ANGALIA PICHA ZA MWANAJESHI FEKI ALIYEKAMATWA LEO TANGA AKIMTAPELI DC

'Koplo' feki wa JWTZ akiwa ofisini kwa mkuu wa wilya.
 'Koplo' feki akijiandaa kupanda  kwenye gari kupelekwa kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi

 'Koplo' feki akiwa na pamoja na Luteni Yahya Wangwe na Mteule daraja la pili Albano Semfuko

Na Mashaka Mhando,TANGA
VIKOSI vya Ulinzi na Usalama Wilayani hapa,vinamshikilia Edwin
John Mponji (31) kufuatia kwenda ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga na
kujitambulisha kwamba yeye ni koplo wa jeshi la Wananchi JWTZ akitaka
kijana wake afanyiwe mpango wa kuingizwa Jeshi la kujenga Taifa. "Koplo" Mponji alikwenda ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga,Halima Dendego
Januari 16 mwaka huu siku ambayo Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani
hapa ilikuwa katika zoezi la kuwafanyia usaili vijana wanaotakiwa
kujiunga na jeshi la kujenga Taifa (JKT).
Akiwa katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya,Mponji alijitambulisha kuwa yeye
ni afisa wa JWTZ ambaye kwa sasa yupo kikosi cha 36 KJ Mkoani Pwani
ambapo aliambatana na kijana Emmanuel Joseph akitaka afanyiwe mpango ili apate nafasi.
 
Hata hivyo wakati akitoa maelezo hayo,Mshauri wa Mgambo wa Wilaya ya
Tanga,Sir Meja Albano Semfuko alimtilia shaka na kumjulisha Mkuu wa
Wilaya ambaye aliamuru ashikiliwe kwa mahojiano zaidi.
 
Akizungumza na waandishi wa habari,Mkuu wa Wilaya ya Tanga alisema
baada ya mahojiano ilibainika kuwa Mponji sio askari wa JWTZ ndipo
akalazimika kupelekwa nyumbani kwake mtaa wa Magomeni Jijini hapa
alipopekuliwa alikutwa na sare za JWTZ zikiwa na cheo cha koplo.
 
Alisema wakati akikamatwa,Mponji alikuwa amevaa kaptura ya jeshi la
Polisi lakini alipowekwa rumande ya kituo cha Polisi Chumbageni
alifanya njama za kuivua na kisha kumpa mahabusu aliyekuwa akitoka
ambaye alitoweka nayo.
 
Mponji alionyeshwa kwa waandishi wa habari akiwa amevalia sare ya
jeshi la Wananchi ambapo alipohijiwa alishindwa kutoa maelezo ya
kueleweka juu ya wapi alikokuwa amezipata sare hizo inagawa alikiri
kuwa aliwahi kumaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kikosi cha 841
KJ Mafinga.
 
Kufuatia tukio hilo,Mkuu wa Wilaya ya Tanga aliamuru Jeshi la Wananchi
kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kumfanyia uchunguzi wa kina ili
kubaini mtandao wake.

Comments

Popular posts from this blog