Tido afiwa na mama yake mzazi
- Get link
- X
- Other Apps
Mama
mzazi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications
Limited (MCL), Tido Mhando, Jessie (85), amefariki dunia Chang'ombe
jijini Dar es Salaam kwa ugonjwa wa moyo.
Akizungumza jana jioni, Tido alisema mama yake ( alifariki baada ya hali kubadilika ghafla).
"Alikuwa na matatizo ya moyo kwa siku nyingi, lakini hali ilibadilika ghafla, akafariki akiwa nyumbani," alisema.
Tido
alisema taratibu za mazishi zinafanyika nyumbani kwa marehemu
Chang'ombe, karibu na Klabu ya Sigara. "Tunafanya maandalizi, taratibu
zinasubiri watoto wa marehemu waliopo Uingereza, Marekani na Australia,
mwili utasafirishwa Tanga kwa maziko."
Ameacha
watoto wanane, enzi ya uhai wake alifundisha Shule za Msingi Mgulani,
Kibasila za Dar es Salaam. Nyingine ni katika mikoa ya Tanga, Dodoma,
Morogoro, Iringa, Arusha na Mwanza.CHANZO MWANANCHI
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment