KIJANA ALIKUFA AIBUKA AWA MSUKULE POLISI WAPIGWA BUTWAA
Kijana Kenedy
Onyango Augustine aliyedaiwa kupotea kimiujiza amerudi nyumbani akiwa
hai baada ya kudaiwa kuwa alikuwa amechukuliwa msukule.
KIJANA Kenedy
Onyango Augustine (22), mkazi wa Kitongoji cha Nyambogo Shuleni, Kata
ya Kitembe wilayani Rorya mkoani Mara aliyepotea kimiujiza amerudi
nyumbani akiwa hai baada ya kudaiwa kuwa alikuwa amechukuliwa msukule.Baba
mzazi wa kijana huyo, Augustine Oyoo alisema kuwa kijana wake alipotea
katika mazingira ya kutatanisha wakati alipokuwa anakwenda kulala
nyumbani kwa baba yake mdogo, Raubeni Oyoo kijijini hapo.‘’Kijana wangu
aliondoka saa tatu usiku Juni 3, mwaka huu baada ya kula chakula cha
usiku na kwenda kulala kwa baba yake mdogo alikokuwa akilala.“Ajabu
hakufika, asubuhi tulianza kumsaka bila mafanikio ndipo tulipochukua
hatua za kumtafuta kwa majirani lakini jitihada hizo hazikuzaa matunda
ambapo walituambia kuwa hawakumuona,’’ alisema Augustine. Aliongeza
kuwa, baada ya kushindwa kumpata walitoa taarifa ofisi ya serikali ya
kijiji na msako ulifanywa lakini kijana wake hakupatikana.
“Juni 6, mwaka huu usiku wa manane, tulimkuta kijana wangu akiwa amesimama nje ya nyumba yetu huku kapakwa matope mwili mzima.
“Tulimsemesha
akawa haongei jambo ambalo lilitushitua sana tukaamua kwenda kwa
Mwenyekiti wa Kitongoji, Michael Owino kutoa taarifa,” alisema mzazi
huyo.
Alisema
anaamini mtoto wake alifanywa msukule na jitihada zinafanywa na wazee
wa kimila kuhakikisha watuhumiwa wanapatikana na ikishindikana
atachanjiwa dawa mwilini mwake kurudisha fahamu pamoja na kujitambua ili
aweze kuongea.
Michael
Owino ambaye ni mwenyekiti wa kitongoji alikiri kupokea taarifa ya
tukio hilo na kuongeza kuwa alimshauri baba wa mtoto kupiga yowe ili
wananchi wakusanyike kwa msaada zaidi ambapo alifanya hivyo na kijiji
kikazizima kutokana na tukio hilo.
Diwani
wa kata hiyo, Thomas Patrick Lisa alisema kuwa tukio hilo tangu aingie
madarakani ni la nane ambapo watu wengine walipatikana wakiwa
wamechinjwa, hivyo kuhusishwa na ushirikina.
Comments
Post a Comment