RAIS JAKAYA KIKWETE APANGUA TENA WAKUU WA WILAYA
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amemteua Bwana Anthony Peter Mavunde kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa,
Mkoa wa Dodoma, kuanzia leo, Jumatatu, Mei 25, 2015.
Aidha,
Rais Kikwete amefanya uhamisho wa wakuu 10 wa Wilaya kwa nia ya kuongeza
ufanisi katika uongozi wa Wilaya mbali mbali nchini.
Katika
mabadiliko hayo, Rais Kikwete amemhamisha Luteni Edward Ole Lenga kutoka
Wilaya ya Mkalama, Mkoa wa Singida kwenda kuwa mkuu wa wilaya mpya ya
Kyerwa, Mkoa wa Kagera. Luteni Lenga anachukua nafasi iliyoachwa wazi na
Luteni Kanali Benedict Kulikela Kitenga ambaye alifariki dunia Aprili
20, mwaka huu, 2015.
Wakuu
wengine wa wilaya ambao Rais Kikwete amewahamisha ni Elizabeth Chalamila
Mkwasa kutoka Wilaya ya Dodoma kwenda Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa
Morogoro, Dkt. Jasmine Tisike kutoka Wilaya ya Mpwapwa kwenda Wilaya ya
Dodoma, Agnes Elias Hokororo kutoka Wilaya ya Namtumbo, Mkoa wa Ruvuma
kwenda Wilaya ya Tunduru, mkoani humo humo na Fadhili Nkurlu kutoka
Wilaya ya Misenyi, Mkoa wa Kagera kwenda Wilaya ya Mkalama.
Wengine
ambao wamehamishwa ni Chande Bakari Nalicho kutoka Wilaya ya Tunduru
kwenda Wilaya ya Namtumbo, Festo Shem Kiswaga kutoka Wilaya ya Mvomero
kwenda Misenyi, Darry Ibrahim Rwegasira kutoka Wilaya ya Karagwe, Mkoa
wa Kagera kwenda Wilaya ya Biharamulo, mkoani humo humo, Elias Choro
John Tarimo kutoka Wilaya ya Biharamulo kwenda Chunya, Mkoa wa Mbeya na
Deodatus Lukas Kinawiro kutoka Wilaya ya Chunya kwenda Wilaya ya
Karagwe, Mkoa wa Kagera.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
Comments
Post a Comment