ALILAZIMIKA KUKEKETWA ILI ASOMESHWE.

ESTER CHARLES (16) ambaye anasoma kidato cha tatu katika shule ya Sekondari Rebu iliyoko wilayani Tarime mkoani Mara, alishindwa kujizuia na kudondosha machozi katika ukumbi wa kantini ya jeshi la polisi wilayani Tarime baada ya kueleza masaibu aliyokumbana nayo kwa kufanyiwa ukeketaji na wazazi wake.Anapofanyiwa ukeketaji huaminika kuwa mwanamke kamili aliyeondolewa mkosi na ambaye anastahili kuolewa. Wakati anafanyiwa ukatili huo, Esta alikuwa anasoma darasa la saba katika shule ya msingi Rebu, ambapo mara baada ya kukeketwa, anasema alipata maumivu makali ikiwa ni pamoja na kutokwa na damu nyingi.Anasema alikubali kufanyiwa ukeketaji na wazazi wake baada ya kufaulu mtihani wa darasa la saba na alikuwa na hamu ya kuendelea na masomo, lakini akapewa masharti na wazazi wake kuwa ili aendelee na masomo lazima akeketwe.
“Sikuwa na jinsi, nilijua ningeenda kukumbana na maumivu makali na kwasababu nilikuwa napenda  shule ilinibidi kukeketwa” anaeleza.
Kutoka maktaba ni moja ya nyenzo za ukeketaji.

Comments

Popular posts from this blog