JK:AKATISHA ZIARA YA MIZENGO PINDA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Waziri Mizengo Pinda amekatiza kwa muda, ziara yake katika Falme za
Kiarabu kwa maelezo kwamba ameitwa nyumbani na Rais Jakaya Kikwete kwa
shughuli maalumu.Waziri Mkuu ambaye yuko katika ziara ya kutembelea nchi za Falme za Kiarabu, ikiwa ni sehemu ya kudumisha ushirikiano na kutafuta wawekezaji, amekatisha ziara hiyo siku mbili baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema kujiuzulu kutokana na kashfa ya Escrow.
Waziri mkuu Mizengo Pinda.
Werema alijiuzulu juzi na Rais Kikwete akaridhia hatua hiyo, huku
umma ukisubiri hatua zaidi dhidi ya mawaziri na watendaji wa Serikali
waliotajwa katika sakata hilo.Katika barua yake ya kujiuzulu, Jaji
Werema alisema ushauri wake wa kisheria kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow
haukueleweka na hivyo kuchafua hali ya hewa.Kwa mujibu wa ratiba ya ziara hiyo, leo Waziri Mkuu alitarajiwa kufanya mazungumzo na washiriki wa maonyesho ya B2B pamoja na kutembelea maeneo mengine lakini ziara hiyo imefutwa na badala yake anaondoka asubuhi kurudi nyumbani.Baadaye leo Pinda alitakiwa kwenda Doha, Qatar kwa ziara kama hiyo hadi Desemba 23.
Baada ya kukamilisha jukumu aliloitiwa, Waziri Mkuu anatarajiwa kurejea Falme za Kiarabu Jumamosi kuendelea na ziara yake.
(Chanzo: BBC)
Comments
Post a Comment