HOT NEWS: WANANCHI WENYE HASIRA KALI WAMPIGA NA KISHA KUMCHOMA MOTO KIJANA MMOJA ALIYETUHUMIWA KUIBA NG'OMBE .
Mwili wa Kijana huyo Ukiwa umefunikwa na Majani Kabla ya Kuchomwa Moto
Akielezea Tukio Lilivyo tokea
Ng'ombe Walioibiwa
Wakichukua Mwili wa Kijana Huyo
Wakichukua Mwili wa Kijana Huyo
**********************
WAKATI
vyombo mbali mbali zikiendelea na jitihada za kuwaelimisha wananchi juu
ya madhara ya kujichukulia sheria mkononi hali hiyo bado ni tete mkoani
Mbeya.
Hali
hiyo imezidi kujitokeza baada ya Wananchi wenye hasira kali wa Mwasanga
Ivumwe jijini Mbeya kumpiga na kumchoma moto mwananchi mmoja ambaye
jina lake halikupatikana mara moja wakimtuhumu kwa Wizi wa Ng’ombe mmoja
na ndama.
Kwa
mujibu wa shuhuda wa tukio hilo ameuambia mtandao huu kuwa tukio hilo
lilitokea mapema leo asubuhi ambapo chanzo ni wizi wa Ng’ombe wa Kongoro
Mwakitalima mkazi wa Isyesye kata ya Ilomba.
Alisema
Ng’ombe huyo aliibiwa jana majira ya usiku ambapo mzee huyo alitoa
taarifa kwa majirani ambao asubuhi walijihimu kutafuta ambapo walipofika
maeneo ya Ivumwe walikutana na mwendesha boda boda ambaye aliwaambia amekutana na mtu akiwa anaswaga hiyo mifugo.
Alisema
baada ya kusikia hivyo waliamua kuanza kumfukuzia wakitumia bodaboda na
ndipo walipofika eneo la Mwasanga relini walimkuta mtuhumiwa akiwa na
hao Ng’ombe.
Alisema
Wananchi mbali mbali walikusanyika na kuanza kumshushia kipigo kutokana
na eneo hilo kukithiri kwa wizi wa mifugo lakini baada ya kipigo hicho
mtuhumiwa alionekana kuwa ngangari jambo lililowatia hasira na kuamua
kumchoma moto.
Shuhuda huyo aliendelea kusema baada ya kuanza kumchoma
lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida mtu huyo hakuweza kukata roho
hadi alipookolewa na Askari wa jeshi la polisi walipofika eneo la tukio.
Hadi tunaingia mtamboni hakuna taarifa zilizothibitisha kama mtuhumiwa huyo bado yuko hai ama amepoteza maisha.
Comments
Post a Comment