MTOTO WA SOKOINE AFUNIKA JIMBO LA LOWASSA
Arusha. Binti wa Waziri mkuu wa zamani, Edward Sokoine, Namelock Sokoine
ameshinda kura za maoni kugombea ubunge Jimbo la Monduli kupitia CCM
huku mkwe wa Lowassa, Siyoi Sumari akishindwa Jimbo la Arumeru
Mashariki.
Namelock ambaye ni mbunge wa Viti Maalumu (CCM) alipata kura 29,582
akifuatiliwa na Loota Sanare aliyepata kura 8,809 na nafasi ya tatu,
ilichukuliwa na Lolinyu Mkoosu aliyepata kura 235 na Payani Leyani
akipata kura 226.
Arumeru Mashariki: Sumari aliyewania jimbo hilo kwa mara ya kwanza baada
kifo cha baba yake Jeremia Sumari na kushindwa na Joshua Nassari wa
Chadema alipata kura kura 3,664 dhidi ya 12,071 za John Pallangyo.
Mshindi wa tatu alikuwa ni William Sarakikya ambaye alipata kura 3,552
na wagombea hao waliwaacha mbali wapinzani wao wengine wanne.
Arusha Mjini: Katika Jimbo la Arusha Mjini, mfanyabiashara Philemon
Mollel ameshinda kwa kura 5,320, akifuatiliwa na mfanyabiashara mwingine
Justine Nyari aliyepata kura 1,894 na nafasi ya tatu, ilichukuliwa na
Moses Mwizarubi aliyepata kura 1,205.
Karatu: Dk Willibrod Lorry alishinda baada ya kupata kura 17,711, Rajabu Malewa (911), John Dado (745) na Joshua Mwambo (67).
Masele ambwaga Mlingwa
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Steven Masele
amembwaga waziri mwingine wa zamani, Dk Charles Mlingwa baada ya kupata
70,900 dhidi ya 669 za mpinzani wake. Wagombea wengine Abdallah Seni
alipata kura 391, Erasto Kwilasa (232), Hassan Athuman (164), Mussa
Ngangala (116), Hatibu Malimi (69), Wille Mzava (65) na Tara Omari (43).
Ushetu: Elias Kwandikwa (11,554) Isaya Sino (5,241) na Elfaidi Sikuli (2,007).
Kahama Mjini: Jumanne Kishimba (9,754), Kintoki Godwin (433), Nkuba
Charles (389), Bundala Maiko (284), Sazia Robert (257), Kapela Robert
(135), Ngalawa Adamu (126), Luhende Jerard (106), Malele Charles (91),
Tunge John kura (78), Mpangama Deogratias (57), Machunda Eliakimu (56),
Masanja Andrew (48) na Kambarage Masusu (28).
Msalala: Ezekiel Maige (11,575), Emmanuel Kipole (1,197), John Sukili
(962), Nicholas Mabula (668), Maganza Mashala (597), John Lufunga (29)
na Wankia Welema (14).
Solwa: Mbali ya matokeo ya kata moja ambayo imerudia uchaguzi, Ahamed
Salum alikuwa akiongoza kwa kura 17,485 akifuatiwa na Amos Mshandete
(2,028), Cyprian Mhoja (1,586), Luhende Richard (1,273), Kasile Paul
(637), Gabriel Shija (361), Renatus Chokala (357) na Hosea Somi (255).
Kishapu: Kabla ya matokeo ya kata tatu, Suleiman Nchambi alikuwa
akiongoza kwa kura 13,443, William Bonda (6,143), Kishiwa Kapale (500),
Limbe Moris (393), Heke Bulugu (356) na Timoth Ndanya (193).
Mawaziri watamba Kanda ya Ziwa
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Titus Kamani ameshinda kura
za maoni Jimbo la Busega baada ya kupata kura 10,697 dhidi ya mbunge wa
zamani wa jimbo hilo, Dk Rafael Chegeni aliyepata kura 9,661. Buchosa:
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba ameibuka mshindi kwa kupata
kura 26,368 dhidi ya Eston Majaliwa aliyepata 9,213.
Misungwi: Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga ameibuka
mshindi kwa kura 26,171, akimwangusha Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM,
Jacob Shibiliti aliyepata kura 7,009. Shomari Chalamila alipata kura
1,840, Dk Makene Doshi (1,339), Cleophace Jerome (1,051).
Ilemela: Mkuu wa Wilaya ya Iringa Angelina Mabula ameibuka mshindi
katika Jimbo la Ilemela kwa kupata kura 6,324 mbele ya Barnabas Mathayo
(3,562), John Buyamba (1,167) na wagombea wengine 16.
Tabora Kaskazini: Almasi Maige (9,466), Shaffin Sumari (6,392) na Joseph Kidawa (5,965).
Bariadi: Andrew Chenge (20,200), Masanja Kadogosa (2,986) na Cosmas Manula (270).
Meatu: Salum Mbuzi (13,180), Oscar Maduhu (2,988), Romano Thomas (358) na Donard Jinasa (350).
Itilima: Njallu Daudi (44,486), Simon Ngagani (2,759) na Danhi Makanga (814).
Comments
Post a Comment