya kiongozi huyo na
familia yake yametengenezwa na CCM lakini anashangaa kuona sasa
anasimama kwenye majukwaa na kuwaeleza wananchi kuwa CCM haijafanya
kitu.
“...Analipwa
asilimia 80 ya mshahara wa Waziri Mkuu aliyepo madarakani, Mizengo
Pinda. Mpaka leo bado ana ulinzi na anahudumiwa na Serikali hii. Kwa
kupitia jukwaa hili la Nzega hebu Sumaye aache mshahara huo, arudishe
walinzi awe raia kama sisi,” alisema Bulembo.
Aliendelea
kurusha vijembe kwa kiongozi huyo akidai kuwa alinyang’anya ardhi ya
wana ushirika wa Mvomero mkoani Morogoro baada ya kutetereka.
Magufuli na michango ya shule
Dk
Magufuli jana aliendelea na kampeni zake mkoani Tabora na kuahidi kuwa
akiingia madarakani atafuta michango yote shuleni inayosababisha baadhi
ya wazazi washindwe kuwapeleka watoto shule.
Alisema
anatambua kuwa baada ya sera yake ya elimu bure kutoka darasa la kwanza
hadi kidato cha nne kuanza kutekelezwa iwapo atachaguliwa, kuna baadhi
watu wataanzisha michango isiyo na maana na kwamba atawashughulikia.
“Kuna
mambo ya kuwaambia wazazi peleka dawati, peleka dawati na hata kama
mtoto wa kwanza akishamaliza shule, ukimpeleka mwingine lile dawati
hulikuti. Ninafahamu haya yote nitayashughulikia lakini pia, hakuna
sababu shule kukosa madawati au viti wakati ipo karibu na miti, mbao
zipo, haya yote tutaangalia tukizingatia masilahi ya walimu wetu,”
alisema Dk Magufuli.
Akiwa
Bukene wilayani Nzega, Dk Magufuli aliwatahadharisha makandarasi
wazembe walioshindwa kukamilisha miradi yao kwa wakati akiwataka kufanya
hivyo kabla ya Oktoba 25 kwa kuwa yeye ni kiboko yao.
CHANZO MWANANCHI
CHANZO MWANANCHI
Comments
Post a Comment