BREAKING NEWZ:Muimbaji wa Chamber Squad Mez B afariki dunia


Muimbaji wa kundi la Chamber Squad, Maze B, amefariki leo saa nne asubuhi, kwa mujibu wa mtu aliyekuwa akimuuguza. 
 
Msanii huyo aliyewahi kufanya vyema na wimbo wake ‘Fikiria’ alikuwa amelazwa katika  hospitali ya Mwananchi mjini Dodoma.

Mez B aliyezaliwa kwa jina la Moses Bushagama alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Pneumonia.
 
Hivi karibuni aliongea na E-News ya EATV na alikuwa anaendelea vyema:
 
“Nilikuwa na tatizo la Pneumonia tokea mwezi wa 12 nikawa nipo vizuri nilivyo kuja tena Dodoma hali ikabadilika ndo nipo hospitali nimelazwa nasumbuliwa na maumivu ya kichwa na shingo,” alisema.
 
“Nategemea kuruhusiwa muda wowote na sasa hivi naendelea vizuri.” 
 
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

Comments

Popular posts from this blog

PICHA ZA UTUPU ZILIZOPIGWA NA MWANAFUNZI WA UDOM ILI KUTANGAZA SOKO LA MWILI WAKE. TAZAMA HAPA

ZITTO KABWE AWAPONDA LOWASSA NA MAGUFULI